baba anjela
JF-Expert Member
- Mar 17, 2013
- 431
- 310
Weka pichaNdugu zangu,
Kuku wangu wamekumbwa na tatizo la ukungu kwenye macho yao. Jicho alivimbi ,muda mwingi analifumba. Rangi ya kile kiini cheusi cha jicho kinakuwa kama kina ukungu.
Je, nitumie dawa gani?
Mkuu ulizingatia chanjo zote kila hatua ?
Huo sio ugonjwa ni tatizo la upungufu wa vitamins A. Kutibu hilo tatizo kuna dawa ya kuwapaka kwny jicho inaitwa 'Optclox' (ni tube flan hv) ukienda agrovet watakupa.
Kudhibiti hilo tatizo uwe una kawaida ya kuwapa vitamins za madukani.