Huu mchezo wa kuchelewesha ujenzi wa jengo la abiria airport Mza alaumiwe nani Wizara,TAA ya bw Mussa, au PPRA nani hasa iwapo Rais kishatoa maelekezo na pesa,Makalla naye kila siku hulisemea mpaka sasa NSSF nao wamealikwa, hapa kuna mchezo mchafu wa kuchelewesha. Kanda ya Ziwa tuamke,wananchi,wabunge na viongozi wa dini tulisemee kwa sauti kubwa kwa manufaa mapana ya taifa, miradi ya kimkakati kanda ya ziwa iko shida. Fikra potofu kuwa kanda ya ziwa ilipendelewa awamu ya 5 ni potofu na ni kichaka cha kujificha kuihujumu Mwanza angalia miradi ya DSm,Arusha,Dodoma Pwani Rufiji nk mbona haisemwi ni mingi na mikubwa na sasa Samiah Stadium inaanza kujengwa keshokutwa Arusha. Airport MWANZA ni mradi wa siku nyingi umezungumzwa zaidi ya miaka 30.Mama shtuka wanakuangusha kimkakati baadhi ya watendaji hususani kwa hili. Tatizo la uwanja huu Linafahamika,halibishaniwi. inasikitisha na kutia hasira kuzuia uchangiaji mkubwa wa mapato kupitia uwanja huu