Tatizo la Overproduction; Where do we Go From Here..... (A Chinese Case Study)

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Pre-amble: Naongelea Dunia kwa Ujumla na Sio Nchi / Taifa

Ni kawaida kwenye Ubepari kutokea tatizo la overproduction; na hili likitokea wazalishaji wanapunguza uzalishaji jambo ambalo linasababisha uchumi wa wakati huo kushuka na matatizo ya ajira... Kinadharia Over Production inasababisha ushukaji wa bei kwa vitu kukosa demand lakini ki-uhalisia overproduction inatengeneza ukosefu wa ajira pia...

Kwa Ufupi nimechukua article Kuhusu kinachoikumba China kwa sasa na dunia kuilaumu kwamba inatengeneza zaidi ya uhitaji jambo ambalo linaweza kuleta Protectionism (na sababu we have been here before) na kufanya hivyo hakukuleta tija...... Nadhani ni wakati wa kujiuliza ni kipi kifanyike (Automation imebadilisha Rules of the Game)

 
Well, huwezi kuzuia mvua
'You can't stop the waves, but you can learn to surf.'

Huu ni wakati wa Automation na Information Technology efficiency imeongezeka maradufu na nguvu kazi haina uhitaji tena... kwahio models zilizotufaa kipindi cha uzalishaji duni au industrial revolution haziwezi kufaa leo hii...

The World Systems needs to be Overhauled and as what is happening now is not fit for purpose....

Kitakachotokea ni kwamba nchi zitaanza Protectionism (China sasa hivi ni kama ana-supply solar panels na electronics nyingine zaidi ya asilimia 90 ya World Supply; Nchi za western can not compete kwahio unakuta huko wanakosa ajira, na kufunga viwanda vyao...; Watakachofanya na kitakuwa hakina faida kwa Dunia ni kuzuia Bidhaa za China kwao ili walinde ajira lakini mtu wa mwisho itabidi anunue kwa Bei kubwa na China akikosa wateja itabidi watu kule wakose kazi - Lose - Lose Situation
 
Soko la bidhaa za china ni kubwa sana especially ulimwengu wa tatu, hiyo overproduction ya china ni propaganda za west
Ulimwengu wa 3,biashara mnayofanya na china ni kama kununua miswaki supermarket,west wao wananunua fridge,tv,redio,oven,AC.

Yaani thamani yenu ni ndogo sana ktk biashara na china.
 
Lakini ni hyo overproduction ndo ilofanya china ikaendelea !!

Imezalisha vitu vya kuitosha dunia na kubaki
 
Lakini ni hyo overproduction ndo ilofanya china ikaendelea !!

Imezalisha vitu vya kuitosha dunia na kubaki
Ndio sababu wanaonywa,kwamba matokeo yake ni nini!!!!

Leo hii watu wanatabiri kwa kasi ya china ukuaji wa uchumi kuna hatari huko mbele ikasimama kabisa.

Fikiria kila nchi ikiiga move zake ambazo ni rahisi tu,nani atanunua bidhaa zake??
 
Prtotectionism haikwepeki, unakumbuka kipindi cha nyuma mafundi seremala hapa bongo walivyoanza kufunga workshop zao? Ila baada ya Magu kuamrisha kodi nzito kwa furniture toke nje ndio sasa tunaona workshop za mafundi seremala wa Vitanda , Masofa nk. kwa sasa zimerudi, na faida kubwa ni kwamba material wanazotumia wabongo ni mbao halisi, kule China walikuwa wanatumia chenga za maranda ya mbao.., poor quality ila good looks. Huku ni poor looks ila durable
 
Lakini ni hyo overproduction ndo ilofanya china ikaendelea !!

