KERO TAWA yafuta barua za ajira za askari wake 12 wa AJIRA MPYA. (Kozi Intake NO.02)

KERO TAWA yafuta barua za ajira za askari wake 12 wa AJIRA MPYA. (Kozi Intake NO.02)

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) Imezuia kukamilisha taratibu za ajira za Askari wake 12 waliomaliza kozi ya mafunzo ya jeshi la uhifadhi kwa muda wa miezi 6 (KOZI INTAKE NO.02).

Mamlaka hiyo imesema kuwa Imebaini askari hao katika taarifa zao imeonekana wamemaliza kidato cha nne wakiwa na umri wengi wao miaka 15. Ambayo TAWA imesema kuwa ni umri mdogo kwa kumaliza elimu hiyo.

Je ni sawa kijana ambae ulihusika nae katika usahili tangu awali kabisa ulimpima afya na kukagua vyeti vyake vyote ukajiridhisha na kumpeleka kozi. Kabla ya kwenda kozi vijana hao walikuja tena TAWA makao makuu kwa ajili ya uhakiki wa vyeti kwa mara nyingine na mliwapitisha wamezu waende kozi.

Baada ya kumaliza kozi ya mafunzo ya jeshi la uhifandhi kwa miezi 6. Mliwapa barua rasmi za kuajiriwa na barua za kupangiwa vituo vya kazi. Askari hao kabla hawajaripoti vituo vyao vya kazi mliwazuia na kuwaita makao makuu ya TAWA.

Mliwapa barua nyingine inayosema mmefuta barua yao ya ajira na barua ya kupangiwa kituo cha kazi na inayowataka kurudi utumishi sekretariet ya ajira.

JE Ni sawa TAWA kwa mnayofanya kuzuia ajira za hawa askari mliokaa nao na kuwapa mafunzo kwa miezi 6 leo hii mnawarudisha nyumbani waanzie wapi kumbukeni watu walikuwa na ajira zao za mkataba. Walivyoona wamepata kazi ya kudumu walivunja mikataba ile.

Pia TAWA mnajiwekea dosari katika taasisi yenu ina maana mmekagua vyeti mara mbili na hamkuona kasoro hiyo. Waacheni vijana hawa wa kimasikini warudi kazini
 
Kama hawajafika miaka 18 kisheria si hawawezi kuajiriwa, ama muktadha wa uzi wako ni nini
 
Kama hawajafika miaka 18 kisheria si hawawezi kuajiriwa, ama muktadha wa uzi wako ni

Kama hawajafika miaka 18 kisheria si hawawezi kuajiriwa, ama muktadha wa uzi wako ni nini
Wamekidhi vigezo vyote ndio maana sekretariat ya ajira imewaajiri. Huko makazini mkuu kuna watu wenye nyadhifa wanataka kujiona Miungu watu haswa maHR. Unafuta barua za ajira kwa askari et. Kisa umeona kamaliza kidato cha nne na umri mdogo wa miaka 15. Kweli!!!
 
Sheria ya kazi labor law act umepitia lakini hususani kwenye kigezo Cha umri na aina ya kazi?
 
Wamekidhi vigezo vyote ndio maana sekretariat ya ajira imewaajiri. Huko makazini mkuu kuna watu wenye nyadhifa wanataka kujiona Miungu watu haswa maHR. Unafuta barua za ajira kwa askari et. Kisa umeona kamaliza kidato cha nne na umri mdogo wa miaka 15. Kweli!!!
MA HR nimeandika kwa herufi kubwa, wanajionaga Miungu watu sana.

Mungu ni Fundi sana, Binadamu tugekuwa hatufii daah basiiiii!!

Kuna binadamu wageteseka sana.

Nakumbuka miaka ya nyuma nilikuwa hospitali fulani ya RUFAA mkoa X, daah HRO alimfanyia zengwe DHRAM akahamishwa kazi, na palikuwa na madaktari bingwa wa upasuaji, Daktari mmoja alikuwa jamaa mmoja mchagga yule jamaa alikuwa balaa daktari balaa, wale ma daktari walikuja kuhama ile taasisi kutokana na UNAAA wa yule HR (mdada) acheni hizo Ma HR. Msisahau kuna siku mtarudi kitaa baada ya kustaafu.
 
Back
Top Bottom