Tatizo la nyufa kwenye nyumba.

father-xmas

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2010
Posts
971
Reaction score
1,117
Heshima kwenu mabosi zangu.

Wakubwa nina nyumba nilijenga miaka michache iliyopita lakini kumekua kuna nyufa moja inajitokeza mara kwa mara.Nimeshapata watu wakisema ni wataalam wa kudhibiti nyufa lakini kila ikidhibitiwa inarudi baada ya miezi kadhaa.

Sielewi tatizo ni nini,wegine wanadai sababu niliijenga haraka sana(nilisimamisha msingi mpaka kupaua pamoja na milango na madirisha kwa miezi minne).

Kila fundi ninayemuita anaongea yake kisha anarepea na baada ya muda inarudi tena.

Wakuu naombeni ushauri nifanye nni kinachoweza kudhibiti huu ufa for good.
Najua humu tuna wataalam wengi wa mambo ya ujenzi mtanisaidia.

Thanks in advance.
 
Picha itasaidia,
nyufa nyingi zinasababishwa na aina ya udongo uliopo chini, kwani huo ndio unaamua namna ya ujenzi wa msingi, japo uzito wa nyumba kwa pande moja ukiwa haupo kwenye mlinganyo unaweza kusababisha hilo.
 
Picha itasaidia,
nyufa nyingi zinasababishwa na aina ya udongo uliopo chini, kwani huo ndio unaamua namna ya ujenzi wa msingi, japo uzito wa nyumba kwa pande moja ukiwa haupo kwenye mlinganyo unaweza kusababisha hilo.

Kwa sasa hivi kupata picha itakua ngumu kamanda wangu.

Udongo wa eneo ni mfinyanzi(mbezi temboni)

Mafundi wanadai ilitakiwa uwekwe mchanga wa kutosha wakati wa kujenga msingi.
Mchanga uliwekwa,ila kama ulikua wa kutosha hapo ndio siwezi kujua,ila fundi aliyenijengea alidai unatosha.

Kwa hiyo tuchukulie haukua unatosha,nifanyaje?
 
Bila picha itakuwa ngumu kupata ushauri sahihi
Kama unaijali nyumba yako kwanini ushindwe kutafuta picha wakati karibu kila sim sasa hivi ina Camera na USB Port.

Maana wewe unatoa maelezo ya kujitosheleza kwa muono wako ila kuna watu ni wazoefu wa kujua nyufa ya wapi inatokana na nini,kila nyufa ina sababu zake.

Ukiweka Picha ndio utaambiwa Sababu.

Maana hata hao mafundi hukuwalipa kabla ya kuja kuona kwanza nyumba ipoje na nyufa zipoje.
Sasa unafikira humu utapataje ushauri bila angalu watu kuona picha ya nyumba.
 
Tatizo liko kwenye vitu vifuatavyo;-
1.Msingi kuwa juu ya udongo usiofaa kwa ujenzi wa jengo.
2.Kina cha msingi kuwa kifupi kuliko uzito wa jengo.
3.Aina ya malighali zilizotumika kwa ujenzi na uwiano wa
uchanganyaji wa malighafi hizo.
4.Kupuuza gharama za kuweka jamvi (concrete ground floor
slab & beams) lenye waya mesh na nondo chini ya sakafu.
5.Zege hafifu kwenye lenta.
6.Paa kuwa kubwa kuliko uwezo wa matofari kuhimili hivyo
nyumba kusukumwa na upepo upande fulani.

Suluhisho

Wasiliana na wataalamu wa majengo kwa ushauri zaidi ikiwezekana
wapeleke site wakaangalie extent ya ufa/nyufa hizo.
Usiogope gharama kwani ni bora kutibu tatizo kuliko kuacha liendelee
na hivyo kusababisha mambo mengine yatakayo kughalimu zaidi.
Hongera kwa ujenzi.
 
Kama walivyosema wengine, picha ingeweza kusaidia kupata ushauri specific zaidi kupitia jukwaa hili. Hizo nyufa zipoje. Vertical, horizontal ama diagonal? Nyumba yako iliwekwa ground beam na lintel? Kama kuna ground beam na lintel, nazo zime crack? Mazingira ya nyumba yako kuna miti ya aina gani (foliage ipoje)? Miti ipo mbali kwa kiasi gani na nyumba yako? Nyumba yako in paa la aina gani? Sehemu ambazo paa na kuta zinakutana kumetengenezwaje (nazungumzia finishing ya eaves na overhang)? - zinaruhusu upepo kuingia ndani kati ya paa na ceiling?
 
Imgawa mm si mtaalam sana ila udongo wa mfinyanzi huwa ynasababusha sana nyufa. Kuna namna ya kujenga msingi kabla hujapandisha. Watu wa kiluvya pia wanalalamika sana na nyufa kutokana na mfinyazi.
 

Shukrani mkuu..nimekupata vizuri kabisa..nitafanyia kazi ushauri japo hao wataalam nishawaleta sana na kila mmoja anaahidi kufix tatizo ila badae linajirudia..Hopefully nitapata mtaalam anayejua anachokifanya maana hawa wengine nahisi walikua wanasolve kwa kuhisi tatizo.
 
Kwa sasa hivi kupata picha itakua ngumu kamanda wangu.

Udongo wa eneo ni mfinyanzi(mbezi temboni)

Huko Mbezi na Kimara karibu kila nyumba ina nyufa... Udongo wa mfinyazi una tabia ya kukakamaa na kujipasua. unapokakaamaa na kujipasua, lazima utaathiri nyumba na hatimaye inapata nyufa. Ni kufanya repair kila mara ndio dawa...Vinginevyo utakuja kujenga ukuta ndugu yangu.
 

