SaaMbovu
JF-Expert Member
- Oct 8, 2013
- 6,027
- 5,344
Habari wana JF! Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa yote na wana JF kwa ujumla hususani uwanja huu wa JF Doctor. Nikienda kwenye mada ni kuwa mimi nina tatizo la kuumwa Malaria na Tyford sana. Na nikifanya matibabu napona kabisa hata nikifanya checkup tena sioni tatizo baada ya wiki tatu au nne. Lakini nikikaa miezi miwili au mitatu lazima nianze kujisikia homa na nikienda hospital kupima tena nakuta matatizo yaleyale. Tatizo hili limeanza toka mwaka 2009 mpaka sasa na imefikia hatua sasa mwili hauna nguvu. Kuhusu uzito ni kwamba nina kg 82 na nimedumu nazo zaidi ya mwaka sasa na urefu wangu ni mita 1.75 kwa hiyo Body Mass Index (BMI) yangu ni 26.77kg/m2 ambayo inasema nipo kwenye Marginally Overweight (MO). Naomba msaada wenu wana JF tatizo liko wapi na nifanye nini ili niweze kuishi kwa raha maana kiukweli sina raha hata kidogo kwakuwa dozi za tyford zimenichosha na mengineyo. Please Nisaidieni.