SoC01 Tatizo siyo vijana kujiajri

SoC01 Tatizo siyo vijana kujiajri

Stories of Change - 2021 Competition

Geneous99

Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
16
Reaction score
24
UTANGULIZI
Vijana wengi zaidi ya laki moja toka mwaka 2015 wamemaliza vyuo vikuu na vyuo vya Kati ngazi ya shahada, stashahada na astashahada katika fani tofauti tofauti ikiwemo ualimu, ( wa sayansi na Sanaa), utawala wa umma na sayansi ya siasa, utalii, geografia na mazingira, udaktari, mawasiliano, teknolojia, habari pamoja na mawasiliano.

Kwa bahati mbaya wengi wao hawajabahatika kuajiriwa mpaka sasa. Serikali imekuwa ikitumia kigezo cha watu kujiajiri wenyewe ilihali fani walizozisomea haziruhusu kujiajiri pengine kwa mazingira ya Tanzania, mfano, ualimu.

MAONI YA WATU
Katika hilo suala, watu wengi wamekuwa wakitoa maoni tofauti tofauti.

Hoja ya kwanza
Je, vijana wanaweza kujiajiri?. Wengine wamekuwa wakidai kuwa vijana wanaweza kuachana na fani walizosomea na kuanzisha biashara ndogondogo Kama vile; umachinga, bodaboda, mamanti'liye, kilimo, ususi, cherehani, sanaa na michezo. Lakini yote kwa yote, imekuwa ni changamoto kubwa Sana kwao kwani wengi wao hawana mitaji, thamani wala kipande cha ardhi ambacho wangeweza kukitumia kujiajiri.

Hoja ya pili
Je, hela ya kujikimu (boom) inatosha na kuitunza Kama mtaji?.Wengine wakadai kuwa wanachuo wengi wanapewa mikopo na fedha ya kujikimu (boom), hiyo wanaweza kuitumia kwa kupangilia bajeti zao na kuweka angalau kiasi kidogo cha kuanzia maisha pindi wanapomaliza masomo. Katika hili ni sahihi, lakini sio wote wanaoweza kufanya hivo, kwa sababu maisha yanatofautiana na watu wanatoka katika familia tofauti tofauti, na wengi wao wanatoka katika familia duni zaidi. Fikiria, mtu huyo huyo anahitaji hyo 505000 kwa ajili ya chakula, mavazi, matumizi mengine kama bando, madaftari, karamu, stationary, nauli. Na wengine huenda mbali zaidi, kwani wao ndo tegemezi kwa familia zao, wadogo zao wanawategemea na pengine hela hiyo aipatayo ndiyo analipa fedha ya pango kwa hostel na wale waishio mitaani, hivyo unakuwa ngumu kutunza pesa ambayo itatosha kujiajiri.

Hoja ya tatu
Hosteli hudumaza fikra na utayari wa kuanza maisha. Fikiria, mwanachuo anaishi hostel, akimaliza atahitaji kitanda na godoro, pengine vyombo, jiko la gesi au mkaa, chakula cha kuanzia, kosi ya nyumba na hela ya mtaji ibaki, vipi inawezekana kwa mtu aliyetunza Tsh laki tatu kufanya yote hayo katika ardhi isiyo ya nyumbani?. Vipi ataweza kujiajiajiri? Hyo akili ya kujiajiri ataitoa wap ikiwa maisha yake yote ya chuo alikuwa hosteli na hakuwa na kitu chochote na wala hakuna somo la ujasiliamali zaidi ya kukalili mafilosofia na mawazo ya wanazuoni kuhusiana na fani anayoisomea. Hii ni tofauti na wale ambao wao tayari wanaishi mtaani , kwani angalau watakuwa na kitanda, godoro, vyombo pamoja Kodi ya pango wamekwishalipa.

Hoja ya nne
Kila mtu anaweza kujiajiri. Hapa wengi wanaamini hivo, tatizo kubwa lilokuja vichwani mwao ni mtaji na mazingira wezeshi ya vijana kujiajiri kutoka serikalini. Je serikali imefanya nini kuwawezesha vijana kujiajiri?, Kuna hoja kuwa kila halimashauri inatoa asilimia kumi ya mapato yake kusaidia vijana kwa kuwapa mikopo katika makundi, je pesa hiyo inatosha?, Vijana wote ikiwemo waliomaliza vyuo wanaweza Wana nafasi ya kupata fedha hizo?, Mi kwa muda gani wanatakiwa kurudisha fedha hizo?, Vipi kuhusu Kodi zisizo za lazima haziwabani vijani kushindwa kujiajiri?, Serikali inafikilia nini kuwapa mitaji vijana na wahitimu wa vyuo vikuu?

