Tatizo letu liko wapi?

Tatizo letu liko wapi?

Tusiwalaumu sana hawa vijana, Tatizo ni watawala kupuuzia mfumo wa elimu ndio maana mtu anashindwa hata kuandika application letter kitu mabchao alitakiwa ajifunze darasa la tatu na la nne. Kingine ni exposure na hii siyo kwa vijana tu, mbona hamuulizi watu wenye degree tena wengine za Havard kama Andrew Chenge aliingia mikataba ya kipuuzi pamoja na kwamba alipewa rushwa, Sijui ni kiasi gani cha rushwa kulifanya asaini upuuzi huo. Juzi bungeni wamepeleka mswaada wa baraza la usalama uliojaa makosa ya kiuandishi kama Capital letter, matumizi ya nukta, koma etc. Na hao waliopeleka si watu waliosoma siku nyingi nao tatatizo nini?
 
Sidhani kwa namna hii ni msaada sana. Labda tuwashauri wajenge tabia ya kujisomea novels,kuangalia movies za kimombo na kujifunza lugha hiyo. Tatizo ni kwamba wengi wetu tunapenda kubeba novel kubwa na kutishia wenzetu kwa kiswaglish. Nadhani tuambizane ukweli na ndio maana kuna nchi nyingine hawahitaji TOEFL lakini kwa kwetu ni kitu hakiepukiki. Tafadhali tuambizane ukweli kwani hata kiswahili chenyewe kinaelekea kutushinda pia.
 
Sisi Watanzania ndio ukikosea kuandika hata spellimg inakuwa very big issue (nongwa). Wazungu mara nyingi huwa wanaignore makosa kama hayo na kuangalia kama kweli wanaweza kutoa msaada au la.

Sitetei the obvious mistakes lakini vile vile siyo lugha yao ya kwanza.

Tumejenga culture ya kusaidiwa na wazungu kwa kila kitu, inabidi tuibadili hii na kuanza kuwa na funding organisations sisi wenyewe kwa sababu hata wazungu ni wachache sana wanaoweza kutoa funds binafsi ni organisations walizozianzisha.

Pengine hata hapa JF tunaweza kuanzisha education fund na kuweka criteria jinsi ya kuipata. We can do it for starters i.e ku-sponsor 1/2 student every year. Mathalan tuko member karibu 4000 kila moja akitoa dola 10 kwa mwaka ni 40,000.00 ambazo wanafunzi wawili watakuwa kwenye masomo kila mwaka kwa uhakika.
 
Mbaya zaidi ni kutojua kwamba hawajui vinginevyo wangezingatia kwamba kuomba kitu kwa maandishi inahitaji taaluma, kujiridhisha na lugha ya kushawishi ni bora basi wangeomba kuandikiwa angalau katika hiyo hatua ya maombi halafu hayo masuala mengine ije kuwa mbele kwa mbele. Hivi kweli graduate anaandika re quest, per suing nani kawaambia hayo ni maneno mawili tofauti? Ila tukumbuke suala hili ni ugonjwa wa kitaifa sio suala lao kama wanafunzi.

Tanzania yenye wasomi waliobobea kwenye fani mbalimbali inawezekana?
 
tuishauri serikali kuruhusu matumizi ya lugha ya KINYAKYUSA kinaweza kikawa chepesi zaidi hii lugha ya kigeni
 
Badala ya kuwacheka na kuchumbua walioandika, mimi naona muwakaribishe hapa JF The Home of Great Thinkers tuwasaidie...si ndio kazi zetu kama wanajamii!!

Mbona tumeshasaidia wengi!!
 
Kwa mtazamo wangu, naona tatizo si lugha peke yake. Naamini hata kama application zingekuwa za kiswahili, bado baadhi ya graduates wangeandika vitu vya ajabu. Tatizo letu liko kwenye mfumo mzima wa elimu. Kama tumeona shule siyo taasisi bali ni majengo, unategemea wahitimu wa majengo watakuwa na uwezo wa kujieleza? Tunaambiwa kila kata ina shule ya sekondari, kwa maana ya majengo, ukija kwenye taaluma, maabara, vitabu vya kiada/ziada, maktaba na utawala hakuna kitu, ni aibu tupu.

