Tatizo la Tanzania sio Katiba Mpya bali utii wa Katiba iliyopo

Tatizo la Tanzania sio Katiba Mpya bali utii wa Katiba iliyopo

MenukaJr

Member
Joined
Apr 24, 2021
Posts
50
Reaction score
128
Mjadala wa madai ya Katiba mpya unaendelea kushika hatamu. Baadhi yetu wanadai kuwa nchi inahitaji Katiba mpya, wanatoa sababu zao. Madai yao ni ya kuheshimiwa kwa sababu ni haki yao lakini ni yenye kustahili kusahihishwa kwa sababu si ya kweli. Ni uongo!

Kwa ajili ya kumbukumbu, nimekusudia kusahihisha madai ya Katiba mpya kama yanavyotolewa. Kimsingi, tatizo la Tanzania kwa wakati huu sio Katiba mpya, tatizo la Tanzania ni UTII wa Katiba iliyopo. Tumekosa watu wenye kuitii Katiba yetu ndio maana inaonekana mbovu. Katiba hata ikiwa mpya, bora kwa namna gani kama haikufuatwa na kuheshimiwa haina maana yoyote.

Hii ndio sababu wenye HOJA hii, tunashauri watu wafundishwe kutii Katiba kisha tunaweza kufikiria kuandika Katiba mpya. Kuandika Katiba mpya katika nchi ya watu wasio na desturi ya kutii Katiba ni kupoteza muda bure kwa kuwa hata hiyo mpya itavunjwa vilevile, itakosa maana.

Katika kusaidia jambo hili, tumewaeleza wenzetu kwamba jambo la Katiba ni la msingi sana lakini limefanywa kwa haraka mno bila maandalizi ya kutosha kwa hivyo litakwama. Tumewaeleza kuwa, mambo makubwa kama haya huhitaji maandalizi ya kutosha kabla ya kuanzishwa kwake. Tumewapa mfano wenzetu kwamba, hata katika uumbaji, Mungu alipokusudia kumuumba binadamu hakuanza na binadamu bali mazingira yake kwanza. Aliumba nuru na giza, anga na ardhi, maji na mimea kwa ajili ya chakula na maji ya kunywa. Halafu mwishoni akamuumba Mwanadamu, akamaliza kazi yake kwa ufanisi.

Kama Mungu angalianza kumuumba Mwanadamu kabla ya nchi, Mwandamu angalikosa mahala pa kuishi. Au kama Mungu angalitangulia kumuumba Mwanadamu kabla ya mimea na maji, bila shaka Mwanadamu angalikosa maji ya kunywa na chakula cha kula. Angalikufa na kazi ya Mungu ingalikosa maana

Huwezi kudai Katiba mpya bila kwanza kuwafundisha watu utii wa Katiba kwa sababu watavunja Katiba iliyopo ili kupata Katiba mpya. Ni kosa hilo!! Sio jambo la hekima kudai Katiba ya nchi nzima kwa kutegemea akaunt ya Kigogo Twitter au Maria Sarungi. Ni ukorofi kumtegemea Mdude Nyagali katika madai ya Katiba mpya kwa sababu Katiba ya nchi ni zaidi ya umbea na matusi. Katiba ya nchi ni jambo kubwa kabisa katika nchi lenye kuhitaji akili kubwa na utulivu wa hali ya juu. Wenye madai haya kwa sasa, wamekosa sifa hizi. Hawawezi kupata chochote!!

Pengine nioneshe udhaifu wa HOJA zinazotumiwa katika madai ya Katiba mpya ambazo zingaliweza kutatuliwa na UTII wa Katiba iliyopo;

1. Mamlaka ya Rais
Wanasema kuwa Rais amepewa mamlaka makubwa sana na Katiba hii. Nadhani, hawakufikiria sawasawa katika madai haya. Rais wa nchi ni kama Baba wa familia, mamlaka ya Rais katika nchi ni sawa na mamlaka ya Baba katika familia. Anawajibika na kila kitu kama msimamizi na mwamuzi mkuu wa familia. Ni kosa kusema Baba amepewa mamlaka makubwa katika kutimiza wajibu wake isipokuwa ikiwa atatumia mamlaka hayo vibaya. Hata ikiwa hivyo, kosa haliwezi kuwa na mwenye kutoa mamlaka isipokuwa mwenye kuyatumia vibaya. Tufundishe watu utii wa Katiba iliyopo.