Mkubwa hiyo nyumba imepangishwa,mimi siishi humo na niko mbali na iliko kwa sasa ndio maana nikajibu huko juu kuwa kupata picha kwa sasa ni vigumu.

Upepo hauingii ndani kati ya paa na ceiling.
Nyufa ni moja kubwa ipo horizontally.
Nyumba iliwekwa ground beam na lintel na yes zimecrack pia.
Nyumba haipo karibu na miti mikubwa zaidi ya midogo midogo ya maua.

Hata hivyo hili tatizo liko kwenye ukuta mmoja tu.Sio nyumba nzima inayosumbuliwa na nyufa.Ni kipande kidogo cha ukuta cha urefu wa kama miguu mitatu lakini kimekua kikijirudia kila kinapotibiwa.
 

Hujakosea ndugu yangu...Jirani zangu wengi nao kilio ni hicho hicho.
Nyumba ingekua inafaa kuhamisha ningeshaihamishia sehemu nyingine siku nyingi.
 
Imgawa mm si mtaalam sana ila udongo wa mfinyanzi huwa ynasababusha sana nyufa. Kuna namna ya kujenga msingi kabla hujapandisha. Watu wa kiluvya pia wanalalamika sana na nyufa kutokana na mfinyazi.

Ina sumbua sana...wengi wanasema kama wewe...udongo wa mfinyanzi ni nuksi sana..
 
.Nyufa ni moja kubwa ipo horizontally.
Nyumba iliwekwa ground beam na lintel na yes zimecrack pia.
Nyumba haipo karibu na miti mikubwa zaidi ya midogo midogo ya maua.
Mkuu, lintel na ground beam ni horizontal members katika heights tofauti.

Kama crack ni moja na ipo horizontal, si rahisi kuwa imepita kwenye ground beam na lintel kwa pamoja. Au ulikusudia kusema vertical (wima)? Horizontal cracks, mara nyingi zinasababishwa na lateral forces (misukumo ama forces zinaotoka kwa upande) na kusababisha sehemu moja ya ukuta kusukumwa kiupande tofauti na sehemu nyingine ya ukuta huohuo. Ni ngumu kujua kwa uhakika ni kitu gani hasa kinasababisha msukumo huo bila ya kufika site. Inaweza kuwa ni namna paa lilivyokaa ambapo inasababisha mzigo kuelemea kwenye ukuta mmoja zaidi (hasa kwa sababu unasema linajirudia) na kusababisha ukuta huo ku bend na hivyo ku crack.

Je upande ulio crack, ndio upande ambao upepo mara nyingi unatokea/unakwenda (windward/leeward)? Na je hiyo crack ni kubwa zaidi kwa ndani au kwa nje?-ama zinalingana? je ni crak inayoongezeka ukubwa?
 

Mkubwa hii crack ipo pale kwenye zege linalounganisha ukuta na msingi.Ipo horizontal mkuu kama nilivyosema mwanzo.
Hii crack inaongezeka ukubwa.Mara ya mwisho nilivyoenda kuangalia unaona kabisa tiles kwa ndani ya nyumba zimeacha ukuta,nilishituka sana maana mwanzoni nyufa ilikua inaonekana kwa nje tu.

Crack ni kubwa zaidi kwa nje.

Kuhusu uelekeo wa upepo nikikujibu kwa sasa nitakua nakudanganya,sina uhakika.

Labda niongezee,nyumba iko kwenye mwinuko,na sehemu yenye hili tatizo ni upande wa kiwanja kwenye slope
 
Reactions: SMU
kaka ufa unasababishwa na mambo mengi ;1,msingi kuwa dhaifu na kushindwa kuhimili uzito wa juu.2,vipande vya tofari kujazana upande mmoja wakati wa ujenzi na kufanya nguvu za mvutano kuelemea upanda dhaifu.kumbuka nyumba inakumbana na force aina mbili; expansion force hii hupasua nyumba kutoka juu na hudhibitiwa na lenta. halafu kuna gravitational force hii ni mgandamizo unaotokana na uzito wa nyumba uzito wote unakua kwenye msingi na ndipo mambo kadhaa yanahitajika kufuata mfano kutanguliza molam au mchanga husaidia wakati udongo mfinyanzi ukicheza(wakati upatapo maji masika) molam au mchanga havibadiliki tabia! jaribu kuchunguza mambo yafuatayo; paa lako au maji kutoka sehemu Fulani yanapita karibu na sehemu husika.maji ya mvua bustani au maji ya bafuni yanaingia taratibu eneo husika msingi unakua disturbed ukuta unaelea ndipo ufa wa vertical unatokea.imarisha eneo ikiwezekana fukua futi moja au zaidi upande husika ,mpaka uzipate tofali za chini toa huo udongo shindili molam na maji kidogo halafu rekebisha ukuta full stop. nyumba zangu ziko sehem yenye udongo mbaya lakini zimetulia mafundi wajenzi wabishi kama nini wakati mambo mengi hawayajui!
 
nilimaanisha ufa wa horizontal ndio unasabishwa na msingi kuwa disturbed hivyo ukuta unakua kama unaelea hewani unakatika nusu.ili kipande cha chini kikakae kuufata udongo ulio sinyaa
 

Mkuu inapokuja suala la crack kwenye nyumba walau nna experience nayo kidogo na kusema kweli inakera. Ukikosea msingi tu mwanzoni matatizo kama hayo yanakuwa makubwa kidogo huko mbele ya safari.
Suluhisho kubwa nadhani ni kukata huo upande wote wenye nyufa na kumwaga nguzo ya maana na pia hakikisha kwenye kona zote unaweka nguzo kuzuia future trends za crack.
Itakubidi upate fundi mzoefu na ujenzi huo akupatie utaalamu zaidi. Crack zinakera sana kwenye nyumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…