TAWA:Wavamizi wa hifadhi Inyonga kukamatwa kama kumbikumbi

TAWA:Wavamizi wa hifadhi Inyonga kukamatwa kama kumbikumbi

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Kanda ya Magharibi, inatarajia kuanza operesheni ya kuwasaka na kuwaondoa watu wanaovamia maeneo ya hifadhi na kufanya shughuli za kibinadamu, zikiwemo kilimo, ufugaji na ukataji holela wa misitu.

Kamanda wa Hifadhi ya Wanyamapori Inyonga, SC John Msirikale, amesema baadhi ya wananchi wameanzisha makazi ndani ya hifadhi, hali iliyosababisha mamlaka hiyo kupanga operesheni itakayohusisha maeneo yote ya hifadhi hiyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Majid Hemed Mwanga, ameunga mkono hatua hiyo na kueleza kuwa operesheni ya kuwaondoa wavamizi itatekelezwa kwa nguvu kubwa, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea msimu wa mvua za masika.

Amesema katika kipindi hicho, baadhi ya wakulima wamekuwa wakitumia fursa ya mvua kuvamia maeneo ya hifadhi kwa ajili ya kilimo cha mpunga na mazao mengine ya biashara.

Chanzo : Tbc digital

 
Huyu nae aache kusema uongo.

Hao wananchi wanaenda hifadhini kulima na kufanya shughuli nyingine na mnawatoza laki mbili kwa kichwa kimoja kwa makubaliano yenu na wananchi.
Sasa hapo aseme tu kwamba kiwango kwa kila mwanachi kimepanda na wamegoma kutoa. sasa mseme kwamba kwa kuwa wananchi wamegoma nyie mmeamua kuwa kama mbwai na iwe mbwai.
 
Back
Top Bottom