Katika kuipa uzito hoja yao hii, wanatumia ibara ya 37(1) kuwa Rais atakua huru na hatalazimika kuchukua ushauri wa mtu yeyote isipokuwa kwa matakwa ya Katiba. Kwa sharti hili, Katiba haimlazimishi Rais kuchukua ushauri wa mtu lakini pia haimzuii Rais kushukua ushauri mzuri wa mtu yeyote. Kuna kosa gani katika Katiba yenye kumpa uhuru Rais katika kushauriwa na yeyote na isiyomzuia kukubali kushauriwa. Bila shaka tatizo haliwezi kuwa Katiba bali utii wa Katiba. Hatuwezi kuwa na Katiba inayomlazimisha Rais wa nchi kuchukua ushauri wa mtu kwa sababu tunaweza kuwa na Ma-Rais wengi kwa wakati mmoja. Rais mwenye kukataa ushauri mzuri ametumia vibaya uhuru wa Katiba sawa na Rais mwenye kuchukua ushauri mbaya. Katiba inayompa Rais uhuru wa kuchagua ushauri wa kuchukua kulingana na maslahi ya nchi haiwezi kuhesabika kuwa Katiba mbaya. Tuwafundishe watu UTII wa Katiba!

2. Tume huru ya Uchaguzi
Kuna kosa gani katika Katiba inayounda Tume ya Uchaguzi na kuweka sharti kwamba Tume haitalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu yeyote au idara yoyote ya Serikali au Chama chochote cha Siasa" (Ibara ya 74(11)). Kuna kosa gani na Katiba ya namna hii??

Tumesema, tatizo la nchi yetu sio Katiba mpya bali UTII wa Katiba. Mwenyekiti wa Tume anayefuata maagizo ya Kiongozi wa Serikali amevunja Katiba kama Kiongozi wa Serikali au Chama cha Siasa anayemwagiza Mwenyekiti wa Tume kitu cha kufanya. Katiba imekataza tayari, imeweka katazo kwa vyovyote hili haliwezi kuwa kosa la Katiba isipokuwa watu wasiotii Katiba ya nchi na kuwa tayari kuisimamia. Katiba inayozuia Chama cha Siasa kuingilia shughuli za tume halafu Chama kikaingilia kwa maksudi, Katiba inayoizuia Serikali kuingilia shughuli za Tume ya Uchaguzi ina kosa gani? Tunataka Katoba mpya ifanyeje ifanyeje matika hili? Hapana. Narudia, tatizo letu sio Katiba mpya bali utii wa Katiba iliyopo. Kama watu wataamua kuitii, kuiheshimu na kuisimamia Katiba hii, tunaweza kuwa na Katiba bora kuliko inavyofikiriwa.

3. Ukuu wa Katiba
Wenye kudai Katiba mpya, wanasema Katiba iliyopo inavunjwa hovyo. Wanatolea mfano Wabunge 19 walioko Bungeni kinyume na utaratibu. Ndio maana nasema watu hawa hawajui hata wanachokidai. Sasa kama Katiba iliyopo inavunjwa hovyo suluhu ni kupata Katiba mpya au kuzuia watu wasivunje Katiba. Hivi, kuna kosa gani katika Katiba inayotaja sifa za Mbunge (Ibara ya 67 (1) (b) kuwa lazima awe na Chama cha Siasa halafu Spika wa Bunge kwa maksudi akaruhusu Wabunge wasio na sifa kushiriki Bunge.

Tunawezaje kuilaumu Katiba kwa kosa hili ambalo imeliwekea utaratibu na sheria. Kama Spika wa Bunge angalitii Katiba hilo lisingalikuwapo. Narudia tena, tatizo letu sio Katiba mpya bali utii wa Katiba iliyopo. Kama watu hawakufundishwa KUTII Katiba, hata ikipatikana Katiba mpya namna gani haiwezi kuwa namaana yoyote. Itavunjwa kama inavyovunjwa hii.

#TufundisheUtiiWaKatibaKwanza.
MenukaJr.
FikraHuru!
 
