G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Mashtaka yalisomwa January sita ila kesho yake DPP akaondoa kesi mahsksmani kimya kimya. Sijui alipewa maagizo?
====
Peter Maduki, ambaye alishtakiwa kwa makosa 280 yakiwamo ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo pamoja na utakatishaji fedha, ameteuliwa na Rais John Magufuli kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta).
Mashtaka yao yalisomwa Januari 6 Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu, lakini ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Umma (DPP) ililiondoa shauri hilo siku iliyofuata baada ya kuonyesha nia ya kutoendelea na kesi hiyo.
Siku hiyo, Maduki na mhasibu wa Wizara ya Afya, Luis Lymo(54) ambaye hakuwapo mahakamani, walisomewa mashtaka na mawakili wa Serikali, Zakaria Ndaskoi na Genes Tesha mbele ya hakimu mkazi mwandamizi, Augustina Mmbando.
Wakati kesi hiyo iliyokuwa imeahirishwa ikisubiri kutajwa, Maduki, ambaye ni mtendaji mkuu wa taasisi ya Christian Social Services Commission, juzi aliteuliwa na Rais Magufuli kuendelea kuwa mwenyekiti wa bodi hiyo ya Veta.
Baada ya taarifa ya uteuzi huo huku kukiwa na kesi hiyo, Mwananchi ilifuatilia kujua undani wake na kuelezwa kuwa ofisi ya DPP ilionyesha nia ya kutoendelea na kesi hiyo.
Wakili wa Serikali, Genes Tesha alilieleza Mwananchi kuwa kesi hiyo iliondolewa mahakamani siku moja baada ya kufunguliwa.
“Shtaka hilo kweli limeondolewa ingawa mimi niko likizo. Taarifa nilizozipata liliondolewa siku iliyofuata baada ya kufunguliwa. DPP alionyesha nia ya kutoendelea na kesi hiyo,” alisema Wakili Tesha.
Mwananchi ilipofuatilia mahakamani hapo ilielezwa na mmoja wa makarani kuwa shauri hilo lilishaondolewa.
“Nakumbuka hiyo kesi ilishaondolewa lakini sikumbuki ni lini jaribu kufuatilia kwa waendesha mashtaka wa serikali,” alisema karani huyo.
Katika kesi hiyo, washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka 150 ya kughushi, mashtaka 128 ya kuwasilisha nyaraka za uongo, moja la wizi na moja la kutakatisha fedha.
Wakili Ndaskoi alidai siku hiyo mahakamani kuwa washtakiwa walitenda makosa hayo kati ya mwaka 2017 na 2019 jijini Dar es Salaam.
Alidai washtakiwa hao kwa nafasi zao wakiwa na nia ovu walighushi hundi mbalimbali zenye thamani ya mamilioni ya fedha na kusaini kwa jina la Upendo Mwingira bila ridhaa yake huku wakijaribu kuonyesha kuwa Luis Lymo alikuwa akilipwa na taasisi ya Christian Social Services Commission fedha hizo kama kamisheni wakati si kweli. Pia walidaiwa kuwasilisha nyaraka za uongo benki ya Standard Chartered.
Pia, washtakiwa hao kwa nyakati tofauti wanadaiwa kuandaa taarifa ya uongo ya benki wakionyesha akaunti iliyopo tawi la NIC Life House la Standard Charterd NIC Life House kuwa ilikuwa na zaidi ya Sh1.7 bilioni.
Pia walidaiwa kuwa kati ya Machi 30/2017 na Oktoba 2018 waliiba zaidi ya Sh1 bilioni mali ya taasisi ya Christian Social Services Commission.
Kwa upande wa shtaka la utakatishaji fedha, walidaiwa kutakatisha zaidi ya Sh1 bilioni wakati wakijua fedha hizo zilitokana na kosa la kughushi.