TAWA
JF-Expert Member
- Jun 23, 2013
- 3,674
- 1,572
Tunashuhudia kiungo wa simba Justice Majabvi akigoma kuelekea Mwanza kwa ajili ya mchezo dhidi ya Toto Africa, sababu kubwa ni Majabvi kutotimiziwa haki zake kama mchezaji wa kulipwa hasa kupatiwa nyumba ya kuishi.
Majabvi wakati anaondoka kwenda kwao Zimbabwe Kwa ajili ya mapumziko, uongozi ulimwahidi kwamba akirudi mambo yatakuwa sawa na hawatamwita kama mambo hayatakamilika. Lakini wakamwita na bado anaishi pale Lamada kama mkimbizi.
Suala la messi (Singano) mpaka leo hayupo mwana simba anayefahamu ukweli wake ila ni viongozi wachache.
Suala la kiwanja kule Bunju, ukienda hovyo unaweza ukakutana na faru kama siyo chui katika eneo hilo ambalo ujenzi wake ulishaanza kwa mbwembwe na tayari kilikuwa kizuri kama kinavyoonekana pichani.
Suala la mohamed Dewji kuinunua klabu au kuweka shea katika klabu ili klabu iweze kuendelea
Yani kuna mambo kibao ambayo yanatia kichefuchefu ndani ya simba. Ila ukiongea utaambiwa, "tuache na simba yetu, simba jina kubwa"
Viongozi wengi wa simba ni shule ndogo hivyo wanashindwa kuendana na mfumo wa kisasa wa kuendesha klabu. Mtu kama Hans Pope ana madaraka makubwa ndani ya klabu kuliko Rais wa klabu.
Hayo tu, tukosoane kwa staha.