Tatizo la watanzania sasa ni huu umasikini. Watanzania wengi wanawaza kuwa na maisha bora angalau pesa itembee mikononi mwao. Kuwaletea Katiba Mpya kwa sasa hata hawakuelewi zaidi wataona ni mpango wenu nyie wanasiasa kujinufaisha.
Turejesheni uchumi wa watu kwanza hiyo katiba itakuja tu. Mbona tumeishi miaka 10 ya Maisha Bora kwa kila Mtanzania na katiba hii hii ya zamani??
 
Umeandika ukweli tupu mkuu!!

Tunaposhindwa kutii katiba zetu ndogondogo za vyama vyetu, Hiyo ni ishara kwamba, hata tukipata katiba bora na nzuri mno, haitatusaidia

Tuanze kwanza kuheshivu tulivyonavyo,

Chadema, inamkwamo wa kikatiba, lakini hawashughurikii, halafu ndio hao hao wanadai tupate katiba nyingine!!

Kuwa chizi ni hadi uokote makopo pekee?

Kama ni hivyo, basi Hao watu wako salama? lakini kama uchizi unaviashiria vingi, ujue wamo hao ndugu zetu, Wanatusumbuaaa...! halafu ndio wa kwanza kuvunja katiba
 
Andiko lako, naliunga mkono, pamoja na kwamba sijasoma uliyoandika humo ndani, mbali ya Kichwa cha habari na 'subtitles' zake.

Lakini, Katika viongozi wote tuliowahi kuwapata Tanzania, pamoja na uwepo wa Katiba hii, sikumbuki uwepo wa kiongozi mwingine mbali ya Magufuli aliyeonyesha waziwazi kutoijali katiba iliyopo, na ambayo aliapa kuihifadhi, kuilinda na kuitetea.

Kwa ujumla, Magufuli hata ingekuwepo katiba ya malaika isingemzuia kuikiuka katiba hiyo na kujifanyia anavyoona yeye inafaa.

Je, kungekuwepo na Katiba inayotamka bayana na waziwazi kwamba kiongozi akifanya mambo kadhaa, kadhaa yanayokiuka katiba anastahili kuchukuliwa hatua kadhaa wa kadhaa, hiyo ingemzuia kiongozi wa aina yake kuyafanya hayo mambo ambayo anazuiwa kuyafanya?

Kiongozi akikiuka katiba afanywe nini?

Nani atasimamia hayo yanayotakiwa kufanywa? Anao uwezo wa kuyafanya, kama hana mitutu ya bunduki?

Kama ni Bunge, litafanya nini kama hilo bunge lipo kwa fadhila za kiongozi huyo?

Mahakama, yataanzia wapi taratibu za kumzuia au kumwondoa kiongozi anayekiuka sheria na katiba?

Mamlaka pekee yenye uwezo ni wananchi wenyewe, lakini nao wataanzia wapi kumdhibiti kiongozi anayewatishia mabunduki, mabomu, n.k.; na hasa wakati wananchi hao wamegawanyika, na hawana viongozi wa kuwaelekeza kipi cha kufanya.

Jeshi, likiwa ni jeshi kweli la kulinda maslahi ya nchi linao uwezo wa kumwondoa kiongozi kama huyo, lakini uongozi wao huko huko ndani ya jeshi lenyewe wanaweza kuwa wanalinda maslahi yao zaidi, kuliko maslahi ya nchi.

Utawafundisha vipi wananchi wajue na wathamini HAKI zao, na zinapovurugwa wawe tayari kuzipigania? Ni nani ataifanya kazi hii na kwa utashi upi?
 
Mkuu kalamu. South Africa wameweza kumuondoa Zuma na sasa wanampwleka Jela . wao wanawezaje? Haya mambo yanawezekan ili mradi katiba iseme hivyo
 
Mkuu 'Menuka jr', imenilazimu nirudi haraka baada ya kubandika niliyobandika mwanzo.

Niulize swali, pengine litakuwa ndilo msingi pia wa mjadala huu:

Hivi katika viongozi wakuu wote katika ngazi zote za uongozi, ni kiongozi yupi hasa anaapa "Kuilinda, kuitetea, kuihifadhi, n.k." Katiba?

Tukiwaacha hawa akina 'spika', ambao uwezo wao wa kutetea wabunge unatokana na huyo huyo mmoja aliyeshindwa kutimiza aliyoapa?
 
