tutaishi milele
Member
- Dec 26, 2015
- 68
- 46
Wakuu kwema, wajuzi wa mambo ya umeme msaada tafadhali. Kimsingi nyumba ninayoishi haijafikiwa na umeme wa tanesco na sababu ni mtaa ninaoishi umepitiwa na mradi wa Rea na mimi sikuwa mnufaika kwakuwa nilichelewa kuhamia hivyo nimeambiwa nisubiri miezi 18 tangu tarehe ya kukabidhiwa kwa mradi ndipo ntaruhusiwa kufanya maombi.
Concern yangu ni juu ya huu umeme wa solar nilioamua kufunga baada ya kukutana na changamoto kama nilivyoeleza. Nilitafuta fundi kwaajili ya kunipa tathmini ya matumizi yangu na mahitaji ya mfumo wasolar.
Fundi nilimueleza nahitaji kutumia friji ndogo, taa zizipongua nane, tv pamoja na laptop na alinishauri kuwa nahitaji solar isiyopungua wat 500 pia betry N200 na inveter wat1000 na charger controler.
Na pia nyumba yangu nilikuwa nishafanya wiring kwaajili ya huu umeme wa tanesco lakini fundi alinihakikishia kuwa haina shida ntatumia wiring hiyohiyo.
Kwa kufuata ushauri wa fundi nilinunua betry n100 mbili inveter hiyo ya wat1000, charger controler na solar wat 560 nikafunga na ilikuwa kiangazi jua la kutosha lakini mwenendo wake nikawa siulewi sababu niliweza kutumia tv taa na laptop na mwisho ilikuwa mida ya saa sita usiku inazima.
Nikatafuta fundi mwingine akabadili uelekeo wa solar kutoka upande ambao haukuwa na jua sana akaiweka upande wenye jua hali ikawa nzuri kidogo japo sio sana na akanishauri kubadili inverter toka hizi za dukani akaniuzia inverter aliyoitengeneza yeye imeleta mabadiliko kidogo sana.
Naomba kujua kama hali hiyo ni sawa kwani naona kama nina mfumo mkubwa lakini matumizi madogo na bado sitoboi ikizingatia kwenye matumizi yangu friji sijawahi kutumia kabisa.
Naambatanisha picha ya jinsi nilivyofungiwa mfumo pamoja na inverter ya zamani.