GM7
JF-Expert Member
- Jun 26, 2009
- 492
- 24
Hapo kwenye bold. Hata mimi yapata miezi mitatu tangu nifunge ndoa na mke wangu tena ya kikristu na tulikuwa hatujawahi kuvuliana nguo mpaka siku ile ya ndoa. Hata mimi ilinitokea mwezi wa kwanza ukapita bila majibu, haadaye mwezi wa pili ukapita bila majibu na kwa mbali nikaanza kuwa na wasiwasi lakini baadaye baada ya kutembeatembea huku na kule kama vile JF na blog mbalimbali za afya nikagundua kitu na baadaye nikafuata ushauri unaotolewa na hatimaye mwezi wa tatu (namaanisha huu mwezi March) nikapata jibu na mke wiki mbili za mwanzo akaanza kuonyesha dalili za ujauzito. Nashukuru kwa elimu tunayoipata kupitia mitandao mbalimbali hasa JamiiForums kwa kweli inasaidia.Yapata takribani miezi mitatu tangu nifunge ndoa.mimi na mme wangu tumejitahid sana kutafuta mtoto tangu siku ile ya ndoa hadi leo bila mafanikio.inawezekana mtu kuwa criaz kutafuta ujauzito miezi mitatu mfululizo bila mafanikio?? Je yaweza kuwa kuna tatizo lingine?? Hadi leo hii hatujachukulia kama tatizo,kwa upande wa mwenzangu cjui anafikiria nini ila kwa mimi nina hofu mno sababu kila nikipima upt napata negative,cna amani ata kidogo. Naomben ushauri wenu jamani, hii ni kawaida? Nifanyeje??
Shemeji yangu Sikwepeshi, usiwe na wasiwasi bado mapema ila kuna maswali ningemuuliza huyo mdogo wangu (bila shaka) ili kuweza kufanikisha suala lenu nadhani linafanana na la kwangu. Labda baadhi yake unaweza kuyajibu.
Je, mnapata mshahara (yaani ku-du) kila siku mfululizo mpaka siku yako ya Ovulation?
Je, mnapata mshahara siku inayofaa yaani siku ya Ovulation au walau siku moja kabla au hata mbili kabla na pia unaifahamu vyema siku ya Ovulation?