... kwa namna moja uko sahihi; utii wa katiba imekuwa tatizo sugu kwa viongozi. Nini kifanyike? Au Katiba yenyewe inasemaje kwa wasiotaka kuitii? Ok, unaweza kusema asiyeridhika "aende mahakamani" kauli pendwa ya viongozi. Huko mahakamani cases zitapigwa danadana forever kwa sababu waamuzi ni wanufaika walinda mfumo wa hovyo uliopo au case ikiamuliwa itaamuliwa jinsi wanufaika wa katiba iliyopo wapendavyo! Ukienda mahakama za kikanda na kimataifa case ikiamuliwa kwa haki utaambiwa sheria za Tanzania haitambui hukumu hiyo.

So, Katiba iliyopo ina matundu ambayo daima viongozi wanaoivunja wana matundu mengi mno ya kutokea hivyo viongozi kufanya lolote wapendavyo. Haina concrete measures za kuwawajibisha viongozi bila kuwapa upenyo wa kutokea. As a result, nchi haipigi hatua katika mambo mengi kwa sababu uwazi na (hasa) uwajibikaji unakosekana. Viongozi wanafanya chochote bila hofu! Lengo la Katiba Mpya pamoja na mambo mengine mengi ni kuziba matundu hayo yanayotumiwa vibaya na viongozi na CCM ili kuongeza uwajibakaji; mtu akifanya kosa au akiivunja atambue atawajibika tena within time. Sio viongozi wanajibu kwa dharau na viburi vya wazi kabisa; "mtatufanya nini".

Kiongozi anatenda jinai halafu uwajibikaji wake ni hisani ya mamlaka ya ya uteuzi (at his/her pleasure) halafu utasema tuna katiba? Mamlaka ya uteuzi haijatekeleza wajibu wake kwa wakati nini kifanyike na yule anayepaswa kua-act mfano Bunge lisipo-act simply wamekuwa cartel moja nini kifanyike? Katiba ya sasa iko kimya!
 
Tatizo la watanzania sasa ni huu umasikini. Watanzania wengi wanawaza kuwa na maisha bora angalau pesa itembee mikononi mwao. Kuwaletea Katiba Mpya kwa sasa hata hawakuelewi zaidi wataona ni mpango wenu nyie wanasiasa kujinufaisha.
Turejesheni uchumi wa watu kwanza hiyo katiba itakuja tu. Mbona tumeishi miaka 10 ya Maisha Bora kwa kila Mtanzania na katiba hii hii ya zamani??
acha uongo,
 
Umeandika ukweli tupu mkuu!!

Tunaposhindwa kutii katiba zetu ndogondogo za vyama vyetu, Hiyo ni ishara kwamba, hata tukipata katiba bora na nzuri mno, haitatusaidia

Tuanze kwanza kuheshivu tulivyonavyo,

Chadema, inamkwamo wa kikatiba, lakini hawashughurikii, halafu ndio hao hao wanadai tupate katiba nyingine!!

Kuwa chizi ni hadi uokote makopo pekee?

Kama ni hivyo, basi Hao watu wako salama? lakini kama uchizi unaviashiria vingi, ujue wamo hao ndugu zetu, Wanatusumbuaaa...! halafu ndio wa kwanza kuvunja katiba
hakuna ukweli hapo huyo hajui maana ya KATIBA.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Mkuu kalamu. South Africa wameweza kumuondoa Zuma na sasa wanampwleka Jela . wao wanawezaje? Haya mambo yanawezekan ili mradi katiba iseme hivyo
Mfano mzuri sana unaohitaji ufafanuzi juu yake kuhusu: wao wanawezaje kufanya hivyo?
Je, Ramaphosa angekuwa ni Magufuli wao na akamwekea kinga Zuma kama wangekuwa ni marafiki tu, ingekuwaje?

Ramaphosa angekuwa amekiuka katiba, je na yeye angewajibishwa? Na nani?
 
