Tatizo si Kikwete na uelewa wake bali chuo kikuu alichosoma!

Papa D

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
753
Reaction score
182
Ukweli ni kwamba wahitimu wengi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam ni vilaza/wababaishaji [Si kikwete tu!]. Hii inatokana na jinsi wanavyofundishwa [wanakaririshwa na si kueleweshwa] watu wa aina hiyo huishia kuwa wenye nadharia nyingi kuliko utendaji. Mwisho wa safari huwa walalamishi wazuri sana. Chanzo kikuu cha kutoa vilaza ni kwamba Walimu/professors wa mlimani wamejaa wivu na husda!!!

Mwanafunzi aliyehitimu Mzumbe au DIT ni bora kuliko mhitimu wa Mlimani!! POLENI SANA WAHITIMU WA MLIMANI!!
 
Very interesting observation sir!!.... am off for now...!!
 
Mkuu do not generalize the affairs. Never draw a general conclusion from particular instances. Always draw a particular conclusion from general affairs. Siyo wote ni vilaza ingawa wapo vilaza!
 
Mkuu do not generalize the affairs. Never draw a general conclusion from particular instances. Always draw a particular conclusion from general affairs. Siyo wote ni vilaza ingawa wapo vilaza!

Ndugu;
Ningesema wote hapo ndo ningekuwa nime-generalize. lakini nimesema wengi [yaani majority]. therefore I still stand for my view!!
 
Kauli yako ina mapungufu ya aina mbili; kwanza ina mtizamo mgando. Ubora wa wahitimu katika miaka zaidi ya arobaini ya uhai wa chuo hicho, umekuwa ukihitirafiana siyo tu kwa fani moja na fani nyingine, lakini pia kwa mwaka hadi mwaka. Pili, kimsingi inalinganisha vitu viwili vilivyo tofauti. Katika hali halisi, wahitimu wa vyuo vya DIT na Mzumbe tangu mwanzo ilikusudiwa wawe watendaji (technitians), wakati wale wa mlimani walitegemewa wawe waratibu (coordinators). Ni kutokana na sababu hiyo, ndiyo maana baada ya kuhitimu DIT na Mzumbe walikuwa wanapewa diploma na mlimani digree. Tofauti kati ya diploma na digree, ni kwamba mtu wa diploma anazama zaidi katika eneo dogo, wakati mtu wa digree anafundishwa kwa lengo la kuwa na uelewa kwa maeneo mengi, ili aweze kuratibu kazi za wengine. Watu wengi huwa wanapotosha ukweli kwamba mtu anaweza akawa mwana taaluma tu kwa kujifunza darasani. Hii si kweli, ndiyo maana si sahihi hata kidogo kumwita JK mchumi au Pinda mwanasheria, kwasababu waheshimiwa hawa tangu wahitimu wamekuwa wakifanya mambo tofauti na fani zao.
 
Kaka you are WRONG, huwezi fananisha wanafunzi wa UDSM na Mzumbe...
 
Ni kweli kabisa watu waliosoma mlimani ni vilaza wa kutupwa na ndo viongozi wetu wengi sana wamepita hapo na angalia nchi walipoifikisha.
 
Mwanafunzi aliyehitimu Mzumbe au DIT ni bora kuliko mhitimu wa Mlimani!! POLENI SANA WAHITIMU WA MLIMANI!!

Baada ya kuandika utumbo unajisikiaje? imekupa faraja sasa kwa kufeli form six au form four? bado haujaamka kutoka katika mshtuko wa kufeli kijana, unaweza rudia mitihani kama unataka ili upate qualifications za kuingia the hill au Chuo kikuu.
 
Papa D yu may be right !!

..but lets see how they put it ...thread is still growing!
 
Hata mimi nimegundua wale wa magogoni college ni wazuri sana kwa 'TYPING' kuliko wa UDSM.
 
Kama ni chuo cha vilaza mbona huwa kinachukua cream yote, hafu mtu akikosa mlimani ndo anafikiria kwenda vyuo vingine, kwa nini?
 
tunapoelekea na hii thread lazima ngumi zitalia humu .... lol
 
Baada ya kuandika utumbo unajisikiaje? imekupa faraja sasa kwa kufeli form six au form four? bado haujaamka kutoka katika mshtuko wa kufeli kijana, unaweza rudia mitihani kama unataka ili upate qualifications za kuingia the hill au Chuo kikuu.

mkuu dizaini wewe muimba taarabu eeh?

mbona signature yako imekaa kimipasho-mipasho tu?

by the way, UDSM kinachukua siagi (cream). ukisikia mtu analalama ama anasagia UDSM ujue ama aliliwa kichwa ama alifeli form 6.

(lakini kweli UDSM kuna vilaza. mfano Bansen Burnner)
 
.....viva muheshimiwa!!!
 
Jamani jamani jamani hii mada tuwachie TCU ndio wenye dhamana ya elimu ya juu na mara zote kila muwamba ngoma kamba huvutia kwake,SAUT watsema wao ndo bora,na SUA watasema wao ndo bora ila ukweli ni kwamba usomi na utendaji ni vitu viwili tofauti.
 
:A S thumbs_down:"If there are no stupid questions, then what kind of questions do stupid people ask?
Do they get smart just in time to ask questions?"
-Scott Adams
:A S thumbs_down:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…