Tatizo ni mfumo wa mawasiliano au? Aliyeshtakiwa makosa 280 ateuliwa kuwa M/kiti Bodi ya VETA

Anglia kwanza jina. Hawa ndio walio mpatia kura za kishindo..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenzako kabebwa na kanda anayotoka, huwezi kuta mtuhumiwa toka kanda pendwa getegete
 
Je siyo mtoto wa dada ?
 
Baba wa taifa mwalimu Nyerere alisema mtu mwenye tuhuma " hafai" kuwa Kiongozi!

Lakini kama kesi iliondolewa na aliyeileta, then Mwenyekiti mpya wa Veta hana makosa!

nyerere was wrong, yeye hakujua kwamba binadamu wameumbwa kusema ? tuhuma hata yeye alikua nazo na alikaa madarakani muda wote huo
maneno ya yule mzee sio ya kuyaamini sana, naye alikua mtu kama wengine t


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo jamaa anipeleke kwa mganga wake. Hakika ni kiboko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna sehemu nyingi za hili jambo.
Kwanza, uteuzi ni haki ya kikatiba kwa mhusika kutokana na katiba.

Pili, ilisemwa wakati wa maoni ya katiba, teuzi ziwe na ''vetting' na kwamba Rais apunguziwe madaraka ili kumuondoa katika sintofahamu kama hii.

Tatu, teuzi huanzia kwa mapendekezo kama si Waziri basi ni tume husika.
Je, hawakuliona hili?

Nne, kitendo cha kuwa na mashtaka 280 hata kama yangepanguliwa alau moja lingebaki.

Mwendesha mashtaka kufuta makosa hayo bila maelezo halafu uteuzi wa mtu yule yule ukafuatia inatia shaka kwa vigezo vyote.
 
Kwanza hiyo idadi ya mashitaka tu inaonesha hawa washitaki wenyewe hawakuwa serious.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…