Tatizo la taa ya 'oil' kuwaka na kuzima

Tatizo la taa ya 'oil' kuwaka na kuzima

Naomba kuleta mrejesho kulingana maada tajwa hapo ambayo niliileta kwenu majuzi. Kwanza niwashukuru kwa ushauri wenu hakika umekuwa msaada sana kiasi cha kuniokolea zaidi ya 400,000 maana nilikuwa nimeambiwa na fundi kufungua engine na kununua shaft. Nilifanyia kazi ushauri wa kusafisha straner na kweli ilikuwa chafu sana tena sana baada ya kusafishwa taa haiwaki tena. Ahsante sana ndugu zangu
Rudi kwa yule fundi mueleze tatizo lilikuwa nini na umesharekebisha ili aone noma
 
Kwahiyo kwenye brake kinachotumika ni nini,au mwenzetu unatumia maji,sikupati vizuri mkuu..?
Matatizo ya brake yanaoneshwaga na ABS sensor! Ukiona ABS imewaka ujue kuna shida mahali kwenye mfumo wa brake kuanzia oil level mpaka brake cylinder au speed sensor!
 
Unapokwenda kubadilisha oil kuwa makini mafundi huwa wanarudisha oil filter ile ile uliyotoa hiyo huwa inasababisha shida sana. Pia jaribu kusafisha engine kwa kuflush wastes zote especially kwenye bakuli ile ya sample....

Pia cheki oil pump unaweza kuta pressure sio nzuri oil haisambai vema.
 
Kwahiyo kwenye brake kinachotumika ni nini,au mwenzetu unatumia maji,sikupati vizuri mkuu..?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], so oil ya kwenye breki na ya kwenye engine vyote vinazunguka pamoja.... Eti?!
 
Naomba kuleta mrejesho kulingana maada tajwa hapo ambayo niliileta kwenu majuzi. Kwanza niwashukuru kwa ushauri wenu hakika umekuwa msaada sana kiasi cha kuniokolea zaidi ya 400,000 maana nilikuwa nimeambiwa na fundi kufungua engine na kununua shaft.

Nilifanyia kazi ushauri wa kusafisha straner na kweli ilikuwa chafu sana tena sana baada ya kusafishwa taa haiwaki tena. Ahsante sana ndugu zangu
Weka picha....
 
Mafundi nao huwa na majibu tofauti tofauti kama wachangiaji wa hii post.
 
Back
Top Bottom