Tatizo ni Diamond mwenyewe, si Nyange wala mama Dangote

Tatizo ni Diamond mwenyewe, si Nyange wala mama Dangote

Diamond Platnumz ana umri wa miaka 31 kwa sasa. Ni mtu mzima. Ni baba wa watoto wanne wanaotambulika.

Wawili kutoka kwa cheupe wa Uganda, Zari The Boss Lady; supermodel Hamisa Mobetto anaye mmoja, kisha Tanasha Donna kutoka kwa Kenyatta.

Akiwa na umri huo, dunia inapokea ‘surprise’ kutoka kwa mama yake, Sanura Kassim ‘Mama Dangote’ kuwa yule mzee aliyefahamika kwa miaka na miaka ndiye baba mzazi wa Diamond, kumbe siye. Ni mwingine tena jina jipya.

Abdul Juma wa Kariakoo, ndiye baba mzazi aliyefahamika wa Diamond. Naye Diamond akajitambulisha kwa sauti na nyaraka mbalimbali kuwa ni Nassibu Abdul Juma.

Ulipoingia mwaka 2021, Mama Dangote akasema “taarifa ya awali haikuwa sahihi”. Watu wakabaki midomo wazi; taarifa sahihi ni ipi? Jina “Salum Idd Nyange” likatajwa.

Kwa mujibu wa mama Dangote, huyo Salum wa Nyange ndiye damu ya Diamond. Kwamba Abdu wa Kariakoo alisingiziwa tu. Ni ya ulimwengu kwa walimwengu, Sheikh! Ingia ndani ya sanduku la ubongo wa Abdu.

Unaweza kupata tafsiri mbili; mosi, maumivu baada ya kuaibishwa. Siku zote alijitambulisha kuwa ni baba wa Diamond. Tena, Diamond si anajiita Simba? Abdul akajiita Big Lion. Kwani hujui kuwa Simba kwa Kiingereza ni lion? Abdu a.k.a Anko Dudu la Yuyu, akajitambulisha ndiye simba mkubwa!

Pili, kwa miaka mingi kumekuwa na mgogoro usio na majibu. Diamond haivi na baba yake. Wakati Mama Dangote akionekana kufaidi matunda ya mafanikio ya kijana wake, Abdu anateseka kwenye lindi la umaskini.

Shida nini? Mengi yamekuwa yakisemwa. Ooh, Abdu alimtelekeza Diamond akiwa mtoto, eti ndio alikuwa anapokea malipo yake. Abdu sasa anawaza: “Kumbe haya yote ni kwa sababu sio mtoto wangu!” Abdu naye mara kwa mara amekuwa akitoa utetezi, kwamba hakumtekeleza mwanaye, isipokuwa aligombana na mama Dangote kipindi Diamond akiwa kidato cha kwanza.

Kisha, mama Dangote akabaki na mwanaye.


Kuyaongea ya Diamond na Abdu ni kusababisha msongamano kwenye ubongo.

Yameshazungumzwa mengi. Tupo kona nyingine. Ni baada ya mama Dangote kusema Diamond si wa Abdu bali ni damu ya Salum wa Nyange.

Kwa kauli hiyo ya mama Dangote, yupo mwanafunzi wa darasa la sita anajiuliza leo; je, Diamond alishaambiwa kitambo kuwa Abdu sio baba yake mzazi ndio maana huwa hamjali? Mama Dangote kasema mchambuzi wa soka Wasafi FM, Ricardo Momo, ni baba mmoja na Diamond.

Inafahamika kuwa kwa miaka michache sasa, Ricardo yupo karibu sana na Diamond. Yupo mwanafunzi aliyefaulu mtihani wa darasa la nne hivi karibuni hataki kabisa kuamini somo kwamba Diamond na Ricardo walianza kuwa marafiki halafu ndipo ikagundulika ni mtu wa ndugu yake.

Huyu mwanafunzi aliyeingia darasa la tano Januari hii, ananishawishi kuamini kuwa hakuna bahati mbaya katika suala la Diamond, Ricardo na Mama Dangote.

Kosa la nani? Wengi wanamlaumu Mama Dangote. Kwamba amezingua ‘big time’ kusema Diamond ni damu ya Salum Nyange. Mimi simlaumu maana sidhani kama anastahili kulaumiwa leo. Kwani Diamond alizaliwa lini?

Mimba yake iliingia tumboni siku gani? Usisahau msemo kuwa ajuaye baba halisi wa mtoto ni mama. Rejea miaka 31 nyuma, ifikie Oktoba 2, 1989. Hiyo ndio siku ambayo Diamond alizaliwa. Anzia hiyo ‘birthday’ ya Diamond, halafu hesabu miezi tisa nyuma. Ni hapo utaweza kubaini siku kosa la mama Dangote lilipofanyika.

Alipogonganisha magari. Akanasa ujauzito. Ikawa siri. Abdu akaambiwa ni mzigo wake, naye akaupokea.

Kimahesabu, kosa la mama Dangote ni la miaka 32 iliyopita.

