Blender
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 4,870
- 8,035
Maendeleo gan we mwiziTunaendelea kuhifadhi pembe kwenye ghala zikiendelea kupigwa vumbi badala ya kuuza tukapata pesa za kusaidia miradi ya wananchi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Maendeleo gan we mwiziTunaendelea kuhifadhi pembe kwenye ghala zikiendelea kupigwa vumbi badala ya kuuza tukapata pesa za kusaidia miradi ya wananchi.
Shida iko wapiHaya sasa ni maajabu, hapo ni kuhalalisha biashara ya meno ya tembo
Biashara ya meno ya tembo hakuna shida?Shida iko wapi
Ukimtazama anaonekana kabisa ana agenda yake ya siri, sababu anazozitoa hazina mashiko kabisa, kwanini asizungumzie kupanua mapori ya hifadhi mara wanyamapori wanaharibu mali na mazao mara tuongeze mapato ya nchi, lipi la kwanza na lipi la mwishoImeelezwa kuwa ongezeko la Wanyamapori Nchini limekuwa chachu ya kuwa na ongezeko la ushawishi wa ujangiri, uvamizi wa maeneo ya Wananchi ambapo humesababisha uhasama kati ya mamlaka za Serikali na Wananchi.
![]()
Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wananyamapori Tanzania (TAWA), Mabula Misungwi Nyanda ameyasema hayo Mkoani Dar Es Salaam 10 Septemba 2022 alipokuwa aliongea na Wanahabari kwenye hifadhi ya pori la akiba la Pande (Pande game reserve)
Una matatizo ya akiliNilishatoa huu ushauri hawa wanyama wavunwe kupunguza athari
Imeelezwa kuwa ongezeko la Wanyamapori Nchini limekuwa chachu ya kuwa na ongezeko la ushawishi wa ujangiri, uvamizi wa maeneo ya Wananchi ambapo humesababisha uhasama kati ya mamlaka za Serikali na Wananchi.
View attachment 2354405
Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wananyamapori Tanzania (TAWA), Mabula Misungwi Nyanda ameyasema hayo Mkoani Dar Es Salaam 10 Septemba 2022 alipokuwa aliongea na Wanahabari kwenye hifadhi ya pori la akiba la Pande (Pande game reserve)
Amesema ongezeko hilo la Wanyama hasa Tembo limekuwa na madhara na inapotokea kunatakiwa kufanyika uwindaji kumekuwa na vikwazo kutoka kwa watetezi wa Haki za Wanyama ambao hawataki Tembo Wavunwe kwa Manufaa ya Nchi.
Kamishna Nyanda anasema: “Idadi ya Wanyama inaongezeka lakini ardhi haiongezeki, Tanzania tunatakiwa kuonesha tunapata faida kutokana na Wanyama tulionao.
“Hata kisayansi inaeleza kuwa kuna hatua inafika inabidi Wanyama wapunguzwe, wasipopunguzwa matokeo yake ndio kama hivyo tunasikia wanavamia makazi ya watu na kufanya uharibifu na wakati mwingine kuua watu.
“Ndio maana tuna kanuni kuwa lazima ifike hatua Wanyama lazima wawindwe na wauliwe kwa faida ya Nchi.
“Mfano Tembo kwa sasa wamekuwa wakihusika katika matukio mengi ya mauaji na uharibifu wa mali, kama hakutakuwa na kitu cha ziada kuokoa hali hii hali inaweza kuzidi kuwa mbaya.
“Tunashauri Serikali iruhusu uwindaji halali wa Tembo kwa maelekezo maalum, ambayo ni kuwinda Tembo wazee na madume hadi itakapobaki idadi fulani ambayo inakuwa haina madhara kwa kiasi kikubwa.
“Inapotokea uwindaji wa aina hiyo kisha pembe za ndovu zikauzwa, Nchi inapata faida, hiyo ni nzuri badala ya kusikiliza NGO ambazo nyingine kwao hazina hata mbuga lakini zinakuwa Hodari katika kusimamia Wanyama kutopunguzwa wakati madhara tunapata sisi. Kama nchi tunao uwezo wa kuangalia Sheria na kanuni zetu, hizi pembe za ndovu zikiuzwa zinaweza nufaisha nchi kwani ni Maliasili yetu.
