TAWA: Ongezeko la Tembo ni hatari kwa maisha na mali za watu, Mamlaka iruhusu Uvunaji wa Pembe kwa faida ya Nchi

Ngoja niwape Siri
Hao wanyama pori Wana wafukuza Kwa kuwasha mioto katika sehemu zao za maskani. Na njia mbalimbali wanazitumia ili kuwafukuza hao wanyama.
Na Wana nao wafukuza in Askari wa wanyama pori, ndio wanao jua mchezo huu wa kishezi

Tuna serikali ya kipumbavu sana
 
Nilishatoa huu ushauri hawa wanyama wavunwe kupunguza athari
 
Ukimtazama anaonekana kabisa ana agenda yake ya siri, sababu anazozitoa hazina mashiko kabisa, kwanini asizungumzie kupanua mapori ya hifadhi mara wanyamapori wanaharibu mali na mazao mara tuongeze mapato ya nchi, lipi la kwanza na lipi la mwisho
 
Haya maneno hayakupaswa kutoka kwa mtu kama huyu aliyekabidhwa wajibu mkubwa hivi wa kuwalinda wanyamapori. Ni hatari sana, ni vyema huyu apangiwe majukumu mengine na mamlaka zilizo juu yake.
 
Kwa nini asiseme population ya wanadamu imekuwa kubwa hadi inamwagikia katika maeneo ya wanyamapori na viumbe vingine vinakosa nafasi ya kutosha kuishi maisha yao??
 

Tembo wamekuwa wengi na wanauwa watu na kuharibu mazao ya wananchi ni vile tu vyombo vyetu vya habari vinaandika habari za mijini tu.
Wilaya ya Nachingwea na Ruangwa mkoani Lindi wananchi wanapoteza maisha kutokana na Tembo. Wananchi wamekuwa na Hasira mpaka walitaka kugomea sensa kutokana na ndugu zao kupoteza uhai na serikali haichukui hatua. Kijiji kuvamiwa na tembo 50 wala sio kitu cha ajabu huku kwetu. Na wakipita wanaharibu mpaka vyanzo vya maji vya wana kijiji.
 
Huyu alitakiwa kutumbuliwa mara moja.Sio kwa mawazo hayo yaliyo kijume kabisa na taasisi anauo simamia ya kulinda hao wanyama wasiwindwe na watu.
Mamlaka husika fanyieni kazi .
 
Ukiua Tembo mmoja kwa kumgonga kwa bahati mbaya na gari, unailipa serikali TShs 35,000,000. Tembo akiua binadamu, familia ya binadamu inalipwa TShs 1,000,000.
AKILI, AKILI, AKILI mtu wangu!
 
Ukiua Tembo mmoja kwa kumgonga kwa bahati mbaya na gari, unailipa serikali TShs 35,000,000. Tembo akiua binadamu, familia ya binadamu inalipwa TShs 1,000,000.
AKILI, AKILI, AKILI mtu wangu!
Kwamba Tembo ana thamani kuliko Binadamu aliyepewa MAMLAKA ya kumuhifadhi chini ya uumbaji wa Mungu [emoji848][emoji16]
 
Halafu sheria zimekaa kifala sana. Wanakuja tembo wanaharibu mazao yenye thamani kubwa. Hata kama thamani ya mazao ni million 5 au zaidi, serikali inakulipa si zaidi ya 300,000. Ovyo kabisa. Wananchi wengi wa kawaida walioathirika na Tembo, wamekuwa na chuki sana dhidi ya serikali. Naunga mkono tembo wavunwe na serikali pekee ili kuwapunguza wasizidi carrying capacity.
 
Kama ambavyo tukizidi wazungu hutupunguza Kwa kutuletea magonjwa ya mlipuko
 
Ondokeni kwenye maeneo yaliyo karibu na Tembo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…