Tatizo la Wanawake Kupata Maumivu Wakati na Baada ya Kujamiiana: Fahamu Sababu na Suluhisho la Tatizo

aorry..mi nna tatizp la kisailolojia..but mbona maumivu nnayopata ni kama vile muwasho wa pilipili mdomoni?
 
Huo muwasho umeanza Lin??
sijazoea kukutana kimwili...nlikua alone miaka mingi..sasa nkajaribu but kila wakati wa shughuli naumia..nna maumbile madogo kiasi kuingia had afosi..
ataenda but baada ya dakika chache naanza kuhisi maumivu..imagine unavokula pilipili mdomoni..ule mwasho sasa ndo similar na nnavohisi huku chini.but kesho yake unatoweka
Atuambie vizuri...

Huo muwasho umemuanza lini Na hutokea wakati wa kufanya tendo tu au hutokea wakati wowote ?
 
Una umri gani?
 
Mkuu ndo umeamua kuja nianika huku jf baada ya siku ile kuniona kwa bahati mbaya nikijisaidia pale kichakani au... Ila siku hizi sikimbiwi tena kama kipindi kile kwa sasa nimesha jua namna ya kulitumia vizuri umbile langu
 
Habari zenu wana JF.

Nina mpenzi wangu toka nikutane nae analalamika maumivu makali wakati wa tendo na hata baada ya tendo maumivu yanadumu kwa takribani cku mbili mpaka tatu. Hata nimuandae vp lakini tukianza tendo tu basi hali inakuwa sio nzui kwake. Sasa nimejaribu kufikiria nikaona yawezekana tatizo likawa ukavu sehemu zake za uke hivyo naomba msaada juu ya kutatua tatizo hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaijua historia yake mkuu? Mmeshawahi kufanya vipimo vyovyote vikiwemo vya mkojo? Angalia na dushe lako usikute ni futi 9
 
Unaijua historia yake mkuu? Mmeshawahi kufanya vipimo vyovyote vikiwemo vya mkojo? Angalia na dushe lako usikute ni futi 9
Yah alishanieleza kila kitu kuhusu yeye na alikuwa msichana bado. Na nilishawahi kukutana na binti mwingine b4 hakuwahi lalamika so kuhusu size sio, iko normal.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuyenge wako unaweza kuwa mkubwa sn pia.
 
Ikiwa unapata maumivu wakati au baada ya ngono, mwili unajaribu kukuambia kwamba kuna kitu hakiko sawa, kwa hivyo usipuuzie.

Nenda kwamwone Daktari.

Ikiwa unaona kuzungumza juu yake kuwa aibu, kumbuka kuwa madaktari wapo kushughulika na matatizo kama haya.
Maumivu wakati wa ngono yanaweza kuathiri mahusiano yenu.
 

UNAUMIA WAKATI WA TENDO LA NDOA? SOMA HAPA!


HII ni hali ambayo mwanamke anakuwa na hamu ya kufanya tendo la ndoa lakini anapata ugumu kutokana na maumivu makali anayopata.

Hali hii inatokana na kubana au kukaza kwa misuli ya uke lakini pia inaweza kusababishwa na matatizo ukeni.

Mfano endapo kuna michubuko au vidonda au kasoro yoyote ya uke, aidha uke ni mdogo au maumbile ya uke hayana uwiano na uume. Tatizo hili huwapata wanawake wa rika zote ilimradi tayari yupo katika umri wa kuzaa.

TATIZO LINAVYOGAWANYIKA
Tatizo hili la maumivu wakati wa tendo la ndoa limegawanyika katika maeneo makuu mawili. Kwanza ni Primary Dyspareunia .

Hapa mwanamke anakuwa hana historia ya maumivu wala hana historia ya kuwahi kufanya tendo hilo ndiyo, kwanza anaanza. Kitaalamu hali hii ya maumivu huitwa Honey moon Dypareunia au maumivu ya fungate na hutokea mara tu anapoanza kujamiiana kwa mara ya kwanza. Katika hali hii misuli ya uke inaweza kubana kutokana na michubuko au kuchanika ubikira au hata kuchanika upande wa chini wa uke na wakati mwingine michubuko hutokea katika tundu ya mkojo.Hali ya michubuko inaweza kuwa mbaya na ikajitokeza hata kwa kugusa tu upande wa nje wa uke.

Maumivu yakiendelea au yakizidi husababisha mgonjwa apate matatizo ya kisaikolojia kiasi kwamba huanza kuogopa tendo lenyewe na kuhisi endapo atalifanya ataumia. Tatizo hili likileta michubuko kwenye njia ya mkojo husababisha maambukizi sugu ya kibofu cha mkojo kutokana na michubuko ya mara kwa mara ya tundu ya mkojo.

