Lafacha
Senior Member
- Feb 3, 2017
- 195
- 275
Habari wana JamiiForums.
Nimekuja mbele yenu kuzungumza na wale wenye tatizo la tumbo kuunguruma, Mimi ni moja wenu na tatizo hili limenisumbua kwa muda sasa lakini hivi karibuni nimepata nafuu kwa kiasi kikubwa.
Mwanzo kabisa sikumbuki tatizo la tumbo kuunguruma lilinianzaje, sijui chanzo wala sababu isipokuwa baada ya muda kupita nikaja kufahamu baadhi ya vyakula nikila basi tumbo litaanza kuunguruma mwanzo mwisho mithili ya genereta iliyoishiwa mafuta.
1. Chai iliyochanganywa na tangawizi,
2. Chakula chenye viungo vingi,
3. Vitafunwa vya ngano,
4. Maziwa mgando kama ni machachu,
5. Maharage,
6. Kuchelewesha kula.
Basi, siku nikijichanganya nikala hiyo misosi apo juu, tumbo litasumbua balaa hata haja sipati vizuri (choo Napata cha mafungu mafungu kama mbuzi ).
Nilishawahi kuambiwa kuwa dalili ninazozipata ni dalili za kuwa na vidonda vya tumbo. Basi kama ni kweli ninachokitumia sasa iv kinaweza kuwa moja ya tiba nzuri ya vidonda vya tumbo.
1. Nimeacha kula misosi inayonisababishia tumbo kuunguruma,
2. Nimeacha kunywa vinywaji vyenye gesi,
3. Nimeacha kuchelewa kula , ratiba yangu ya jana inafanana na leo [ muda ni ule ule].
HITIMISHO: sijajua kama hiki ninachotumia kinaweza kikasaidia wengine wenye tatizo kama langu, ila napenda nawe ukajaribu kama itakusaidia utakuja HAPA KUTUPA MREJESHO, pia sijajua inaweza kuwa msaada kwa wenye stage zote za vidonda vya tumbo au kwa baadhi tu.
Jambo kubwa ninalolifanya mimi ni kuhakikisha kila siku kabla ya kula kitu chochote lazima ninywe class mbili za maji ya uvugu uvugu [umoto moto kama wa chai sema upoe kidogo tu sio sana].
Na muda wote ninao sikia kiu basi maji yangu ni ya uvugu vugu. Nina wiki moja tu toka nimeanza kutumia maji ya uvugu vugu na matokeo ni mazuri kwani siku nzima tumbo linaeza unguruma mara moja au mbili basi.
MAJI HAYA YAMEKUWA MSAADA MKUBWA KWANGU NAKUOMBEA KWA ALLAH NAWE YAKUSAIDIE .