JACKLINE CELESTINE KITALE
Member
- Jul 29, 2021
- 81
- 158
Kwa muda mrefu sana watoto wetu wamekuwa ikiwalazimu kubeba mzigo mkubwa wa madaftari wakati wa kwenda shuleni.
Na kwa watu wengi imeshachukuliwa kana kwamba ni hali ya kawaida kumuona wanafunzi akiwa amebeba begi kubwa na zito lililojaa madaftari mengi, na wengi wamekuwa na dhana potofu ya kwamba mwanafunzi anaye beba madaftari mengi ndiye ambaye anasoma kwa bidii na yule anaye beba machache au asiyebeba kabisa hasomi kwa bidii, huenda kucheza tu shuleni, kitu ambacho si sahihi.
Kwa dhana hii tunasababisha watoto wetu wapate madhara mengi ya kiafya kwasababu ya kubeba mzigo mzito mgongoni. Mtoto anaweza kupata matatizo ya uti wa mgongo, maumivu ya shingo (Neck Pain), maumivu ya kiuno, maumivu ya mgongo kiujumla na hata kupata kibiongo.
Hii ni changamoto ambayo sisi kama Wazazi, walezi, ndugna, walimu, na serikali kiujumla inabidi tushirikiane kuitatua ili watoto wetu waepukane na haya matatizo. Tukianza na walimu, walimu wanatakiwa kutengeneza ratiba rafiki kwa wanafunzi iliyo na masomo machache au yakujitosheleza na siyo masomo mengi. Na kwa wazazi ni muhimu kuhakikisha watoto wao wanafuata ratiba hizo zilizo tengenezwa na walimu na kuhakikisha kuwa watoto wao wanabeba madaftari yale tu ambayo wanatakiwa kusoma siku hiyo na siyo vinginevyo.
Kwa shule nyingi za binafsi yaani private schools, wamefanikiwa kupunguza hili tatizo kwa wanafunzi wao. Walichofanya ni kutengeneza makabati (yaani Cabinets) ya kila mwanafunzi ambazo hukaa nje ya madarasa yao. Haya makabati huwa yametengenezwa kwa chuma na kila mwanafunzi hupewa ufunguo wa droo yake ambayo anatakiwa kuitunza. Kwahiyo mwanafunzi anakuwa hana haja ya kubeba madaftari mengi kwa kuwa yote anayahifadhi kwenye kabati lake na akihitajinya kusomea anachukua machache na mengine anayaacha pale yakiwa salama.
Nadhani hii Ni njia nzuri Sana na ninaiomba serikali iweze kuiga na kuifanya hii kwenye shule zake zote za kiserikali ili wanafunzi wasiendelee kupata hii changamoto ya kubeba madaftari mengi kila siku.

Upvote
6