Tazama baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza katika majina ya ajira za Ualimu yaliyotolewa. Jina la 'ABADALLAH LEONARD SHONDE lajirudia mara 196

Anarudia mtihani wa form four wa nini kama alishafika chuo na akasomea ualimu? How can people be this foolish hata kuchambua vitu virahisi? So kasomaje chuo hadi aje aresit saivi smh
 
Anarudia mtihani wa form four wa nini kama alishafika chuo na akasomea ualimu? How can people be this foolish hata kuchambua vitu virahisi? So kasomaje chuo hadi aje aresit saivi smh
Mkuu kwenye maisha kila mtu ana focus yke na kumbuka kwenye familia zetu Kuna presha za familia wala sio Jambo la ajabu inawezekana alisomea ualimu (bila kupenda) hakupata ajira akabaki mtaani 2019 akamua kurudi kutegeneza na kutafuta credit ili aweze kutimiza ndoto na hitaji lake kwani hairushiwi?
 
Watanzania tunatia haibu Dunia nzima
 
Usikute hata Halima mwenyewe hajuwi kama kachaguliwa kuwa mwalimu ila kutakuwa na mtu anataka kutumia hilo jina ili apate kazi serikalini.
 
Wewe acha viswahili vingi.

Hata awe amerudia mara mia mbili........ mwaka wake wa kumaliza kidato cha nne ni 2019. FULL STOP.

Ntantarira mingi.... ikaenda ikarudi...... sijui alienda kwa bibi ake akarudi kufanya mtihani, mara aliugua kifafa....

Hii orodha nzima ya majina hewa ina mushkeli karibu kila mahali. Majina megi humu ni ya kupikwa.

Wacha viswahili vyako!
 
Sasa kama alisomea ualimu, kwanini asingeajiriwa kwa kutumia namba yake ya kidato cha nne iliyotumika kusomea ualimu?

Inawezekanaje itumike namba ambayo haishabihiani na qualifications zake za kitaaluma?

Wacha maneno mengi wewe!

Ujanja ujanja tu na viswahili vingi!
 
Mkuu piga spana hawa mbumbumbu. Eti mtu karudia mtihani mwaka jana, kaomba nafasi ya kazi kwa matokeo ya mwaka jana kisha kaajiriwa kwa matokeo ya zamani ambayo hayakumpa vigezo vya kupata kazi.
Sasa sijui matokeo ya form four mwaka jana yamempeleka lini chuo miaka miwili/mitatu mpaka kuwa na vigezo kuajiriwa.
Hizi ni bhangi
 
Si bora huyo ni private candidate
Angalia vizuri kuna school candidate wengi tu wamemaliza form four mwaka jana na wamepata ajira
 
Hizi ajira zinamagumashi kibao....Katibu Mkuu haponi! Tusubiri
 
We jamaa kwani lazima umuonyeshe kwa umma mdada wa watu......

Be patient mkuu
Ajira utapata
 
Na usipochukua hatua za haraka dhini ya hao wafanyakazi wa tamisemi tutajua unewatuma wewe
 
Dogo langu limekosa nimebidi nilinunulie TVS liwe bodaboda
Ndo hivo hakuna namna watu wanacholalamika si kukosa ila ni kwa nini watoe majina katika hali hyo ikiwa walikuwa na mda wa kutosha kufanya uchambuzi mzuri
 
Kuna mwingine kapangiwa , kufundisha , history , kiswahili na mathematics ,

Sasa sijui huyu alisoma combination ipi?
 

TAMISEMI HAWAKUONYESHA UMAKINI KWENYE MCHAKATO WA AJIRA ZA WALIMU ?

Mimi kama mdau wa elimu hapa nchini nimekuwa nikifatilia mchakato mzima wa hizi ajira za ualimu yaani tokea kuomba mpaka kutangazwa kwake na haya ndio machache niliyo yagundua;

1.Mfumo wa kuomba ajira yaani OTEAS ulizidiwa pale pale mwanzo na kufanya ugumu katika kuomba ajira hizo kwa zaidi ya siku 15.

2. Udanganyifu wa idadi ya watakao ajiriwa na walio ajiriwa ( ajira walitangaza ni 13,000 lakini wameajiri 9,000 +, je kama kibali cha ajira kilikua ni cha watu 13,000 hao watu wengine wameajiliwa wapi au wanabana matumizi?).

3. Mchakato sio wazi na shindani (non competitive and lack of transparent). Hawakusema wametumia kigezo gani kuajiri waliowaajiri na kuwaacha wengine kati ya wengi walio omba hizo ajira.

4. Uzembe na Uvivu. hii imejidhihirisha wazi kabsa kwa jina moja kujitokeza mara 196 inamaana wameprint tu na kuzitoa wameshindwa kuyapitia hayo majina na pia kushindwa kuweka namba kwenye majina hayo ili watu washindwe kutambua idadi halisi.

5. Kutoainisha majina kama mahitaji yalivyokua yakionesha kwenye tangazo la kazi yaani kwa taaluma mbali mbali kama lab technician 10 na majina yao haya au walimu daraja la 111 A 150 na majina yao haya wa 111 C. 670 na majina yao. Kuliko kuyachanganya na kufanya mkanganyiko kwa waliomba na jamii kwa ujumla.

6.Wasi wasi wa utendaji wao wa kazi na kazi yao kwa ujumla ( kwa waombaji )



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…