MAPENDEKEZO
1. Kwa vijana na wahitimu wa vyuo na vyuo vikuu

Mosi, ni vijana kutambua, serikali iliyopo madarakani imeshindwa kuwapa ajira pamoja na kuwatengenezea mazingira kwa wao wenyewe.

Kivipi?, Fikiria Serikali inasema hamna ajira serikalini, wakati huo tafiti zinaonesha kuwa kuna uhaba wa walimu, madaktari(watabibu), manesi(wauguzi), watendaji, maafisa mazingira na wahandisi, kuwataja kwa uchache. Bila ya sababu za msingi, kisingizio kikiwa ni kujiajiri.

Mbili, vijana sasa tukubali nyakati zimebadilika, na tuwashauri wadogo zetu kuhusu nyakati hizi, lakini tusiishie kukubaliana na nyakati, Bali tushirikiane pia katika kubadilisha mifumo, mfumo wa utawala, mahamaka, bunge, hivi vimekuwa vikitukandamiza sana. Mfumo wa utawala ikiwemo katiba mpya, time huru ya uchaguzi, bunge huru, mahakama huru, na mfumo mzuri wa elimu.

Tatu, tuendelee kujituma zaidi na kufanya shughuri ndogondogo zitakazotupa ugali wa kila siku, tusione aibu kuwa tumemaliza chuo, hatuwezi kufanya shughuli nyingine, tuzifanye kwa moyo mmoja na Imani kuwa zitaweza kututoa wakati mpaka pale mfumo utakapobadilika. Ukiweza kufanya biashara, fanya, ukiweza kushona nguo, shona, ukiweza kuuza uji, uza, na hata ukiweza kuokota makopo, okoto, ila tuaikubali mfumo ukawa dhalili kwetu.

2. Kwa Serikali
Moja. Serikali ifanye tafiti za kina na kujiridhisha kwamba, je ni kweli walimu wanatosha na hawahitajiki tena? Je ni kweli wauguzi na watabibu na wengine wa fani tofauti tofauti wanatosha na hawahitajiki tena?. Kama hawatoshi kwa nini tusiajiri ili watoshe na vijana wengi wenye sifa wapo mtaani, je hatuna hela za kutosha kuajiri? Kwanini? rasirimali hazitoshi( na Imani zinatosha, kwani tuna watu wa wengi, bahari, mito, maziwa, bandari, wanyamapori, madini ya aina tofautitofauti, misitu, ardhi, hewa mvunde(gas) na rasilimali nyingine nyingi), je Serikali imefanya nini kuzichakata hizo rasilimali na kuzibadilisha kuwa hazina ili ziweze kusaidia katika kuajiri? Majibu yote wanayo wao

Mbili. Je, Serikali imeweza kujenga mazingira wezeshi kwa vijana kujiajiri?. Katika mapendekezo ya wengi, vijana wamekuwa wamekosa mitaji ya kujiajiri, kwa nini serikali isiangalie uwezekano wa kuwapa mitaji vijana walioko mitaani mmoja mmoja au kwa makundi iwe kwa mikopo isiyo na riba na ya mda mrefu ili waweze kufanya kazi zao kwa uburu, kwa sababu srikali itakuwa inapata Kodi kutoka kwao mpaka pale watakapolejesha, kwa Serikali isiwape mitaji wanafunzi wote wanaomaliza vyuo vikuu na ambao wanaona hawatakuwa katika mpango wa kuwaajiri ili waweze kujiajiri? Mfano ikiwapa kila mmoja mil2 mpaka 5 je haitakuwa suruhisho kwa wale wanaodai hawawezi kujiajiri kwa kukosa mitaji?

Tatu, serikali ikitaka watu wajiajiri, waanze kwanza kutengezeza mfumo pamoja na kubadilisha mfumo mzima wa elimu, ili vijana wasome wakijua hamna ajira na ni mfumo wa elimu ya kujiajiri ili waweze kusoma fani ambazo hazitawabana kujiajiri tofauti na kukimbilia ualimi, uuguzi, utabibu, geografia, mazingira au utawala na utendaji

Nne, Serikali ishirikiane na wadau kupata katiba mpya kwa maslahi mapana ya taifa na kujenga mihimili iliyo huru na haki na kuepuka upendeleo.
 
Upvote 4
Back
Top Bottom