Tatizo la Simba, timu inaendeshwa kienyeji

TAWA

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2013
Posts
3,674
Reaction score
1,572
Tunashuhudia kiungo wa simba Justice Majabvi akigoma kuelekea Mwanza kwa ajili ya mchezo dhidi ya Toto Africa, sababu kubwa ni Majabvi kutotimiziwa haki zake kama mchezaji wa kulipwa hasa kupatiwa nyumba ya kuishi.

Majabvi wakati anaondoka kwenda kwao Zimbabwe Kwa ajili ya mapumziko, uongozi ulimwahidi kwamba akirudi mambo yatakuwa sawa na hawatamwita kama mambo hayatakamilika. Lakini wakamwita na bado anaishi pale Lamada kama mkimbizi.

Suala la messi (Singano) mpaka leo hayupo mwana simba anayefahamu ukweli wake ila ni viongozi wachache.
Suala la kiwanja kule Bunju, ukienda hovyo unaweza ukakutana na faru kama siyo chui katika eneo hilo ambalo ujenzi wake ulishaanza kwa mbwembwe na tayari kilikuwa kizuri kama kinavyoonekana pichani.

Suala la mohamed Dewji kuinunua klabu au kuweka shea katika klabu ili klabu iweze kuendelea
Yani kuna mambo kibao ambayo yanatia kichefuchefu ndani ya simba. Ila ukiongea utaambiwa, "tuache na simba yetu, simba jina kubwa"

Viongozi wengi wa simba ni shule ndogo hivyo wanashindwa kuendana na mfumo wa kisasa wa kuendesha klabu. Mtu kama Hans Pope ana madaraka makubwa ndani ya klabu kuliko Rais wa klabu.

Hayo tu, tukosoane kwa staha.
 

Attachments

  • 1450465611553.jpg
    24.9 KB · Views: 863
Huku mwanza nmewakuta hotel ya isamilo Lodge. Ni albu. Wanalala wawiliwawili. Ni shida tupu. Hii clabu haina pesa
 
Klabu kukosa hela sio aibu, ni umaskini tu. Hata wewe au ndugu yako akikosa hela sio jambo la aibu, ni umaskini tu. Yanga na Azam zinaonekana zina hela, si ujanja wa viongozi wake, bali kuna mtu amekuwa anatoa tu hela zake binafsi kuendesha klabu, na wala si mapato ya klabu. Leo mfadhili akitaka kujitoa, watu wazima wenye familia zao wamampigia magoti, hiyo ndiyo aibu!
 
Huku mwanza nmewakuta hotel ya isamilo Lodge. Ni albu. Wanalala wawiliwawili. Ni shida tupu. Hii clabu haina pesa

Tatizo siyo pesa mimi nazungumzia club kuendesha kienyeji. Wachezaji wanacheleweshewaje mishahara wakati anayelipa ni mdhamini ambye ni Kilimanjaro? Kuchukua ubingwa simba msimu huu ni ndoto za mchana kweupeee
 
Viongozi Wa simba wamekaa kiudalali Na kuzulumu wachezaji halafu wanajifanya wanajua sana Sheria kumbe hawajui
 
Ukiondoa Klabu ya Azam, ambayo uendeshaji wake upo kisasa, klabu zingine zote kubwa hapa Tanzania plus TFF zinaendeshwa kihuni, kienyeji na kiujanja ujanja tu. Hazina vision wala mission, zipo zipo tu. Simba na Yanga, zote ni pasua kichwa. Zinaingiza pesa nyingi sana lakini zina mifumo mibovu balaa ya kutumia pesa.
 
Vilabu vyetu badilikeni,akili ndogo iache nafasi kwa elimu kubwa Ili ilete maendele
Nalog off
 
Nilimshangaa sana Mohamed Dewji kutaka kuwekeza pesa zake Simba. Ni mara mia akaanzisha timu yake binafsi, akaikuza baada ya miaka minne itakuwa ligi kuu, ikiwa na viwanja vyake, Jezi zake, Wachezaji wake, nk na kuwa Big brand ya Soka hapa Tanzania na Ukanda wa Afrika.
Azam wameweza na wataweza zaidi na zaidi. Kwa nini MO Dewji asiige mfano huo?
 

Alishawahi kumiliki timu inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania Bara.. Ilikua inaitwa African Lyon.. Baada ya msimu mmoja, ikamshinda.. Akaipiga bei kwa Rahimu Zemunda.
 
'Viongozi wengi wa klabu ya simba elimu ndogo 'hapo umeongea point hicho ndicho kinaimaliza simba
 
haipiti mwezi bila kusikia kuna vituko msimbazi kilikoni??..
 

Alishawahi kumiliki timu inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania Bara.. Ilikua inaitwa African Lyon.. Baada ya msimu mmoja, ikamshinda.. Akaipiga bei kwa Rahimu Zemunda.
Ishu kwa Mo Dewji kuitaka Simba, kwanza yeye ni simba damu, pia ni mfanyabiashara anayeona fursa za kupata faida, pili ni kuwa simba na yanga zina FANBASE kubwa sana! Viongozi wa hizi timu wangekuwa smart, kuna hela nyingi sana!

Azam itaendelea kuwa timu inayoendeshwa kisasa, ila kamwe upande wa fanbase hawataifunika simba au yanga! Hata miaka mingi ijayo, hizi timu mbili zitaendelea kuwa na fanbase kubwa! Timu zingine kama Azam zitaendelea kuwa na fans wa mkopo, Azam wakicheza na simba, watawapata fans wa yanga na yanga wakicheza na azam watapata fans wa simba, simple!
 

Sio kila jambo baya linalofanywa na timu ya simba linafananishwe na yanga, Kuna mchezaji wa yanga anaelalamikia sehemu ya kulala!! Mishahara je!!!?
Tumia akili unapocomment
 
Tatizo siyo pesa mimi nazungumzia club kuendesha kienyeji. Wachezaji wanacheleweshewaje mishahara wakati anayelipa ni mdhamini ambye ni Kilimanjaro? Kuchukua ubingwa simba msimu huu ni ndoto za mchana kweupeee

tatizo la simba hakuna m2 mwenye final say..kila kiongoz anajiona ana nguvu kuliko wengine...kwakweli m/kiti(sijui anajiita rais)we2 jipu....
 
Tatitizo niTFF imeshindwa kuweka kanuni na sheria za uendeshaji klabu katika ligi.
Timu zinatakiwa ziwe na Taarifa ya fedha na hesabu za mwaka zilizokaguliwa na ziwasilishwe TFF.
Viongozi wa TFF wameshindwa kuweka sera itakayo inua kiwango na ubora wa soka letu.
Kiongozi ametumia fedha kupata madaraka,na kujikuta hana mtazamo wa kuendeleza soka.
Mapato yatokanayo na mechi kubwa yamekuwa yanavuja na hakuna mkakati wa kudhibiti mapato,kila siku ni visingizio!
Sera,kanuni na sheria nzuri zingeweza kuzuia kuwepo kwa ubabaishaji katika uendeshaji wa soka kwenye klabu hadi chama cha soka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…