Imezalisha vitu vya kuitosha dunia na kubaki
Ndio maana mwanzo nimesema siongelei China pekee (China ni Case Study ambapo hata wao kuna Ukosefu wa Ajira) naongelea Dunia - Wala kwa China sio Overproduction sababu China ina-supply ulimwengu ila kwa zile nchi zinazoagiza ambazo hawawezi ku-compete na China kwao inabidi waache hizo production sababu Bei zao zinakuwa kubwa zaidi (ni rahisi kuagiza kuliko kutengeneza)

Kwahio hizo nchi zinaweza kwa kupoza hii shida kuamua kuongeza kodi bidhaa za China au kukataza zisiingie Jambo ambalo ni hatari kwa dunia nzima...., unaweza kujikuta unavaa shati bei mara kumi na quality mbovu ukivaa mara mbili limechanika...., Unaweza kunganganiza watu wanunue TanBond kwa kukataa Blueband ila je Tan bond ni bora kuliko hio Blueband (na kama sio bora nani anafaidika hapo)
 
Ndio sababu wanaonywa,kwamba matokeo yake ni nini!!!!
Wanaonywa na West sababu sio West wala nchi yoyote inaweza kushindana na China..., Wachina ni wachapakazi, wanachukua ujira mdogo, sio wabishi na wanaweza ku-adapt kwa kasi sana..., Unadhani kwanini Viwanda vya Iphone vipo China au India na sio USA ? Jibu ni Production Cost....
Leo hii watu wanatabiri kwa kasi ya china ukuaji wa uchumi kuna hatari huko mbele ikasimama kabisa.
Uchumi wa Dunia (Capitalism as we know it) inabidi ubadilike sio China tu..., Capitalism can not Survive hii Efficiency inayoletwa na automation hivyo kutokuwa na uhitaji wa nguvu kazi... Watu watapata wapi pesa ya kuendelea kufanya manunuzi ? Na manunuzi Consumerism ndio fuel inayoendesha Capitalism
Fikiria kila nchi ikiiga move zake ambazo ni rahisi tu,nani atanunua bidhaa zake??
Hakuna nchi inayoweza kufanya kama China tungeweza hata nguo tu na viatu tungeweza kufanya wenyewe ila ndio hivyo hata toothpick ni cheaper kuitoa China kuliko wewe kutengeneza
 
Protectionism ilifanyika sana kipindi cha nyuma ila kilichotokea ni hasara kwa Dunia nzima..., Kuna kipindi USA alikuwa ndio jemedari wa kutengeneza magari na innovation za kina Ford.., baada ya kufanya Protectionism kina Toyota kwa kufanya kazi na wengine na kuruhusu competition ikapelekea innovation......

Leo ukatae furniture za mchina na yeye akisema hataki parachichi zako ? Kama kweli furniture za Bongo ni nzuri kuliko mchina kwanini mteja anunue mchina.... Am all for self reliance lakini more than that ninajua Mr Adam alimaanisha nini aliposema......

It is the maxim of every prudent master of a family, never to attempt to make at home what it will cost him more to make than to buy...What is prudence in the conduct of every private family, can scarce be folly in that of a great kingdom.

Kama hatuwezi kuengeneza furniture cheaply basi tujikite tunachoweza zaidi / mfano labda hospitality kule Serengeti (Mchina hawezi akatengeneza Serengeti yake) Au tuige kwanini wao zinakuwa cheap hivyo tutengeneze huku na kuuza cheap (sababu kutakuwa hakuna transport cost wala kodi)
 
Uchumi sio kampeni za siasa ni matokeo ya kazi zenye thamani,na huwa una kanuni zake,huwezi kuzifunja kwa namna yako wewe.hao wachina wanaofuatwa kwa gharama ndogo za uzalishaji,unajua kwamba wanatakiwa kuongezwa malipo kutokana na gharama za maisha kukua??huoni kwamba wanarudi kule kule iliko US??
Kumbe sio uongo anachoambiwa china ni kitu halisi.
Hakuna nchi inayoweza kufanya kama China tungeweza hata nguo tu na viatu tungeweza kufanya wenyewe ila ndio hivyo hata toothpick ni cheaper kuitoa China kuliko wewe kutengeneza
Kama wewe huwezi usiseme haiwezekani,unajua india ni ya ngapi kiuchumi duniani??ina mikakati gani ya kimaendeleo??
Walikopita china india ndiko huko wanafata,viwanda kama vga Apple tayari vimenza hatua za kuhamia india maana china kumeshaanza kuchacha na pili kumekuwa si kwa kutabirika kutokana na misuguano ya mara kwa mara na magahribu.
 
