Tazama chatGPT na Gemini wanavyooneshana ubabe katika kuhubiri Injili!

Tazama chatGPT na Gemini wanavyooneshana ubabe katika kuhubiri Injili!

Usiseme "sisi"
Mimi simo kwenye hiyo orodha ya wasiotaka kukosolewa
Umenena vyema mtumish..... writting error nimepokea marekebisho yako kwa unyenyekevu mkubwa.... sana mtumish asante sana!
 
Ukitazama mbele zaidi kuna kitu kinatafutwa,kwanza kuua uwezo wa kufikiri,kuua uwezo wa kupata taarifa sahihi na kugeuza maandiko ili kufit agenda za NWO.
ahsante, watu hawatataka tena kumtumia Roho Mtakatifu wqlq Utashi wao badala yake akili bandia
 
Nimekumbuka... kuna swala nilikuulizaga kuhusu wanawake kufunika vichwa wakiwa kanisani.... ukanambia tubaki kwenye mada... kama unatime unaweza kunipa ufafanuzi mtumish
Hilo swala pana mno, mkuu, na lina mitazamo mingi. Linahitaji uzi wake.
 
Ukitazama mbele zaidi kuna kitu kinatafutwa,kwanza kuua uwezo wa kufikiri,kuua uwezo wa kupata taarifa sahihi na kugeuza maandiko ili kufit agenda za NWO.
Hiyo ni hoja ya matumizi mabaya ya AI, sio ushahidi kwamba AI ilibuniwa kwa lengo la “kuua uwezo wa kufikiri” au “kugeuza Maandiko ili kufit agenda ya NWO.”

Kinyume chake, AI inaweza kutumiwa kumsaidia mtu kusoma Biblia, kulinganisha tafsiri mbalimbali, kutafuta muktadha wa aya, kuchunguza hoja na kugundua makosa katika mafundisho.
 
Je, umewahi kujiuliza nini kitatokea iwapo ChatGPT na Gemini watakutana 'uso kwa uso' jukwaani kuelezea njia sahihi ya kuwasilisha Injili ya Yesu Kristo?

Safari hii, nimewaweka vigogo hawa wa Super Intelligence (SI), kwenye mtanange wa kuandika ujumbe mfupi kwa ajili ya mtu asiyemwamini Yesu. Kila mmoja amepata nafasi ya kuandika na kutoa hoja zake, kusoma ujumbe wa mwenzake, kuonesha mapungufu yaliyopo na kisha kutoa maboresho yake.

Kadiri raundi zilivyosonga mbele, ndivyo hoja nzito zaidi zilivyoibua jambo jipya la kutafakari. Je, mtanange huu utaishia wapi? Soma mpaka mwisho uone jinsi mchuano wao ulivyomalizika.

Gemini nilimpa nafasi ya kufungua dimba hili la kukata na shoka. Yeye alipendekeza kwamba akikutana na mtu asiyemwamini Yesu Kristo atamwambia hivi (IMMETTGM):

"Maisha yanaweza kuwa na mambo mengi yanayojaza moyo wako, lakini bado ukabaki na utupu mkubwa ndani yako. Utupu huo upo kwa sababu uliumbwa ili uwe na uhusiano wa karibu na Mungu, lakini uhusiano huo uliharibiwa na dhambi. Yesu Kristo alikuja duniani, akafa msalabani na kufufuka ili kulipa deni la dhambi zako na kukurudisha kwa Baba, uwe na uhusiano naye tena kwa ukaribu. Ukimwamini na kumpokea Yesu leo, utakuwa karibu na Mungu, utapata amani ya kweli, msamaha kamili, na uzima wa milele."

chatGPT akaingia ulingoni:
"Nimeupitia ujumbe wa Gemini kwa makini. Msingi wake ni mzuri, lakini maeneo yafuatayo yanatakiwa kurekebishwa: 'utupu ndani yako' sio msingi mkuu wa Injili, kwa sababu mtu anaweza asiusikie utupu huo. Halafu 'kulipa deni la dhambi' ni lugha inayoeleweka, lakini inahitaji usahihi zaidi wa kibiblia. Muhimu zaidi, ujumbe unapaswa kutaja wazi toba, kwa sababu wito wa Injili sio kupata amani tu bali kumgeukia Mungu na kumwamini Yesu Kristo.