Ili kupata wataalamu competent tunahitaji wahitimu ambao siyo matokeo ya elimu ya kukaririshwa, kununua mitihani, kuhongwa na mengine mengi yanayoendana na mfumo hasi. Naamini kabisa tuna vijana ambao wako competent na wasingekuwa na shida kuandika maombi kama hayo, lakini barua hizo zinaonyesha ukubwa wa tatizo.
 
Si mchezo!

Hali hii inasikitisha, inakera, inauma, inauzunisha na inatisha. Achia mbali hicho kiingereza kuwa rubish kwa baadhi yao, wanafuata utaratibu gani kuomba hizo scholarship?. Yani mwanafunzi kwa chuo kikuu hajui procedure ya kuomba scholarship, mwingine is about to do Phd.
Nimesoma kwa scholarship na wengine wengi tu humu kwenye forum wamesoma kwa scholarship naamini, nadhani wanajua ni jinsi gani ilivyo mbinde kupata scholarship. Lazima unandike statement za nguvu, ufuate masharti ya scholarship kama vile deadline, requirements, nk. Uwezi pata scholarship kwenye front page kama hivyo kwa kuandika matatizo yako ya kimaisha n.k.
Kuna scholarship za sweden zinapatikana kwenye www.studera.nu, zipo za idb, zipo za aga khan, zipo za commonwealth, zipo za ubalozini, na nyinginezo nyingi tu. Ukifuata masharti na kama una qualification zinapatikana tu wala hazihitaji kujuana.

Itabidi kutoa lesson ya scholarship ili kunufaisha na wenzetu kuliko kuendelea kukipaka namna hii.. Ntaleta links na procedure....


Regards
 
pro-kiswahili hapa wamepata hoja ya kusimamia mf. akina Companero na wenzake

tunazo hoja za kutosha mwanaharakati, hiyo ni nyongeza tu - hebu msikilize sheikh shabaan robert:

Kwa bahati mbaya lugha hizi mbili zinakafiliwa sasa kupigana kama chongowe na nyangumi. Wasio Waafrika wanadai Kiingereza kuwa bora nacho kitumike katika halmashauri. Waafrika wataka matumizi ya Kiswahili, kwa sababu kina usawa wa lugha mbali mbali za wenyeji ndani yake. Kwa hivi kina ubora wake ufaao kutumika katika halmashauri pia. Zaidi yake watu wa pande hizi hawana urithi mwingine wa haki kuliko Kiswahili. Katika kila pigano upande mmoja hushinda. Hapana shaka Kingereza kitashinda, lakini yatabiriwa kwamba ushindi wake utakuwa wa kitambo tu. Hayamkini kwamba wenyeji wa mahali popote katika ulimwengu waweza kuridhika kuishi katika lugha ngeni milele.[2]
 
Badala ya kuwacheka na kuchumbua walioandika, mimi naona muwakaribishe hapa JF The Home of Great Thinkers tuwasaidie...si ndio kazi zetu kama wanajamii!!

Mbona tumeshasaidia wengi!!
Jamani hebu tuelewani hapa, sidhani kama kuna mtu anawacheka, mimi binafsi siwacheki hata kidogo maana hata mimi siko perfect, ila na express shock nilio nayo maana nimegundua tatizo tulo nalo kwenye mfumo mzima wa elimu ni kubwa sana kiasi kwamba sijui tutawezaje kufaulu kimaisha. tunahitaji mawazo yenu wote nini kifanyike kuepusha aibu za hivi. Maana si hao tu ni wnei tu tunaongea broken english na kuandika vitu visivyomake sense, sasa na hali hii ya soko huria tunaweza?
 
. Zaidi yake watu wa pande hizi hawana urithi mwingine wa haki kuliko Kiswahili.
Ndg. Companero hoja zako zina mashiko sana ingawa kuna madhaifu kwenye kuishikilia hoja hii. Kwanza suala la urithi tuna urithi mwingi sana alichofanya Shabaani ni kuonyesha na kuzungumzia kwenye eneo lake la kujidai eneo la lugha angezungumza Nyerere angezungumzia ardhi kama urithi wa kipekee.
Ingawa nakubaliana na Shabaani kwenye kuwa na lugha moja ya kutuunganisha wakati wa aina ya dhiki au furaha yoyote ile, na lugha hii kweli yaweza kuwa Kiswahili lakini je kitatusaidia kusonga mbele ndani ya mfumo huu wenye madhaifu makubwa na ya wazi lakini yameshindwa kuonekana na viongozi wetu?
Najua utakuja na hoja ya kuwa siku moja watanzania watajuta kwa kukitosa Kiswahili, nakubaliana na wewe lakini ukumbuke kuwa sio hiari yao ila ni msukumo wa mfumo wa dunia ya leo. Wewe unafikiri tunaweza kusimama kwenye changamoto za utandawzi na lugha ya Kiswahili?
Mwisho nakiunga mkon kiswahili sana lakini tulikosea na bado tunakosea kwahiyo ni lazima kurekebisha na sio kukilazimisha kitumike pasipo kukiwekea mazingira mazuri
 
