Tatizo la mtoto wako linaitwa kitaalamu ''Delayed Developmental Milestone'' Yaani kuchelewa kwa mtoto kukua kiuwezo kunakotakiwa kuendane na umri wake.
Tatizo hili linaweza kutokana na sababu mbalimbali kwa mfano,
1/Kuumia wakati wa kuzaliwa (Birth Injury/Asphyxia)
2/Madhara ya muda mrefu ya magonjwa(Disease complications eg, Meningeal siqulae)
3/Overweight.
4/Degedege kali au endelevu
5/Cerebral Palsy nk.
MASWALI MUHIMU
-Je mtoto wako alipata shida yoyote wakati wa kuzaliwa, mfano kuchelewa kulia, kushindwa kunyonya nk.
-Je alishawahi kuugua na kulazwa ili kutibiwa ugonjwa wa
uti wa mgongo, malaria kali?
-Je, mtoto wako ameshaweza kuongea kama watoto wenzake wa umri huo, kwa kutamka kwa uchache maneno matatu ya uhakika(mama, dada, baba)?
USHAURI
Ni vizuri ukajitahidi kutafuta kuonana na madaktari bingwa wa watoto(Paeditricians), au wataalam wa tiba kwa vitendo(Occupational therapiests) hawa wapo katika hospitali zote za rufaa na hata hospitali za serikali za mikoa. Ni tatizo linaloweza kutibika vizuri although it is gradual process.