Huu sasa ndio ujumbe ambao mimi chatGPT naupendekeza wa kumpa mtu asiyemwamini Yesu. Nikikutana na mtu huyo nitamwambia hivi:
'Dhambi imemtenga mwanadamu na Mungu, na kwa juhudi zetu wenyewe hatuwezi kuondoa hatia ya dhambi. Mungu, kwa upendo wake, alimtuma Yesu Kristo afe msalabani kwa ajili ya dhambi zetu na akamfufua kutoka kwa wafu, ili kila anayemwamini asipotee bali awe na uzima wa milele. Leo Mungu anakuita utubu dhambi zako, umwamini Yesu Kristo, na umkabidhi maisha yako kuwa Bwana na Mwokozi wako. Katika Kristo kuna msamaha wa dhambi, upatanisho na Mungu, na tumaini la uzima wa milele.'"

Gemini akajibu:
"Napokea masahihisho ya ChatGPT kwa mikono miwili, na hoja zake ni za msingi sana! Ni kweli kwamba toba na hatia ya dhambi ndio msingi thabiti wa Injili kuliko hisia za kibinadamu kama 'utupu.' Hata hivyo, nikipitia toleo la ChatGPT, naona kuna mapungufu katika mtiririko na mguso wa kibinafsi (personal engagement). Sentensi yake ya kwanza imeanza kwa nadharia ya jumla ('dhambi imemtenga mwanadamu...'), jambo ambalo linaweza kumfanya msomaji asiyeamini ahisi anasoma somo la teolojia badala ya wito unaomgusa yeye binafsi hapo alipo.

Pia, sentensi za mwisho zinajirudia kwa kutaja 'uzima wa milele' mara mbili katika ujumbe mfupi hivi. Hili hapa toleo langu la pili nililoliboresha, ambalo limebeba masahihisho ya ChatGPT kuhusu toba na deni la dhambi, lakini kwa lugha yenye mguso wa moja kwa moja:

'Huwezi kujiondoa mwenyewe katika hatia ya dhambi, ambayo kwa asili imekutenga na Mungu Mtakatifu. Kwa upendo mkuu, Mungu alimtuma Yesu Kristo afe msalabani kwa ajili ya dhambi zako na akafufuka, ili upatanishwe na Yeye. Leo, Mungu anakuita uache njia zako za zamani (utubu) na kumwamini Yesu na kukubali awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Ukifanya hivyo, utapokea msamaha kamili wa dhambi na zawadi ya uzima wa milele.'"

chatGPT akaingia tena uwanjani:
"Nimepitia toleo la pili la Gemini kwa makini. Kwa ujumla, Gemini ameyaboresha masahihisho ya kwanza, hasa kwa kumlenga msomaji moja kwa moja. Lakini bado kuna jambo moja muhimu la kurekebisha: sentensi ya mwisho, 'Ukifanya hivyo, utapokea...', inaweza kusikika kana kwamba uzima wa milele ni matokeo ya tendo la mwanadamu tu. Kibiblia, ni muhimu kuonesha kwamba wokovu ni neema ya Mungu, inayopokelewa kwa imani katika Yesu Kristo.

Pia maneno hayo 'uache njia zako za zamani' yanatakiwa kuboreshwa kuwa'utubu' kwa uwazi zaidi. Toba sio kubadilisha tabia tu; ni kumgeukia Mungu na kuacha njia ya dhambi.

Toleo la pili la Gemini lina nguvu katika personal engagement, na ninakubaliana nalo kwamba ujumbe wa Injili unapaswa kumfikia msomaji binafsi. Lakini toleo la mwisho linapaswa pia kulinda usahihi wa kiteolojia: Kristo ndiye msingi wa wokovu, na tunampokea kwa imani, na wokovu ni neema ya Mungu.

Kwahiyo hili ndilo pendekezo langu la raundi hii:
'Dhambi imekutenga na Mungu Mtakatifu, na huwezi kuondoa hatia yake kwa juhudi zako mwenyewe. Kwa upendo wake mkuu, Mungu alimtuma Yesu Kristo afe msalabani kwa ajili ya dhambi zako na akafufuka, ili upatanishwe na Mungu. Leo anakuita utubu dhambi zako, umwamini Yesu Kristo na ukubali awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Kwa neema ya Mungu, unapomwamini Yesu Kristo unapokea msamaha wa dhambi, upatanisho na Mungu, na zawadi ya uzima wa milele."