Kama ni lawama au adhabu, alipaswa kulaumiwa au kuadhibiwa kipindi hicho. Akaficha, ama alimficha Abdu au aliwazuga walimwengu. Jiulize, kwa nini ameamua kuyasema haya leo? Urahisi ni upi? Ukijiuliza maswali hayo vizuri ndipo utajua tatizo halisi lilipo. Ni Diamond Platnumz. Ameshakuwa mtu mzima, ni baba, maarufu, anayo heshima ambayo anapaswa kuilinda.

Hata hivyo, kwake mama yake imekuwa rahisi kumbadilishia baba. Mtoto yupo kimya. Unadhani kesi ya Diamond haifanani na wengi kwenye jamii? Wapo akina mama wanakufa na siri za baba halisi wa watoto wao.

Sababu ni hofu. Unaanzaje kumwambia mtoto anayejitambua kuwa “baba yako sio Abdu ni Salum wa Nyange”. Inawezekana vipi?

Kingine, akina mama wengi hufanya makosa kwa kunasa mimba nje ya ‘line’. Kwa kumheshimu mtoto wake, anamtambulisha mwanaye kwenye ‘line’, inabaki hivyo mpaka kifo.

Watoto wengi ambao wamelelewa na baba wasio wao, wamekufa, wanakufa na watakufa pasipo kujua ukweli kuwa baba zao wazazi sio waliowalea.

Mama anayemheshimu mwanaye, hawezi kumyumbisha, leo anamwambia baba yake ni Abdu, kesho Salum wa Nyange. Hapo unakuwa hujui kama kuna siku atamtaja Anko Shamte au yeyote yule atakayependa kumtunuku.

Ukifika hapo jiulize; Diamond amejiweka kwenye kundi gani? Hajitambui ndio maana mama yake anampelekapeleka? Na kwa nini anakubali kudhalilishwa ukubwani? Mpaka anafikisha umri wa 31 bado anatajiwa baba?

Diamond angekuwa amewahi kumuonesha mama yake kuwa hapendi ujinga, Mama Dangote asingethubutu kumleta Salum wa Nyange kwenye uso wa umma na kumtambulisha ndiye baba halali wa Diamond.

Angeogopa. Na angethubutu basi leo pangechimbika kati ya mtoto na mama. Rudia tena swali, kama Diamond alipokuwa na umri wa miaka 10 mpaka 15, hakuambiwa ukweli kuwa baba yake sio Abdu bali Salum wa Nyange, kwa nini aambiwe leo? Hutakosea ukisema Diamond alipokuwa na umri wa miaka 10, aliheshimiwa na mama yake kuliko sasa. Mama Dangote ameona Diamond wa sasa anaweza kuambiwa chochote na asifanye lolote kuliko yule wa miaka 16 iliyopita.



[emoji2398]Luqman Maloto
Sasa, una hakika gani kuwa Diamond alipenda kubaki kuwa mtoto wa Abdul? Pia unadhani shinikizo ni huyo Diamond au hali halisi? Huwezi kumhukumu kijana wa watu kwa makosa ya wazazi wao.
 
Wanaweza kwenye dna, na wakatoa Ela kwa mkono wa nyuma, kumkana baba, huyo hawamtaki toka alivyopata mafanikio mtoto, baba hasipate chochote, kwakuwa hakumtunza na aliwatelekeza akiwa form one.
Lakini ukweli watakuwa wameufahamu, hata wakimkana!

Hizi drama za mitandao ni publicity stunts tu hizi.. Sehemu ya kupata ukweli wanaifahamu ila wapo bize kula publicity, lakini ndo vizuri.

Sababu hata mie kama ningekuwa Meneja wa Msanii yeyote yule basi tungekuwa tunapiga Kazi sambamba na kufyatua ma-KICK mengi, tunawapa wananchi umbea, watu wapige UMBEA halafu tunapiga PESA.

Ukizidi kuongelewa ndivyo unavyozidi kuwa ON TOP OF THE GAME, na ukizidi kuwa Top ndivyo watu wanazidi kuwa na Hamu na wewe, strategically unakula Pesa. (Kazi kwa sana + Publicity Stunt kwa sana)

ENTERTAINMENT INDUSTRY haitaki mtu wa upole upole, uzubae zubae au kuwa very innocent, inataka AMSHA AMSHA! Makeke makeke!
 
Ni wakumbushe wanaume kusimama kwenye jukumu lenu, kwa kesi ya Daimond huyo mtoto ni wa mama maana kuzaliwa bila ndoa na ndo maana huyo anafanya huo uhuni bila wasiwasi, Ukitaka kuwa baba Basi jiandae kujenga ufalme wako utakao usimamamia kwa nguvu zako zote, oa mke awe wako na ukifanikiwa kupata watoto Walee kwenye ufalme wako wawe wako hata kama ukiachana na mama yao wewe ngangania kulinda kizazi chako na ikiwa uliwapotezea watoto Basi achana nao wawe watoto wa mama mpaka mwisho na wewe jenga ufalme wako utakao usimamia kwa kupambana kutoa mahitaji na kuujenga, Ila kwa kesi ya Daimond yeye ni mtoto wa mama tena mama ambaye hakuingia kwenye umalikia hayo ya mzee Abdul itakuwa ni mambo ya ukahaba tu kwa wote hata huyo Daimond hakujengwa kwenye ufalme Ila kajengwa na mama asiyekuwa malkia.
 
