Tatizo la mtoto kujikojolea

Enugu

Member
Joined
Nov 7, 2017
Posts
70
Reaction score
72
Wadau habari ya sahivi! kuna mtoto wa jirani yangu kanasoma chekechea shida ya huyu mtoto ni kujikojolea yani akiwa amekaa tu mkojo unatoka wenyewe inafika kipindi hadi walimu wanampigia simu mzazi aje amchukue mtoto shule sababu hiyo, na ameenda hospital wamemwambia kwamba kuna vitu sijui vimelegea kwa maelezo alivyoniambia yeye sijui wanasema U.T.I ilimla sana ikaharibu mishipa! je kuna dawa yoyote jamani anaweza akatumia? au kuna njia gani nyingine kama ni oparesheni au nini kwa ajili ya kumasaidaia. msaada wenu madokta please
 
Madaktari hawakusema zaidi juu ya huyo mtoto baada ya kusema U. T. I ilimshambulia sana
 
Mimi sio Dkt. lakini uelewa wangu (nina material experience wa hili suala) hilo ni tatizo la kisaikolojia ambalo mara nyingi husababishwa na malezi, wazazi hao kama wako "very harsh" kwa huyo mtoto inaweza kuwa sababu, malezi "harsh" huharibu "self- esteem' ya mtoto na kupelekea mtoto kuwa "anxious" muda wote na hayo ndio baadhi ya madhara yake, mtoto asaidiwe kwa njia hiyo na kuwaona wanasaikolojia na madaktari wengine wa tiba.
 
mtoto anajikojolea au kujinyea kutokana na woga, anaogopa kusema na au kutoka kwenda msalani. ni vyema wamjengee saikolojia ya kuacha woga na kuona kwamba kujisaidia ni wajibu wa lazima.

hata watu wengine wakubwa akiwa "say"kanisani anakosa ujasiri wa kunyanyuka kwenda msalani mpaka mkojo unambaaaaana hatari in such a way bomu likilipuka mkojo utafyatuka, au akipiga chafya, kucheka ghafla. ni woga tu
 
Na vipi wale watoto wa miaka 10 lakini wanajikojolea kitandani?
Unapozaliwa mfumo wa fahamu unakuwa haujajitenga vizuri hivyo binadamu hawezi kujizuia haja kubwa na mdogo. Katika umri wa miaka miwili mtoto anaanza kuelewa haja inapokuja, kutokana na uchanga wa akili huwa kuna kujisahau tunaita ajali hutokea na akakojolea nguo alizovaa lakini akikumbuka anawahi. Huu ndiyo wakati wa potty training.

Huku uswahilini kwetu utazomewa na wenzako mpaka akili iingie. Miaka mitano mtoto anakuwa na uwezo wa kuamka usingizini mkojo ukimbana. Kibofu kikijaa ubongo hupata habari na usingizi kukatika.

Mtoto wa miaka saba akiwa bado. Anakojoa kitandani ni kuwa mfumo wa fahamu una matatizo na wataalamu wa afya ya akili wanaweza kukusaidia.
 
Huyo mzazi ampeleke mtoto kwa dr wa watoto afanyiwe check up kuanzia ya mfumo wa fahamu pamoja na kibofu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…