Tatizo la mtindio wa ubongo (CEREBRAL PALSY)

Tatizo la mtindio wa ubongo (CEREBRAL PALSY)

Youngblood

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
19,433
Reaction score
56,810
1.Mtindio wa ubongo ni nini?.

Ni tatizo la kiuneurologia( mfumo wa fahamu) unaohusisha ubongo na mfumo wa neva za fahamu.
Tatizo hili hasa huathili sehemu ya ubongo ambayo inahusika na misuli ya mwili na tatizo hili hutokea kama ubongo haujakamilika katika ukuaji wake au kupata shida wakati wa kukifungua au baada ya kujifungua.

NB.Mara nyingi sana watu huhusisha tatizo hili na mambo ya kishirikina mfano watu wanasema wazazi wamefanya hivyo ili kujitajirisha kitu ambacho sio kweli.

2.SABABU ZA MTINDIO WA UBONGO.

Kuna sababu nyingi za mtindio wa ubongo ila nitawaeleza hizi kwa uchache, sababu hizo ni kama:-
» maambukizi anayopata mama wakati wa ujauzito
» kupata matatizo wakati wa kujifungua kama kumbana mtoto au kutumia mda mrefu wakati wa kujifungua au kujifungua kabla ya wakati( premature birth).
» kutokwa kwa damu kwenye ubongo wa mtoto( periventicular hemorrhage- intraventicular hemorrhage).
» kubadilika kwa mfumo wa vinasaba(genes) ambazo zinaweza kuathiri ukuaji wa ubongo wa mtoto.

3. DALILI ZA MTINDIO WA UBONGO.


Dalili za mtindio wa ubongo kwa kawaida huonekana sana katika kipindi cha umri wa miaka mitatu ya mwanzo ya ukuaji baada ya kuzaliwa. Dalili hizo ni kama:-
» spastic cerebral palsy - kukaza kwa misuli au misuli ya mwili kushindwa kufanya kazi ( hypotonia).
» Dyskinetic cerebral palsy - kulegea au kuishiwa nguvu kwa misuli.
» Ataxic cerebral palsy - kutokuwa na uwezo wa kuuzuia na kuufanya mwili anavyotaka ( balance and co-ordination problem).
Dalili hizi zinaweza kuonekana sehemu mbali mbali za mwili na inategemea na kiasi gani umeathiliwa na tatizo hili.wengine wanaweza kuwa na matatizo madogo madogo ila wengine inawapelekea hadi ulemavu.
Watoto wengi wenye mtindio wa ubongo huwa wanapata matatizo kama kifafa wakati mwingine pia kushindwa kutafuna na kumeza chakula, kutoweza kuongea ( dysarthria) , kupata choo kigumu au kwa shida( constipation), kutoweza kuzuia mkojo kutoka( urinal incontinence) , matatizo ya kuona na kusikia, matatizo ya kiunzi( skeleton) kama kupinda kwa uti wa mgongo ( curved spine) , mifupa kukaa sehemu tofauti kama mfupa wa paja( hip dislocation). N.k.
4.JINSI YA KUGUNDUA KAMA MTOTO WAKO ANA MTINDIO WA UBONGO.
Mtoto kuchelewa kukua kama watoto wengine.
Mtoto kuchelewa kukaa au kukaza shingo vizuri, viungo kukakamaa mara kwa mara au kulegea kupita kiasi(floppy)

Pindi tu unapogundua kuwa maendeleo ya mtoto wako sio mazuri katika ukuaji wake basi muone daktari haraka ili kujua ni nini tatizo, daktari anaweza akamfanyia uchunguzi kitaalam na kujua tatizo liko wapi.

Asante
Karibuni kama kuna mwenye swali au ushauri
2e5085bd02096bd3cb2020596a770d3a.jpg
 
mwanangu alifarki mwaka jana akiwa na tatizo hilo hilo,alikuwa na miaka mitatu,hakuwahi kutembea wala kutambaa,alijuwa anastuka stuka,nashukur sana kwa elimu yako ingawa watu walileta iman za kishirikina
 
mwanangu alifarki mwaka jana akiwa na tatizo hilo hilo,alikuwa na miaka mitatu,hakuwahi kutembea wala kutambaa,alijuwa anastuka stuka,nashukur sana kwa elimu yako ingawa watu walileta iman za kishirikina
Pole sana mkuu,binadamu ndivyo walivyo.
 
Vipi na mtoto kuchelewa kuongea inaweza kua ni dalili ya utindio wa ubongo?
 
Vipi na mtoto kuchelewa kuongea inaweza kua ni dalili ya utindio wa ubongo?
Hapana mkuu mtoto kuchelewa kuongea inaweza kuwa ni tatizo lingine tofauti na mtindio wa ubongo.
 
Back
Top Bottom