Tax exemption for UN Personnel

Tax exemption for UN Personnel

kidumeso

Member
Joined
Mar 23, 2007
Posts
49
Reaction score
12
Jamani ninaomba kuwasilisha mawazo ya wengi kwenu wana jamii, hivi inakuwaje watu wanaofanya kazi na mashirika ya umoja wa mataifa wanakataliwa kukununua kitu (gari) na kukiingiza nchini bila kulipia ushuru, wakati wafanyakazi wa serikali (Madaktari,Wanajeshi,Walimu n.k) wanapewa kipaumbele kwenye hilo.
Kilichonipelekea kuulizia hili ni kwamba kila mtumshi wa umoja wa mataifa anakatwa kwenye mshahara wake kiwango fulani cha pesa kikiwa ni sehemu ya pesa zinazoongezwa kwenye serikali ya Tanzania kuchangia kwenye umoja huo, cha kushangaza ukitaka kuingiza kitu (gari) ulichonunua ukiwa kwenye kazi hizi za umoja wa mataifa unaelekezwa inakubidi uwe umekinunua na kukitumia kitu hicho kwa muda wa mwaka mmoja, sasa kama upo sehemu ambapo kuna mapigano yanaendelea utawezaje kutumia kitu hicho (gari), kama jinsi hali ilivyo basi watumishi wengi wa mashirika haya hawatendewi haki na serikali yetu, nitafurahi kama kuna mtu wa serikali atakayeweza kulitolea ufumbuzi suala hili ambalo lina tuumiza kichwa watu wengi.
 
Kila mtu akitaka asamehewe Kodi sasa hii Nchi yetu Tutaijenga Vipi? Wakulima ndio Hivyo Hawalipi hata sent Moja!! Hata na wewe mfanyakazi wa UN? Acha hizo nenda Kalipe Hiyo Kodi!! Ila najua zinachakachuliwa ila ni muhimu Kulipa
 
Kwanza hebu toa sababu zinazokufanya wewe au nyie mfikirie kuwa mnaumuhimu sana mpaka msamehewe kodi?????
 
Babalao hiyo kauli mbiu yako ya tuwatoe meno tehe tehe kwi kwi
 
Sawa unalipia staff assesment ambayo inaenda serikalini lakini haulipi kodi ambayo wafanyakazi wengine wa serikali ulipia,sasa wewe na mshahara wa mamilioni tena international staff unataka exemption ya kodi,sasa nani alipe?huna hata aibu ,tena wewe tungetegemea ungekuwa unaiomba serikali ulipie mara mbili ya kiwango kilichowekwa ili utunishe mapato,hapo tungekuelewa mshikaji.
 
Back
Top Bottom