“Hata kama mamlaka haitatoa ruhusa hiyo, kumbuka kuwa kadiri Tembo wanavyosababisha madhara kwa wananchi ndivyo ambavyo nao (Tembo) wanakuwa hatarini kuuawa kinyume cha sheria na haohao Wananchi.” Pia inaongeza uhasama kati ya Serikali na Wananchi wake.
=====
MY TAKE
Six African Nations Agreed to Push for Restarting Ivory Trade
31 May 2022
With the elephant population growing out of control in parts of southern Africa, several countries in the region agreed at a conference to support Zimbabwe’s push for the legalization of the international ivory trade.
Last week’s conference, organized by Zimparks, Zimbabwe’s wildlife management authority, was attended by representatives of Botswana, Namibia, South Africa, Tanzania and Zambia.
![]()
Six African Nations Agreed to Push for Restarting Ivory Trade
With the elephant population growing out of control in parts of southern Africa, several countries in the region agreed at a conference to support Zimbabwe’s push for the legalization of the international ivory trade.www.occrp.org
Uajabu hapo upo wapi na kama watavunwa kwa mujibu wa sheria nini tatizo?Haya sasa ni maajabu, hapo ni kuhalalisha biashara ya meno ya tembo
Huyu aache uhuni hakuna tembo walioongezeka. Tembo walipungua sana zikaundwa kila kampeni kuwalinda, wakatumika kila aina ya wasanii na watu maarufu kupiga vita mauaji ya tembo. Aache ujinga huyu ana beep hapo.
Ila mama amezidi kuwa mpole, mtu Kama huyu anayezungumza hivi ilipaswa amuweke pembeni faster tu
Kwamba Tembo ana thamani kuliko Binadamu aliyepewa MAMLAKA ya kumuhifadhi chini ya uumbaji wa Mungu [emoji848][emoji16]Ukiua Tembo mmoja kwa kumgonga kwa bahati mbaya na gari, unailipa serikali TShs 35,000,000. Tembo akiua binadamu, familia ya binadamu inalipwa TShs 1,000,000.
AKILI, AKILI, AKILI mtu wangu!
Halafu sheria zimekaa kifala sana. Wanakuja tembo wanaharibu mazao yenye thamani kubwa. Hata kama thamani ya mazao ni million 5 au zaidi, serikali inakulipa si zaidi ya 300,000. Ovyo kabisa. Wananchi wengi wa kawaida walioathirika na Tembo, wamekuwa na chuki sana dhidi ya serikali. Naunga mkono tembo wavunwe na serikali pekee ili kuwapunguza wasizidi carrying capacity.Tembo wamekuwa wengi na wanauwa watu na kuharibu mazao ya wananchi ni vile tu vyombo vyetu vya habari vinaandika habari za mijini tu.
Wilaya ya Nachingwea na Ruangwa mkoani Lindi wananchi wanapoteza maisha kutokana na Tembo. Wananchi wamekuwa na Hasira mpaka walitaka kugomea sensa kutokana na ndugu zao kupoteza uhai na serikali haichukui hatua. Kijiji kuvamiwa na tembo 50 wala sio kitu cha ajabu huku kwetu. Na wakipita wanaharibu mpaka vyanzo vya maji vya wana kijiji.
Ndio hali ilivyo.Kwamba Tembo ana thamani kuliko Binadamu aliyepewa MAMLAKA ya kumuhifadhi chini ya uumbaji wa Mungu [emoji848][emoji16]
😸Mimi na meno ya tembo wapi na wapi? Au unawashwa?
Wamezidi wangapi?Yuko sahihi.
Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma tembo wanaharibu mazao ya wananchi na kuua watu mara kwa mara.
Tembo ni wengi mno huko Liwale, Tunduru na sehemu nyingine
Halafu sheria zimekaa kifala sana. Wanakuja tembo wanaharibu mazao yenye thamani kubwa. Hata kama thamani ya mazao ni million 5 au zaidi, serikali inakulipa si zaidi ya 300,000. Ovyo kabisa. Wananchi wengi wa kawaida walioathirika na Tembo, wamekuwa na chuki sana dhidi ya serikali. Naunga mkono tembo wavunwe na serikali pekee ili kuwapunguza wasizidi carrying capacity.