Tatizo la vipele vinavyotokana na kunyoa nywele kichwani chini ya kisogo (Acne Keloidalis Nuchae)

dah,kumbe ni janga kwa watu wengi....wapi mkuu MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
Paka medicated cream inaitwa Betacort-N,nilikuwa navyo vikapotea jumla,sasa sijui vyako viko kwenye extent gani,kwani mimi vilishanitokea kama mara mbili na nilipotumia hiyo dawa ika-work very successful.
 

Pole sana ndugu yangu.Mimi nilikuwa navyo nimetumia dawa moja kutoka Bk NIMEPONA KASIBA wao BK wanaita nshundo.Anyway nPM nikupedata zaidi na jinsi tunaweza kuwasiliana
 
Paka medicated cream inaitwa Betacort-N,nilikuwa navyo vikapotea jumla,sasa sijui vyako viko kwenye extent gani,kwani mimi vilishanitokea kama mara mbili na nilipotumia hiyo dawa ika-work very successful.

Nakumbuka nmeshawahi kutumia hiyo dawa kipindi cha mwanzoni kabisa tena nilikuwa natumia na dawa flani ya kumeza,sikumbuki jina ila ilikuwa ya kijani kijani hivi, ilikuwa vinapungua tu, dawa ikiisha vinarudi kama kawa ikafika kipindi nkachoka, nkabadilisha dawa nyingine nayo hali kadhalika, nilichoona hizo dawa zinatuliza tu baada ya muda vinarudi kama kawaida
 
Pole sana ndugu yangu.Mimi nilikuwa navyo nimetumia dawa moja kutoka Bk NIMEPONA KASIBA wao BK wanaita nshundo.Anyway nPM nikupedata zaidi na jinsi tunaweza kuwasiliana

tayari ndugu, nasubiri kusikia kutoka kwako
 

itabidi nimshauri mume wangu atumie ulivyotumia,na yeye vinamsumbua sana,kila mara anapaka dawa vinapona akienda salun tu vinarudi
 
Pole sana ndugu yangu.Mimi nilikuwa navyo nimetumia dawa moja kutoka Bk NIMEPONA KASIBA wao BK wanaita nshundo.Anyway nPM nikupedata zaidi na jinsi tunaweza kuwasiliana
unataka akupm ili umpe jina la dawa, unaona ukiweka hapa peupe watu watafaidika? watu wabinafsi bwana...saidia wenzio wenye tatizo, kuna wengi hapa wanahitaji kama hilo, hapa ni jf where we dare to talk openly, sasa mambo ya sirisiri ya kupm ya nini? weka jina hapa peupe ili watu walijue wakatafute iyo dawa, kwani wewe pia si unafaidia na vingi tu vya wenzio wanaoweka mambo mazuri hapa na haulipii chochote kwao?....acha ubinafsi.
 
Habari wadau,

Katika kunyoa nywele kichwani imenitokea nimeota vijipele nyuma ya kichwa karibu na shingo. sasa kila nikienda pharmacy na dispensary wananipa dawa ambazo zimeshindwa kunisaidia. Hali hii imekuwa ikinikosesha raha sana, nimepanga kwenda hospitali kubwa lakini nimeona kabla sijaenda huko inawezekana kuna mtu akanipa ufumbuzi rahisi wa kuweza kutatua tatizo hili. Kwa yeyote mwenye ufumbuzi wa kuondoa vijipele hivyo naomba anisaidie.

Wasalaam
 
umepanga kwenda hospital. nenda mkuu humu utaombwa picha tu. cc mzizimkavu

nimeona kabla sijaenda huko inawezekana kuna mtu akanipa ufumbuzi rahisi wa kuweza kutatua tatizo hili

Mkuu sentensi hii wakiipa umuhimu naamini wataweza kunisaidia.
 
Mkuu ivo vipele usivitumbue la sivyo utaota linyama nyuma ya Shingo. Kwa uchunguzi wangu niligundua ugonjwa huu unaambukizwa kwa kupitia mashine za kunyolea masaluni Nina ushahid wa watu waliotoka linyama nyuma ya shingo.
 
Mkuu ivo vipele usivitumbue la sivyo utaota linyama nyuma ya Shingo. Kwa uchunguzi wangu niligundua ugonjwa huu unaambukizwa kwa kupitia mashine za kunyolea masaluni Nina ushahid wa watu waliotoka linyama nyuma ya shingo

Kaka sivitumbui ila kuna wakati vinauma ila wakat mwingine kama vinakauka hivi then vinarudi tena. sasa sijajua hatima yake
 
Chukuwa kitunguu Saumu Ukitwange mpaka kiwe laini kisha Uchukuwe maji ya moto Uoshe sehemu zenye vipele Ufanye kama Unasugua

Kaka asante kwa ushauri wa tiba, sasa hiyo tiba dozi yake ipoje? namaanisha nioshe kwa siku mara ngapi na kwa muda wa siku ngapi? Asanate sana MziziMkavu
 
Jaribu dawa za asili zaidi, nina rafiki yangu nae anatatizo hilo, alishatumia dawa nyingi tu za hospitali lakini bado vipele havijaisha, bahati mbaya amekuwa mbishi kutumia dawa za kiasili lakini nadhani mimi hizo zinafaa.

Pole
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…