Tatizo namba moja la Yanga ni Clement Sanga

Tatizo namba moja la Yanga ni Clement Sanga

DREAMBOY

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Posts
2,117
Reaction score
1,369
Habari wanamichezo!

Tangu kujiuzulu kwa Manji kwenye timu ya Yanga, sauti ya mamlaka ya kiuongozi imepotea! Huo ndo ukweli hata ukibisha.

Tatizo la Mzee Sanga ni kupenda madaraka ambayo pia hajui atayapataje, yupo yupo tu kifupi hajielewi. Kajaribu kuwajaza watendaji wa upande wake lakini nao ni tatizo yaani mizigo.

Yanga chini ya Clement Sanga imekuwa Yanga ya malalamiko na kibaya zaidi tumeaminishwa kuwa timu haina pesa mpaka wengine tumechangia. Lakini timu ina udhamini kutoka
1. Vodacom
2. Maji ya Afya
3. Yanga TV kupitia Azam TV
4. Sportpesa.
5. Gate collection n.k.

Cha ajabu mishahara inacheleweshwa, wachezaji hawaambiwi sababu na kama kuna upungufu ni wa kiasi gani wanachama hatujui. Ni ngojera kila uchao.

Mzee huyu ameshindwa hata kuitisha mkutano wa wanachama ili nafasi hiyo izibwe, sasa katuwekea Katibu ambae anatamani kuwa Kocha, very selfish! Sasa amemleta msemaji ambae ameshindwa kuisemea brand ya timu yetu. Umaarufu wa timu unashuka, si bora Jerry Muro pamoja na mapungufu kadhaa ila alisaidia kuimarisha brand ya club yetu.
Ndugu Dismas Ten, hata huko alikotokea hakuwa jina lenye ushawishi, sijui ni ndugu wa Mzee Sanga?!

Nasikia eti Mzee wa saba anaitaka timu. Sawa lakini asifikirie Yanga ni kama Taifa Stars, watu watamfanyia vurugu kama Nchunga. Naskia umeitwa mkutano mwezi Mei, lengo ni kubadili Muundo wa uendeshaji. Nashauri sambamba na hilo uongozi chini ya Sanga utupishe tujaribu akili mpya. Hata huyo atakaenunua hisa namuonea huruma, atapata hasara isiyomithilika.

Tunataka akili mpya na siendi uwanjani tena mpaka haya majinamizi yapishe.
 
Mbona mnakuja kugombana mwishoni mwa msimu baada ya kuona mnakosa ubingwa!
Vumilieni wakati wa shida ndo wakati wa kuungana
 
Way forward ni kubadili mfumo wa uendeshaji.... Hizo nyingine ni blah blah. Mfumo wa unachama kushika timu ni pasua kichwa.
Pia Madrid inamfumo wa wanachama na Arsenal ina mfumo wa hisa. Tatizo la club zetu ni viongozi halafu mifumo ndo inafuatia
 
Kawaida ya uvumilivu una mwisho
 
Mkwasa.ni bahili mno sasa anuleta kwenye timu
Ubahili kwenye mambo yako binafsi,sio kwenye mambo ya watu wengi. Mfano unachelewesha mishahara wakati bajet yake ilkuwepo.
 
Back
Top Bottom