Tatizo nini mpaka baadhi ya binadamu kuwa homoni za kike au kiume?

Tatizo nini mpaka baadhi ya binadamu kuwa homoni za kike au kiume?

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
2,971
Reaction score
9,437
Maandiko yanasema Mungu ndio muumba wa kila kitu, alimuumba mwanamume na baadae akaona siyo vyema aishi peke yake akamletea msaidizi mwanamke.

Kuna video nimeiina mitandaoni inasikitisha sana vijana wadogo wakiume sasa ni mashoga, kuna mmoja wao wakati anahojiwa akadai amezaliwa akiwa na homoni za kike.

Mimi kama mzazi ambaye nina kijana wa kiume hii inanifikirisha sana, kama Mungu ndiye Muumba wa binadamu anaweza vipi kumuumba bianadamu wa kiume mwenye homoni za kike?

Au kuna makosa sisi kama wazazi huwa tunayafanya kipindi cha ujauzito? Kama kuna vitu vinavyochangia mtoto kuzaliwa na homoni tofauti ni vyema jamii zikaelimishwa ili kuepuka haya matatizo maana yamekuwa mengi sana.
 
Hili suala la ushoga ni tatizo sana, kuna watu humu wanaamini ushoga unafundishwa kwamba fulan akiwa shoga akaendekezwa basi atamfundisha mwingine naye awe shoga.
 
Hormonal imbalance sio sababu kuu ya ushoga wanaokua mashoga ni maamuzi yao binafsi. Alafu unajua hormone za kiume zikizidi mwilini ili ku regulate hormones, mwili hubadili hormone hizo za kiume, Testosterone hormone kua hormone za kike, estrogen hii utokea hasa kwa wale wanaotumia sindano za Testosterone kutengeneza miili ya ki baunsa. Si ajabu unakuta pande la mtu lakini shonki au mashonki wengi hasa mambele uko wanamiili ya kibabe.
 
Hormone in-balance ipo... Ila matendo yake ni ya kusikitisha sana...
 
Inawezekana ikawa kweli kama watu wanavyozaliwa na ugumba au ulemavu uzazi una mambo mengi sana mtu anazaliwa moyo uko nje itakua kuzaliwa na homoni za kike.
Kwahiyo wanawake ndo wanafanywa kinyume na maumbile sio???

Kwahiyo wanawake wanaoenda kwa mpalange hao wamezaliwa wakiwa na homoni gani mkuu??
 
Hili janga lipo...
Shuhuda hapa mtaani kwetu kuna mtoto wakiume kabisa lakini hawezi kukaa na wanaume wenzake na kutwa kukaa na wanawake na kushinda nao.

Na hivi naskia miamba washaanza kumtanua dah..

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Hata kama mtu anazaliwa hivyo sio justification ya kufanya vitendo hivyo.

Kwa sababu mbona watu huzaliwa na abnormalities lakini huangaika mahospitali kitafuta tiba ili kuwa sawa, so why kwa ushoga kuwe na exception?
 
Back
Top Bottom