Ni ngumu sana watu wengi kuelewa logic behind andiko lako. Ila ukweli uko hapa wazi watanzania tumetapeliwa; Upinzani ule wa Mwanzo sio upinzani tunaohuona sasa.
Unajua narrative iko wazi,wapinzani hawa walivishwa njaa kali sana wakati wa Magufuli na lengo ni kuwarahinisha, nakuhakikishia wanatepeta kwelikweli, na ni kweli walipitia chuma cha moto, wote ni mashahidi na kwa hilo nawapa pole. Sasa unajua adui muombee njaa, siku Mh Mbowe anatoka jela na kwenda moja kwa moja ikulu bila kupita popote na bila kuwa na mwakilishi yeyote wa chama chake, then tukaona vikao vya usuluhishi bila instant na reliable feeback of what exactly transpired in those closed door meetings.Pale ndipo nilipokata tamaa, waswahili wanasema kunusa harufu mbaya.
Kibaya tukasikia wapinzani wamelipwa malimbikizo yao yote ya miaka yote, wakaweza kujenga angalau kajengo ka chama, kiufupi Chama cha upinzania kikishaanza kuwa financed na chama tawala kwa njia yeyote ile basi hicho kinakuwa chama cha kuverify nchi ina utawala wa sheria na uchanguzi wa kidemokrasia.
Hakika tunasafari ndefu ya ukombozi wa mtanzania. Sitegemei hii safu ya sasa ya upinzani kuleta changes;the real changes.
Nilishaandika hapo nyuma, upinzani inabidi ubadilike, tatizo letu tunakosa vichwa zaidi vitakavyoleta vitu vingine vipya. Ni kweli kuna baadhi ya vichwa kwenye safu ya upinzani, ila haviwezi kutusua peke yao.
Tunahitaji vichawa vipya; mfano vijana wa TEHAMA watakaotranform policies, advocacies na strategies zao kitehama na kidigitali kwa kutumia platform zetu nyingi tulizonazo,, tunahita strategic thinkers , mind players, manipulators, hypnotizers watakaoweza kucheza na mindset weak za watanzania kuwatranform kwa kutumia real and recent life challenges zinazotukabili. Watanzania wengi hawawezi kulink umasikini, ujinga, taabu za maji, umeme, sukari na maisha duni na serikali iliyopo; wengi tunafikiri ni mpango wa Mungu au ni nature imetaka sisi tuwe hivi; tumeikubali hii hali ( STATUS QUE)
Hii ni golden opportunity kwa vyama pinzani, suala la umeme ni chance nzuri kushow-case the magnitude, the negative impact to our daily life, most importantly the alternatives if given the chance to lead, kwa sababu umeme ni eneo mtambuka na linagusa maisha yetu woote watanzania moja kwa moja bila kutofautisha tajiri na masikini;ingawa kiwango cha maumizu kinatofautiana.
Sijakataa katiba, ila je watanzania wengi wanaelewa logic ya katiba, ni wangapi hao? ila ukisema umeme, kila mtu anaelewa, ukisema njaa na umasikini kila mtu anaelewa, ukisema elimu duni kila mtu anaelewa, ukisema makazi hafifu, kupanda kwa ugumu wa maisha nakwambia kila mtu atakuelewa. Cha muhimu ni namna tunavyowasilisha hoja hizo, uchanguzi wa maneno na tafsida, ni wakati gani tunatoa hizi mada, platform zipi ni relevant, na tunazirudia mara ngapi kwa siku, kwa wiki, kwa mwezi , kwa mwaka?. Very very important.