Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Magharibi kichama, Mhe. Tauhida Cassian Gallos ametoa wito kwa viongozi wenzake kuutumia mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kusaidia wanachama wao hasa wanapopata matatizo.
Mbunge Tauhida Gallos Ameyasema hayo tarehe 24 Machi, 2024 katika Wilaya ya Magharibi A wakati alipofanya ziara ya kumfariji Mjane mwenye Watoto 5 ambaye mume wake alifariki wakati akiwa njiani kurudi kumpeleka mke wake hospitali.
Mbunge Tauhida Gallos Amesema mwezi huu ni mzuri kwa kusaidia watu mbalimbali ikiwemo Wajane, Watoto yatima, Wazee, wagonjwa na Wenye matatizo mbalimbali.
Aidha, Tauhida Gallos amesema kuwa kufanya hivyo ni kuigusa jamii moja kwa moja jamii ambapo pia ni kuunga mkono juhudi za Viongozi wakuu wa Serikali.
Tauhida Gallos Amebainisha kuwa kwa takribani mwezi nzima wa Ramadhani Viongozi hao wamejielekeza kwa Mwenyezi Mungu kwa kuftari na Watu wa makundi maalum ikiwemo Wajane, Watu wenye ulemavu na Wagonjwa.
Mbali na hayo, Mhe. Tauhida Gallos amesema mama huyo, anahitaji asaidiwe kwa hali na mali hivyo ameahidi kutomuacha mkono na kuwa nae bega kwa bega.
Mbunge Tauhida Gallos Ameyasema hayo tarehe 24 Machi, 2024 katika Wilaya ya Magharibi A wakati alipofanya ziara ya kumfariji Mjane mwenye Watoto 5 ambaye mume wake alifariki wakati akiwa njiani kurudi kumpeleka mke wake hospitali.
Aidha, Tauhida Gallos amesema kuwa kufanya hivyo ni kuigusa jamii moja kwa moja jamii ambapo pia ni kuunga mkono juhudi za Viongozi wakuu wa Serikali.
Mbali na hayo, Mhe. Tauhida Gallos amesema mama huyo, anahitaji asaidiwe kwa hali na mali hivyo ameahidi kutomuacha mkono na kuwa nae bega kwa bega.
Attachments
-
WhatsApp Image 2025-03-24 at 11.16.31.jpeg87.1 KB · Views: 35 -
WhatsApp Image 2025-03-24 at 11.16.30 (1).jpeg85.4 KB · Views: 38 -
WhatsApp Image 2025-03-24 at 11.16.30.jpeg81.2 KB · Views: 31 -
WhatsApp Image 2025-03-24 at 11.16.29.jpeg96.2 KB · Views: 30 -
WhatsApp Image 2025-03-24 at 11.16.27 (1).jpeg84.1 KB · Views: 36