Kwa maelezo niliyowahi kusikia na niliyosoma hapa, naamini coin ingesaidia ku-balance pressure ya nje ya kitovu dhidi ya pressure ya ndani wakati ukuta wa tumbo
(pale palipo kitovu) ukiendelea kufunga. Hata hivyo, ushauri wa
Riwa ni wa kuzingatiwa sana kwani kwa hakika madhara yanaweza kuwa makubwa.
Kuhusu kuzungushia plasta kwenye coin, daktari mmoja wa watoto bado alikataa utaratibu huu japo coin imezungushiwa plasta. Hata hivyo, alitoa njia mbadala akipendekeza kumvisha mtoto kaptula au bukta yenye mkanda mpana utakaofunika kitovu.
Ndugu
christmas ni vyema ukampeleka mtoto akaonwe na daktari kama ilivyopendekezwa hapa. Binafsi nimehisi huenda ulichokieleza sicho tunachodhani ndicho, kwani kitovu kuvimba na kitovu kutuna inaweza kuwa vitu viwili tofauti. Na je, kitovu kimeshapona kabisa kwamba hakuna dalili ya kidonda?