Diamond na umaarufu wake ni mpumbavu tu.
Mama yangu kwa anavyonifahamu hawezi kuthubutu kuniambia huo ujinga anajua kabisa undugu wangu nayeye utaisha siku hiyo hiyo
 
Lakini ukweli watakuwa wameufahamu, hata wakimkana!

Hizi drama za mitandao ni publicity stunts tu hizi.. Sehemu ya kupata ukweli wanaifahamu ila wapo bize kula publicity, lakini ndo vizuri.

Sababu hata mie kama ningekuwa Meneja wa Msanii yeyote yule basi tungekuwa tunapiga Kazi sambamba na kufyatua ma-KICK mengi, tunawapa wananchi umbea, watu wapige UMBEA halafu tunapiga PESA.

Ukizidi kuongelewa ndivyo unavyozidi kuwa ON TOP OF THE GAME, na ukizidi kuwa Top ndivyo watu wanazidi kuwa na Hamu na wewe, strategically unakula Pesa. (Kazi kwa sana + Publicity Stunt kwa sana)

ENTERTAINMENT INDUSTRY haitaki mtu wa upole upole, uzubae zubae au kuwa very innocent, inataka AMSHA AMSHA! Makeke makeke!
Nina shauku ya kujua ivi izi drama zinawezaje kumuongezea hela huyu jamaa
 
Nina shauku ya kujua ivi izi drama zinawezaje kumuongezea hela huyu jamaa
Na kama zinamwongezea hela kwa nini wasiwe wanammegea mgao wa kutosha huyo mzee Abdul kutoka kwenye zile pesa zilizovunwa kutokana na zile drama zilizomhusisha?
 
Nina shauku ya kujua ivi izi drama zinawezaje kumuongezea hela huyu jamaa
Msanii anapokuwa ni mchapakazi, anayejua kuji-brand, anayebadilika kimuziki kwenda na muda.

Halafu akiwa na Drama (publicity stunt) nyingi basi ndivyo anavyozidi kuongelewa sana na jamii, na ndivyo anavyozidi kuwa ON TOP OF THE GAME.

Na watu (jamii) ndivyo wanavyozidi kuwa na HAMU na SHAUKU ya kutaka kufahamu kila next moves zake (Nyimbo zake, Biashara zake, Mafanikio yake, Maisha yake etc.)

Hii ni nzuri kibiashara, maana DEMAND (uhitaji) ni kubwa tayari, na SUPPLY ipo. Hivyo msanii hapo yeye ni ku-Supply kazi zake tu (Nyimbo mpya, Shows, Merchandise, Endorsement deals, Biashara ya Matangazo etc.)

Hata Makampuni Makubwa mengi yanapenda kufanya biashara na wasanii wakubwa wenye USHAWISHI (influence) katika jamii.

Drama zikiambatana na Kazi Nzuri zinaweza kumsaidia msanii kuongeza USHAWISHI na MVUTO katika Jamii, na kutengeneza Mashabiki Wengi ambao wako radhi hata kukopa bando ili kuingia online na kufuatilia maisha na drama za msanii wao.

Hivyo msanii wa hadhi na calibre hiyo ni rahisi kwake kupata Endorsement Deals kutoka katika makampuni makubwa.

Kampuni zinataka msanii ambaye ni highly marketable and easily recognizable.

Kazi nzuri zinazoenda na wakati zikiambatana na drama basi zinaweza kumsaidia kumfanya msanii awe highly marketable and easily recognizable.

Msanii akifikia status (hadhi) hiyo basi ni rahisi kwake hata kuanzisha BIASHARA ZAKE NYINGINE NJE YA MUZIKI na Kuzitangaza kwa wepesi zaidi na kupata wateja wengi.

NB:
Lakini inabidi msanii awe na team ya watu sahihi wanaojua jinsi ya kutumia jina la msanii kuongeza mapato (pesa).

Sanaa haihitaji mtu mpole mpole, very innocent, sanaa inahitaji Amsha! Amsha!, mbwembwe na makeke mengi.. Wape watu kitu cha kukuongelea, kile kitu ambacho unaona hakiwezi kukushusha kimuziki bali kitakunyanyua.

Watu Wanataka UMBEA, wewe wape UMBEA!
Changa karata zako ili Umbea ukupe pesa kupitia BIASHARA za NYIMBO katika platforms mbalimbali, SHOWS, ENDORSEMENT DEALS, MATANGAZO, MERCHANDISE (bidhaa mbalimbali au biashara zozote zenye chapa ya msanii) etc...
 
Back
Top Bottom