Tax on rental income

Tax on rental income

Joined
Jul 24, 2015
Posts
80
Reaction score
38
Jamani naomba msaada ninapangisha kwa mkataba wa 5 years lakini makubaliano ni kama ifuatavyo (1) Kodi ya pango kwa mwaka ni 12. Million. (2) Mpangaji atafanya ukarabati utakao gharimu TShs 30 Million na kumlipa mkandarasi mojakwamoja hizo pesa ni nusu ya kodi yote ya pango kwa miaka mitano, hivyo mimi atakuwa akinilipa TShs 6 Million kila mwaka.

Na TShs 6 Million inayobaki inafidia gharama za ukarabati kwa miaka yote mitano. Naomba msaada nijuwe kodi (tax) ambavyo natakiwa kulipa TRA kwa ajili ya rental Income ni kiasi gani?
 
Hapo inatategemea makubaliano yenu wewe na mpangaji,Kwanza kama atakuwa analipa Withholing tax kabla ya Kodi au baada ya kodi ila kwa Mujibu wako ni hivi

Mkataba ni miaka mitano kwa TZS 12M kwa mwaka hapo inatakiwa ukatwe asilimia 10 ambayo ni TZS 1,200,000 kwa mwaka na kwa miaka mitano hiyo utalipa kwa TRA TZS 6M.

Ila unaweza kubaliana na mpangaji hii gharama atailipa yeye conditions unaweka Withoholding tax italipwa na mpangaji mwenyewe yeye akulitee Risiti ya TRA tu.
 
Hapo inatategemea makubaliano yenu wewe na mpangaji,Kwanza kama atakuwa analipa Withholing tax kabla ya Kodi au baada ya kodi ila kwa Mujibu wako ni hivi

Mkataba ni miaka mitano kwa TZS 12M kwa mwaka hapo inatakiwa ukatwe asilimia 10 ambayo ni TZS 1,200,000 kwa mwaka na kwa miaka mitano hiyo utalipa kwa TRA TZS 6M.

Ila unaweza kubaliana na mpangaji hii gharama atailipa yeye conditions unaweka Withoholding tax italipwa na mpangaji mwenyewe yeye akulitee Risiti ya TRA tu.

Lakini mkuu Mtu wa Kigamboni kiukweli ana gharama za kukarabati nyumba yake ambayo ni 6M kila mwaka. Hii M6 sio hela inayoingia mfukoni mwake bali inatoka kwenda kutengeneza nyumba (business expense).

Na katika hiyo gharama ya kukarabati itabidi aongeze gharama nyingine zake za ku-supervise matengenezo ya nyumba yake. (tuseme M3 kwa mwaka). Kwa hiyo pato lake kwa mwaka pengine ni M3 au chini ya hapo kwa mwaka.

Ni hivi, nitarudia tena:
  1. Anapata kodi ya M12 kwa mwaka (pato)
  2. Analipa M6 kwa mkandarasi kwa mwaka (business expense)
  3. Anahangaika kuhakikisha nyumba inakarabatiwa vizuri - gharama yake M3 au M4 kwa mwaka
  4. Net revenue inayoingia mfukoni ni M3 au M2 kwa mwaka (Hii ndio ya kupigwa kodi na TRA)

Mimi ningemshauri atafute accountant amuwekee mahesabu vizuri. Ni muhimu katika ujasiriamali tujue namna ya kuweka gharama zetu sisi wenyewe kabla ya kulipa kodi.

Kwa mawazo yangu ni kuwa huyu bwana kipato chake kwa mwaka anachopaswa kulipia kodi ni M2 tu. Na kama ni 10% basi anapaswa kulipa Tsh. 200,000 tu kwa mwaka.
 
Na mimi naona hiyo TShs 30 Million ni Capital expenditure sitakiwi kulipia kodi. Wataalamu mnasemaje?
 
Na mimi naona hiyo TShs 30 Million ni Capital expenditure sitakiwi kulipia kodi. Wataalamu mnasemaje?

Hata mimi naona hivyo hivyo. Lakini uongezee hapo juu administrative/supervisory costs zako ambazo ni kadri ya m15 mpaka M20 katika kipindi cha miaka 5. Kinachobakia ndio net revenue yako ya kupigwa kodi.

Hii ni biashara, usiite kipato income bali ni revenue ya biashara na ni lazima utoe expenses zako, kinachobaki mzungumze na TRA.

In fact kama unaendelea kuongeza majumba mengine ya kupangisha na unaitumia hiyo net revenue (pengine na mshahara wako) kuendeleza hiyo biashara, unaweza kujikuta unakuwa na negative cash flow ambapo hupaswi kulipa kodi yoyote. In fact kama uki-record loss mwaka huu unaweza kuitumia kupunguza kodi za miaka ijayo.

Ngoja tusubiri wataalam waje watoe ushauri.
 
Maana kuna gharama za mawakili, dalali, property tax n.k. Watu wa TRA karibuni mnipe Dalasa.
 
Serio, Tafadhali tupatie ujuzi wako. Watu wa Chuo cha Kodi hapa ndiyo kwenu mjitokeze!
 
Dah, am just helping you because umeleta uzi hapa kwa wanajamii but next time u have to pay for this consultancy service:

Ok lets come back on the issue: Tax on rental income iko hivi kama ifuatavyo:

huyo mapangaji anatakiwa akate kodi ya 10% (rental withholding tax) immediately kwenye hyo lump sum ya 30m atakayokulipa kwaajili ya wewe kumlipa huyo mkandarasi. kwahyo 10% ya 30M ni 3M kwahyo wewe utapokea 27M.


Pia hyo 30M nyingine iliyobaki atakua anakulipa kwa yearly instalment ya Tshs 6M. vilevile kwa kila mwaka huyo mpangaji atatakiwa kukata 10% ya Withholding tax ambayo ni Tshs. laki 6. Kwahyo wewe itapokea 5.4M kwa kila mwaka.

Genarally, kwenye 60M uliyotakiwa upokee kama rental income, utapokea jumla ya Tshs 54M, na 6m zilizobaki ni kodi.


kwa upande wa makandarasi utakayompa tenda ya kufanya ukarabati Tax yake iko hivi:

30M utakata 5% endapo mkandarasi ni resident(service fee withholding tax) ambapo huyo mkandarasi atapokea Tshs. 28.5M. Na endapo huyo mkandarasi ni non-resident, na utakata 15% ambapo sasa mkandarasi atapokea Tshs. 25.5M


Angalizo. Hizo wittholding tax zinazokatwa zinatakiwa ziwe remitted to TRA, sio zenu!!:mad2::mad2::mad2:
 
Back
Top Bottom