Wanatakiwa kuongezewa pesa na nani ? Capitalism ni Profit at all costs sio Welfare..., (Ingawa China a Market Socialist) angalau kuna some State companies nyingi ila muwekezaji mwingine yeye yupo answerable kwa shareholder kwahio kama kuna uwezekano wa kupata mtu kwa pesa ndogo hawezi kukupa wewe pesa zaidi...

Na hapa kuna issue ya Automation ambayo tunapoelekea wala mtu hatahitajika tena let alone mtu wa ujira mdogo....
Kumbe sio uongo anachoambiwa china ni kitu halisi.
Overproduction kwa dunia kuisambazia bidhaa zake ila kwa wachina bado kuna wahitaji wa kazi / shughuli hivyo kwao wanaona hio sio overproduction ; pili automation inapunguza uhitaji wa hao watu hata kama production ikibakia constant na mwisho kabisa bado uhitaji wa bidhaa za China upo (Ina-supply more than 90% ya solar panels za dunia na inafanya hivyo cheaper than anyone can....
Kama wewe huwezi usiseme haiwezekani,unajua india ni ya ngapi kiuchumi duniani??ina mikakati gani ya kimaendeleo??
Tusiongelee kwanza Uchumi wa kwenye makaratasi India pamoja na huo uchumi wao ni nchi yenye masikini wengi wa kutupwa na ajira bado ni tatizo na hata hivyo bado unajijibu western hawewezi kupambana na nchi ambazo zina production cost ndogo; kwahio huwezi kushindana na watu kama China kutokana na ukweli kwamba Production cost kule ni ndogo....
Walikopita china india ndiko huko wanafata,viwanda kama vga Apple tayari vimenza hatua za kuhamia india maana china kumeshaanza kuchacha na pili kumekuwa si kwa kutabirika kutokana na misuguano ya mara kwa mara na magahribu.
Corporations hazina nchi zinaweza kuhama wakati wowote kama tu wanapokwenda kutakuwa na a Better Bottom Line.....; Na hio better bottom line inatokana na cheap labor..., wewe unaongelea leo Viwanda vya Adidas na Nike vimekuwepo India tangu enzi na enzi..., kwanini sababu watu wanakaa kwenye ma-domitory na kulipwa peanuts kulinganisha na kama kingekuwepo USA

Lakini with automation huenda hata hao waliokuwa wanapata hizo peanuts hivyo kuweza kutuma vijisenti makwao hio ikawa historia....
 
Okay, Magu alijua kwamba huwezi zalisja vitu cheaply kama nishati ni expensive mara 10 ya mpinzani wako kwenye soko, hivyo akajenga Rufiji, cha ajabu huyu Mama anakuja kusema hashushi bei, ni vile tu mwanasheria wangu yupo likizo, ila…
 
Okay, Magu alijua kwamba huwezi zalisja vitu cheaply kama nishati ni expensive mara 10 ya mpinzani wako kwenye soko, hivyo akajenga Rufiji, cha ajabu huyu Mama anakuja kusema hashushi bei, ni vile tu mwanasheria wangu yupo likizo, ila…
Magu angalau alikuwa na Vision Like him or hate Him lakini alikuwa mtendaji na mchapakazi (the guy would have made a great Prime Minister)

Nishati ikishuka bei hata tusipozalisha na kuuza angalau tutatumia majiko yetu ya umeme kupikia hence tutapunguza kununua LPG ambayo inazidi kutu-cost...; Anyway sasa hivi tumeamua kuingia mikataba na EU kufungulia kila kitu ni kwamba tutakuwa flooded na junks kutoka huko na sisi hatuwezi kupeleka junks zetu (tutaambiwa we can not meet the quality standard)

Na vile ambavyo tungeweza hata kukodi experts ili tuweze kubaki na 100 % (Bandari et al) na vyenyewe tunawapa so called wawekezaji... Nachelea kusema Kesho yetu itakuwa ngumu sana....
 
Actually, we are done for.., i don knw, labda Mungu anakusudi lake kutuletea huyu mama, atuchemshe kabisa ili akili zizibuke , who knows..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…