... kwa mtanzania kama Profesa Kabudi ambaye Katiba iliyopo inamhakikishia kupita bila kupingwa popote; inamhakikishia hata kama asipopata jimbo ana uhakika wa kuwa mbunge kupitia zile nafasi 10; ni retired government officer usitegemee hata mara moja a-support mawazo ya Katiba Mpya; never! Katiba iliyopo inamhakikishia ugali maisha yake yote yaliyobaki. Msome hapa: Profesa Kabudi: Katiba tuliyonayo ni madhubuti ndio maana imetuvusha tulipopata matatizo!
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Tatizo la watanzania sasa ni huu umasikini. Watanzania wengi wanawaza kuwa na maisha bora angalau pesa itembee mikononi mwao. Kuwaletea Katiba Mpya kwa sasa hata hawakuelewi zaidi wataona ni mpango wenu nyie wanasiasa kujinufaisha.
Turejesheni uchumi wa watu kwanza hiyo katiba itakuja tu. Mbona tumeishi miaka 10 ya Maisha Bora kwa kila Mtanzania na katiba hii hii ya zamani??
katiba ndio msingi ambao sheria zote zinazoendeshwa nchi zimejengwa juu yake mkuu, sheria za uwekezaji au umiliki ardhi na zinginezo zote zinatungwa kwa kuzingatia misingi ya katiba, maisha bora hayawezi kuletwa na katiba mbovu au sheria zitokanazo na katiba mbovu, ila naunga mkono hoja kuwa issue si katiba mpya issue ni kuanza kuheshimu hii iliopo kwanza
 
Rais anaemiliki hazina na majeshi, kama hakuna hulka ya kuheshimu taratibu zilizopo hata kama mkiwa na katiba nzuri vipi atawayumbisha tu.

Vinginevyo mtajikuta mnataka kuandika katiba nyingine kila mwaka.
Kukiuka yaliyomo ndani ya katiba ni "KUVUNJA SHERIA" ; maajabu leo ni kwamba tunao wananchi wanaoshangilia kiongozi wao mkuu ambaye ni Jambazi, mvunja sheria mkuu!

Kama hilo haliwezi kukushangaza, sijui ni lipi litakushangaza!

Kwa hiyo, mimi nadhani, pamoja na kuwepo kwa katiba inayotamka wazi kabisa madaraka aliyonayo mkuu wa nchi, yanayoruhusiwa na katiba moja kwa moja, na yanayokatazwa na katiba kwa uwazi kabisa...

Ni jukumu la wananchi wenyewe kujua katiba yao inatamka yapi, na utashi wa wananchi hao kuisimamia katiba ya nchi yao isivunjwe hovyohovyo.

Wananchi wawe na ufahamu wa mamlaka za taasisi zinazowatumikia, na wajuwe mifumo iliyopo inayoiendesha nchi yao.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kukiuka yaliyomo ndani ya katiba ni "KUVUNJA SHERIA" ; maajabu leo ni kwamba tunao wananchi wanaoshangilia kiongozi wao mkuu ambaye ni Jambazi, mvunja sheria mkuu!

Kama hilo haliwezi kukushangaza, sijui ni lipi litakushangaza!
Wewe umefanya nini baada ya hiyo katiba kuvunjwa ??
 
"Hatuwezi tatua matatizo yetu kwa kujidanganya kwamba hayupo"Mwl.Nyerere

Kama tushagundua katiba ina tatizo basi lazima hatua kadhaa zifanyike kutatua tatizo hilo ni wazi katiba inashida hivyo lazima itafutwe dawa ya kutibu tatizo JK aligundua hili ndo maana alianza mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya Kama taifa lazima tuwe na maono ya pamoja kuhusu taifa sio suala la kusubili hisani ya kiongozi au kundi fulani.

Swali la msingi ni je, Kama taifa tunahitaji katiba mpya Kama jibu ni ndio na Kuna sababu ya kuhitaji basi mchakato uanze na Kama jibu ni hapana na Kuna sababu basi hakuna haja.
 
kweli kabisa yaan ht tukicopy katiba ya ufaransa still kwetu itakua tabu tupu maana mtu atakwambia mhimili wake umeenda chini zaidi ingawa hamna mahali pameandikwa hivyo,
 
Tutaelewana mi nilishaandika juzi hii iliopo inanajisiwa na kubakwa na haijafuatwa ipasvyo. Haitafanyika wakomae na utii wa katiba iliopo na kubadilisha vifungu ama kuweka vilaka
 
Back
Top Bottom