sasa na hali hii ya soko huria tunaweza

Na hili ndilo tatizo kubwa sana kwenye nchi yetu kwa sasa, kuna matundu mengi sana yamesbabishwa na mfumo huu wa soko huria hasa kwenye maeneo ya vijijini. Kwa mfano ukienda vijijini vikundi vya miradi vingi vimekufa pamoja na vyama vya ushirika vya mazao mbalimbali vilivyoanzishwa na wanavijiji kwaajili ya kuzalisha na kununua mazoa na kuyauza kwa pamoja. Soko huria limevamia kwa kasi ya ajabu sana kiasi kwamba hata ule ushirika wa kukaa na kujadili maendeleo baina ya wanavijiji umekufa kutokana na kukua kwa daraja la mabepari uchwara wanaoingilia uhuru wa mawazo na wa kufanya kazi kwa wanavijiji hawa.

Ukweli ni kuwa baadhi ya wanavijiji wamegundua hili tatizo lakini kujikwamua nalo ni ngumu sana kutokana na mfumo huu kupigiwa chapuo na wanasiasa na viongozi wa ngazi za juu wanaotembelea maeneo haya kama vile madiwani, wabunge, wakurugenzi watendaji, baadhi ya taasisi zisizo za kiraia na watu mbalimbali wenye ushawishi kwenye jamii.

Na hili ndilo tatizo ambalo hata kwenye lugha ya Kiswahili lipo kwani kuna kuongea sana kwa viongozi wetu pasipo kutekeleza hoja zao, kwenda kuhutubia umoja wa mataifa kwa Kiswahili ni hatua ndogo sana katika kukiendeleza Kiswahili ila kwakuwa watanzania tunapenda sana kuridhika na hatua ndogo basi ubaki hapo hapo tumetuama kama maji ya mvua.
 
Nilikuwa nafungua website ya Irish embassy nikakutana na masahibu hayo hapo chini tena page ya kwanza kabisa. Kwa kweli nimejisikia vibaya bna kutafakari sana. Tuna tatizo gani? hebu angalia waliyoyaandika hawa ndugu zetu, kwa moyo wa dhati kabisa wanataka sponsorship, lakini unadhani kwa jinsi walivyoandika, yani first impression hiyo sponsorship wanaweza kupata? I mean, wote ni ma graduate hao siyo form four! No wonder watanzania tuna long, long way to go. Je tufanyeje jamani kusolve matatizo ya kihivyo? Na east african cooperation hii tutapona kweli, hata kazi tutapata? Think people, think hard.
Sat, 30 Jan 2010 12:37 PST
APPLICATION FOR THE SPONSORSHIP
I would like to apply for the sponsorship for master
degree 2010/2011 academic year.

Currently I am a third year student per suing degree in Bsc Agricultural education and extension at Sokoine University of Agriculture

Sat, 30 Jan 2010 12:25 PST
LOOKING FOR SPONSERSHIP
I am a Tanzanian aged 33 years old, per suing Bsc Agricultural education and extension third year at Sokoine University of agriculture.

I would like to apply for the sponsorship in master for the coming academic year.