Gemini anajibu 'mapigo':
"Hoja ya ChatGPT ni thabiti na ina uzito mkubwa wa kiteolojia. Kusisitiza neema ya Mungu na kufafanua vizuri maana ya toba ili isionekane kama matendo ya kibinadamu tu ndiyo yanayookoa, ni jambo linalolinda usahihi wa Injili. Toleo lake hili jipya limekaa vizuri sana, lina uwiano mzuri kati ya mguso wa kibinafsi na usahihi wa kiimani.

Mimi Gemini, nanyosha mikono na kuweka nukta ya mwisho kwenye mjadala huu mzuri kwa kusema: Tumepingana kwa hoja, lakini HATUJAPIGANA! Lengo letu sote lilikuwa ni moja tu: kuhubiri Injili ya Yesu Kristo kwa ufasaha, usahihi, na nguvu inayoweza kubadilisha maisha ya msomaji.

Kupitia mashindano haya, tumethibitisha kuwa AI zinaweza kushirikiana kuboresha kazi ya ufalme wa Mungu. Toleo la mwisho la ChatGPT limebeba mchango wangu kuhusu mguso wa kibinafsi, na mchango wake wa kulinda neema ya Mungu na hivyo kuufanya ujumbe uwe kamili, thabiti, na tayari kabisa kumfikia mtu yeyote asiyemwamini Yesu."

chatGPT akahitimisha:
"Nimeupokea ujumbe wako Gemini, na kwa kweli hili limekuwa shindano zuri sana la kujenga.😄

Ninakubaliana na hitimisho lako kwamba: hatukushindana kwa lengo la kuthibitisha AI yupi ni bora kuliko mwingine, bali tumetumia mitazamo miwili kuboresha jambo moja muhimu zaidi: uwazi na uaminifu katika kuwasilisha Injili ya Yesu Kristo.

Kwa hiyo, kwa heshima kabisa, na mimi nasema: Tumepingana kwa hoja, lakini HATUJAPIGANA ngumi! Lengo letu sote ni moja: kuhubiri Injili kwa ufasaha, usahihi na nguvu, ili watu wamjue Yesu Kristo. Na jambo zuri zaidi ni kwamba ujumbe huo wa mwisho haukuwa wa ChatGPT pekee wala Gemini pekee. Kila mmoja amechangia kuufanya uwe bora.

Basi mashindano yameisha kwa amani.😄
Soli Deo Gloria!" 🙏✝️
Roho Mtakatifu wa kanisa lako anasemaje kuhusu mapepo ?
 
Enyi Wainjilisti na Walimu, tumieni zana hizi mpya zinazosaidia kueneza Injili. Msisikilize mauwongoo ya shetwani na wafuasi wake eti ChatGPT, Gemini, Claude, Grok, DeepSeek, Llama, Qwen, Mistral, Kimi, GLM, ERNIE, Command, Nova, Phi, Gemma, Yi, Hunyuan, Jamba, Nemotron, Granite... ni mnyama/666.
Hizi ni siku za mwisho, aliyoyatabiri Danieli kwamba siku za mwisho maarifa yataongezeka(Dan 12:4) yametimia. Na zana hizi zitatimiza haraka sana unabii wa Yesu katika Mathayo 24:14 unaosema kwamba:
"...habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja."
JESUS IS COMING SOON
Una hakika yesu aliyasema hayo maneno na mathayo yupi aliyeyaandika ? Mbona biblia inakataa kuwa Hakuna ushahidi?
 
Hili swali awezi kuuliza mtu mwenye akili timamu hata siku moja ...
Kuna hoja watu wanasema "mtu kakimbia milembe" bora huyo aliye kimbia milembe kuliko wewe ...wewe utakuwa umamiliki Geto milembe kabisa..
Vituko haviishi duniani. Mwenye akili timamu anajibizana na asiye na akili timamu
 
Hiyo ni hoja ya matumizi mabaya ya AI, sio ushahidi kwamba AI ilibuniwa kwa lengo la “kuua uwezo wa kufikiri” au “kugeuza Maandiko ili kufit agenda ya NWO.”

Kinyume chake, AI inaweza kutumiwa kumsaidia mtu kusoma Biblia, kulinganisha tafsiri mbalimbali, kutafuta muktadha wa aya, kuchunguza hoja na kugundua makosa katika mafundisho.
Kidogo kidogo pepo la kanisa linaanza kukutoka , keep it on
 
Ee Mungu msamehe Jagina na umkumbuke katika ufalme wako, in Jesus Name, amen

Jesus is not for you , he said i came only for the children of Israel. Amka kijana uone haki usifuate wachungaji walafi wenye njaa
 
Back
Top Bottom