Tatizo na Nyumba Ndogo...

I just edited what I said, sikugusa ulicho sema wewe... Halafu mpolee yuko wapi? anasoma hata sunday? ukimuona mpe salam.
nimemwambia ahakikishe PCB anafunika pwenti 5, lazima awe mkali ili nimpeleke Havard
 
exactly
zipo nyumba ndogo mtu unaambiwa kabisa
wahi kurudi kwa mkeo.'sitaki matatizo mie' lol
Mazee inaonyesha una siri flani huko unatuficha, tumpe mwangaza ili nasisi tufanye.
 
Mwanamke kama hana wivu kwa mme wake, basi mpeni pole mana hapati raha kutoka kwa mme wake.

Wenzako wanapelekwa dunia ingine, wewe sijui unafikishwa pale katikati ya dunia na hio ingine, nadhani hujafikishwa bado kwenye dunia ile ingine.
 
Yawezekana wewe ni mmoja wa wale wanaoamini kuwa.......mume kuwa na nyumba ndogo sio kwamba hakupendi, and it is okey as far as he cares for you and the family as well.......provided that nyumba ndogo haikuletei kashkash!
 
nimemwambia ahakikishe PCB anafunika pwenti 5, lazima awe mkali ili nimpeleke Havard

Itapendeza sana mkuu, nawasalute watu wanaosoma science.......labda kwa vile mie nilikuwa kilaza!! LOL
 

Wewee.....ebu kuja hapa!!! Mbona kabla haujaoa ulikuwa haukamatii kiivo ilhali uwezo wa kuongeza vidate hata kumi ulikuwa nao?? Baada ya kuoa ndo unasogeza mpango wa kando.....sio issue!!! LOL
 
Nadhani umejikatia tamaa kuachana na mambo ya kuktesa wakati mumeo hataiacha. Vizuri kujipa raha mwenyewe kuliko kuteswa na mambo ya nyumba ndogo, maana mume akishapenda hawezi kuiacha nyumba ndogo kama haijamkorofisha.

Chuakachara hahah hapana siwezisema kuwa nimekata tamaa hapana. Nina shindwa kujielewa tu kwa nn sina uoga nao
 

Kama nilivyosema katika post yangu iliyopita, nakupa mfano: Shemeji yangu (mdogo wa mke wangu) mme wake alipata nyumba ndogo. Shemeji ilimuumiza sana roho na kukosa amani na kukata tamma ya maisha. Nikampa wazo kuwa chagua mawili: Jiondokee, uanze maisha yako AU dharau na uyaone ya kawaida, ila usimpe ngono. Akafuata ushauri wa pili. Mbona bwana aliumia sana kukosa ngono toka kwa mke wake. Kesi zikawa kesi lakini akashikiria msimamo kuwa hatampa ngono. Sasa amezoea maisha na hana wiivu tena. Anamuona mme kama kaka yake na maisha yanakwenda vizuri, anafanya biashara zake na anafanikiwa. Nyumba ndogo anatamani kuiacha lakini ameshaizalisha na ugomvi kila leo!!
 
MJ1 umepotea kweli leo ngoja nijisomee tu hapa uwe na jumapili njema.
 

Siku ukiletewa gonjwa la zinaa utaendelea kutokushtushwa na kutokupata shida?
 
mara nyingi mtu anaenda huko nyumba ndogo kwa tamaa tu................ sasa kama bado ana haja na mkewe hawezi kuweka mambo hadharani, lazima adanganye.... mimi anidanganye tu, maana akiniambia ukweli kwamba ana nyumba ndogo nitaumia sana, maana hadi kufikia kuniambia, najua mambo yameshakuwa magumu kwangu
 
Aisee, usikute wewe unaandika maneno yangu! nashangaa tu hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…