DOTTO MUNGO
Member
- Mar 11, 2012
- 15
- 1
Inasikitisha kuona kuwa tunaanza semista ya pili wiki ya pili sasa (udom) bila kuwa na chochote katika akaunti zetu kwa wale tunaoitegemea serikali kupitia bodi ya mikopo ya elimu ya juu (HESLB). Wanachuo wengi wanageuka kuwa ombaomba kwa ndugu, jamaa na marafiki huku idadi kubwa ikihaha kupata walau mikopo kutoka sehemu yoyote ili kuendelea na masomo wakati wakisubiri bodi kuwajaza mikwanja kwenye akaunti zao. Tatizo ni nini jamani?