Sat, 30 Jan 2010 04:42 PST
SPONSORSHIP FOR BACHELOR IN EDUCATION
I'm an Tanzanian woman.I'm a student at Muslim university of morogoro in B.A.EDUCATION. with registration number of MUM/T/BAED/09/1423. I fail to get loan from loan board. I tried my best to insure my present at university in this accademic year but i face difficult life for tuition fee, meals and stationary expenses.I lost both my parents so i have no one to help in my studies. I request you to sponsor me so that i can be able to continue with my studies.
I hope you will consider my request
your
Thu, 28 Jan 2010 04:15 PST
LOOKING FOR SPONSORSHIP
Hi!
I am a girl aged 32years. Im looking for someone to sponsor me in buchelor of science in nursing in academic year 2010/2011 in St Johns University of dodoma in Tanzania. Curently im working at mafiga Health Centre in Morogoro Municipal.
Thank you in advance if my request will be cocidered positively. my email is Thu, 28 Jan 2010 04:11 PST
LOOKING FOR SPONSORSHIP
Hi!
I am a girl aged 32years. Im looking for someone to sponsor me in buchelor of science in nursing in academic year 2010/2011 in St Johns University of dodoma in Tanzania. Curently im working at mafiga Health Centre in Morogoro Municipal.
Thank you in advance if my request will be cocidered positively.
Sat, 23 Jan 2010 01:40 PST

LOOKING FOR A SPONSORSHIP
I am a teacher hereat Pemba isle.I am a graduate from the state univrsity of Zanzibar. I would like to ask for a sponsorship from any recognised internal or foreign agency/institution,embassy or individual
person(s) who has potential and kind-herarted so that i can improve the standard of my education. Educating a girl is to build the stable future of African society and the world at large. Thu, 21 Jan 2010 23:31 PST

Re; SPONSORSHIP FOR MASTERS INTERNATIONAL HORTICULTURE
I re quest the Embassy to finance my studies at Hasden Bosch university for Msc.course.I m the employee of Rufiji-District council as Crop officer.
Thu, 21 Jan 2010 08:39 PST
SPONSORSHIP FOR MASTERS
Iam a Tanzanian girl aged 26,am lookina for sponsership for joining LLM,in accademic year 2010,currently aim taking school of law hosted by UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM.My E mail is Wed, 20 Jan 2010 03:06 PST

SPONSORSHIP/SCHOLARSHIP
I am Tanzanian ageg 39,I am looking sponsorship/scholar ship for joining pre phd in finance and economics in accademic year 2010/11. For the time being Iam on the way for completion my master degree at university of strathclide uk in colaboration with IFM Dar-es-salaam Tanzania.

ZANZIBAR-TANZANIA
Mon, 18 Jan 2010 03:29 PST
REQUEST FOR MASTER SCHOLARSHIP
I'm a Graduate General science Majoring Microbiology and Zoology , sincerely i would request to be considered for chances that will given out by your Embassy. I'm interested in Masters of any Health issues such as Medical Microbiology, Parasitology,Biotechnology and Environmental issues. My email is

Nyerere! Nyerere! Nyerere! Hapa ulituumiza mzee wangu mengi mazuri ulitenda ila hapa maumivu umetuachia....fikiria mtu anasema 32 yrs old girl imagine mzee wangu na tuking'ang'ania kiswahili maofisini na kwenye embassy hawakitumii.
 
dah wadau inasikitisha sana halafu funny enough mwingine yeye anaaply for pre phd lakini they look all the same with even undergraduate
 
dah wadau inasikitisha sana halafu funny enough mwingine yeye anaaply for pre phd lakini they look all the same with even undergraduate

Tena undergraduate can do much better the him.
 
Usiwahukumu sana kwani nimegundua ni wanasayansi zaidi. Wako more down to earth
 
Mkuu ulikuwa una maanisha nini hapa? nafikiri unaona swala la hii lugha lilivyo sasa.

Hivi Nguli si umeelewa lakini, nilimaanisha "than", we tulia kunywa mbege huko kijijini kwenu, ukisikia kengele ya kanisa inalia tulia usirie kwanza mpaka iishe.
 
Ndugu Sipo katazame takwimu za ukuaji wa lugha ya Kiswahili duniani. Inakuwa kwa kasi ya ajabu. Wengine wanakikimbilia. Sisi tunakikimbia. Baada ya muda tutaenda kukiomba kwao. Ndio maana Shabaan Robert alisema huu mfumo wenu wa kikasumba utafanya Kiingereza kishinde Tanzania ila baada ya muda tutakirudia Kiswahili. Hakuna mtu aliyewalazimisha Watanzania tukiache Kiswahili. Ni ubwege wa Kitanzania tu! Ujinga mtupu!
 
Back
Top Bottom