Maumivu ukeni hutokana pia na maandalizi mabovu kabla ya tendo ambapo uke unakuwa haujalainika kwa kutofanya romance ya kutosha, kutofanya tendo hilo kwa ustaarabu, yaani kutumia nguvu au endapo mwanamke atakuwa na maambukizi ukeni mfano fangasi ambayo huambatana na kutokwa na uchafu ukeni na muwasho, magonjwa ya uke kama kuvimba kwa tezi za uke, kuvimba kwa mashavu ya uke au hali yoyote inayomwondolea amani mwanamke pale ukeni inaweza kumfanya kisaikolojia aathirike na kuhisi maumivu wakati wa tendo.

Michubuko ukeni au kuhisi moto ukeni wakati wa tendo la ndoa kunaweza kusababishwa na matumizi ya vilainishi visivyofaa au kuumwa kutokana na uwepo wa vinyweleo virefu ukeni na endapo havikupunguzwa vitaingia ukeni wakati wa tendo na kukuchubua. Kasoro katika ubikira pia husababisha mwanamke ahisi maumivu wakati wa tendo.

Maumivu haya huwa hayahusiani na yale ya awali ya fungate na wakati mwingine huanza baada ya kipindi kirefu cha miaka mingi tangu uanze tendo la ndoa na wengine huwa na tatizo hili tayari wana watoto. Chanzo cha tatizo hili ni ukavu ukeni, umri mkubwa wa mwanamke na kusinyaa kwa misuli ya uke.

Matatizo haya isipokuwa la umri mkubwa hutokea katika umri wa kati na tayari mwanamke anayo historia ya kuwa katika mahusiano na hata tayari ana watoto. Umri mkubwa tunaouzungumzia ni zaidi ya miaka hamsini. Kubana misuli ya ukeni hutokana na makovu baada ya kushonwa msamba au kuongezewa njia wakati wa kujifungua au upasuaji wa kurekebisha fistula pia husababisha tatizo hili.

Vyanzo vingine vya maumivu haya ya tendo la ndoa ni kushuka kwa kizazi ambapo mwanamke atahisi kitu kama gololi ukeni wakati akijisafi sha au kuhisi kizazi kinasukumwa wakati wa tendo, kugeuka kwa kizazi, matatizo katika tabaka la ndani la kizazi, maambukizi sugu ukeni ambapo uchafu na muwasho ukeni hujirudiarudia, matatizo katika njia ya mkojo na maambukizi katika viungo vya uzazi ’PID’ husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Matitizo ya kisaikolojia husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa pale ambapo misuli ya ukeni itakaza na mwanamke anapochunguzwa huwa hana tatizo au kasoro yoyote ukeni. Matatizo katika mishipa ya fahamu ya ukeni, kuogopa tendo lenyewe kuhisi utapata maumivu au kama kuna historia ya kuingiliwa kwa nguvu na ukaumia, kutokuwa na taarifa sahihi kuhusu tendo la kujamiiana, yote haya na mengine mengi humharibu mwanamke kisaikolojia na kujikuta anaanza kuhisi maumivu hata kabla ya tendo lenyewe kwa kuingiwa na hofu.

Hali nyingine inayoweza kumfanya mwanamke aathirike kisaikolojia na asiwe tayari kwa tendo na hata akilifanya apate maumivu ni kuogopa kupata ujauzito wakati hayupo tayari kwa hilo, kuogopa kupata maambukizi, kulazimishwa penzi endapo haupo tayari na mwanaume uliye naye na kuhisi kuna tofauti ya maumbile na mume uliyenaye.

Endapo mwanaume anakukwaza kutokana na kutokwa na jasho jingi sana wakati wa tendo, kutoa harufu mbaya ya pua, kinywani, makwapani au sehemu zake za siri, huwa na magonjwa ya ngozi au hata mwilini mwake, matatizo haya huweza kumwathiri mwanamke kisaikolojia na asifurahie tendo na kutotoa ushirikiano wakati wa tendo na kupata maumivu.

UCHUNGUZI Tatizo hili ni pana sana, unaweza kuhisi una kasoro au maambukizi kumbe tofauti. Kwa hiyo basi ni vizuri uchunguzwe kwa umakini katika kliniki za madaktari wa akina mama katika hospitali za mikoa ili kujua chanzo halisi cha tatizo.

Chanzo: GBP
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…