Salam Jf!
Naomba msaada wa tatizo nililonalo ambalo naona siku zinavyozidi kwenda linaongezeka sana.
Huwa nikilala usiku nikishtuka usingizini nakuta mapigo ya moyo yanaenda kasi sana. Hadi muda mwingine nakuwa kama nataka kushindwa kupumua.
Naomba msaada kwa wataalamu wa Afya tafadhali
Km unakuwa umelala unajuaje mapgo yko ya moyo!:what:
Jichunguze mwenyewe kwanza kwa sababu unasema ni kila unaposhtuka usiku. Yawezekana unapataga manjozi mabaya ka ni hivyo, hayo tunayaitaga kuwa ni mapepo. Hospitali watakupima kila kitu, hakuna ugonjwa.
Nenda kwenye kanisa la kiroho, mwone mchungaji, atayakemea nayo yatakutoka. Utapata usingizi mzuri bila kushtuka usiku. Nimekupa tu ushauri
Nasubiri majibu,mimi tatizo hili limenianza sasa wiki ya pili,nikiamuka moyo unaenda kasi sana,wataalamu watusaidie jamani
Unatumia dawa za kuongeza nguvu za kiume??
Swali la muhimu. Unalala kwenye nyumba au stoo??
Hakika chumba ninacholala ni kifinyu sana,nimepanga vyombo humo humo na kila kitu changu,kwani vipi?
Hapo ndiyo pakuanzia sasa. Tafuta chumba kikubwa au punguza vitu ubakiwe na vichache tu ndani ili upate hewa ya kutosha. Hapo ni unalala stoo. Ndiyo maana unapata shida zote hizo. Unavuta hela finyu mbaya na chafu.
Teh! simple answers to difficult questions,ok thanks