Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kuwa Simba wako mbioni kukamilisha usajili wa kocha mmoja kutoka Afrika ya Kusini. Kama tetesi hizi ni za kweli basi simba watakakuwa wanakosea, huu ni mtazamo wangu binafsi.
Tatizo la Simba lipo kwenye uongozi, wengi wao ni wapigaji ambao wanaangalia zaidi maslahi yao badala ya timu,
Wanasajili wachezaji wa kigeni wenye viwango vya kati ambao hawana tofauti na wazawa,
Kwa upande wa kocha mi nadhani wangempa nafasi kocha mzawa Juma Mgunda ambaye amefanya vizuri kwa muda mfupi alioakabidhiwa jukumu la kukaimu nafasi ya kocha mkuu.
Mgunda amekuwa akikaimu nafasi ya kocha mkuu kwa kipindi kifupi, japo anafanya vizuri lakini Simba wakimpata kocha mwingine wanamtema, hii ni dharau kwa makocha wetu wazawa, asikubali tena kutumika kama bazoka.
Nawasilisha.