Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Magharibi, Mhe. Tauhida Gallos Nyimbo akiwa Wilaya ya Magharibi A tarehe 06 Machi, 2025 amewataka Wazazi na Walezi kuwashajihisha Vijana wao kutumia vizuri mitandao ya kijamii ili kujipatia kipato.
Mbunge Tauhida Gallos Ameyasema hayo mara baada ya kukabidhi Mchanga na Saruji kwa Viongozi wa Skuli ya Tucheze Tujifunze (TUTU) Mtofaani Wilaya ya Magharibi A alipofanya ziara na kuzungumza na wazazi na walezi.
Mbunge Tauhida Gallos Amesema kuwa, kuna Vijana wengi ambao wanatengeneza Pesa siku hadi siku, kupitia Mitandao ya kijamii na hivyo amewataka vijana wa Mkoa wa Magharibi kuchangamkia fursa hiyo muhimu.
Aidha, Mbunge Tauhida Gallos amesikitishwa na baadhi ya Vijana wanaotumia Mitandao ya kijamii kwa kufanya mambo maovu ikiwemo Wizi, Udhalilishaji na kuangalia picha chafu.
Hata hivyo, Mbunge Tauhida Gallos amewataka wazazi na walezi kushirikiana katika malezi ya Watoto wao ili waweze kuwa Vijana wema watakaoweza kusonga mbele kimaendeleo.
"Watoto wetu wanaangamia, tushikamane jamani katika malezi, Mtoto halelewi na Mzazi mmoja" - Mbunge Tauhida Gallos
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Mfenesini, Majuto Juma Haji amewataka wananchi kuwaunga mkono Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ili waendelee kuwaletea maendeleo.
"Viongozi wetu tunawaona jinsi wanavyojikita katika kuwajengea Wananchi Mabarabara, Mahospitali, Masoko na mikopo mbalimbali, lazima tuwaunge mkono ili kuwapa moyo" - Bi Majuto.
Naye, Mlezi wa Skuli ya Tutu Mtofaani ambaye pia ni Sheha wa Shehia ya Michikichini Kijakazi Ferusi Khamis amesema kuwa wamejenga Skuli mbili kwa nguvu za wananchi na kumpongeza Mbunge Tauhida Gallos kwa kutoa msaada huo.
Hata hivyo, amesema lengo la kujenga Skuli hiyo ni kuwaondoshea usumbufu kwa Watoto wao kwa kufuata masomo masafa ya mbali na kuwakinga na vitendo viovu.