Tazama chatGPT na Gemini wanavyooneshana ubabe katika kuhubiri Injili!

Jesus is not for you , he said i came only for the children of Israel. Amka kijana uone haki usifuate wachungaji walafi wenye njaa
Namshukuru Mungu unashawishika kusoma mada za kiroho na kuchangia. Hiyo ni dalili njema kuwa Mungu anakuvuta uingie zizini.
 
Ee Mungu msamehe Jagina na umkumbuke katika ufalme wako, in Jesus Name, amen

Namshukuru Mungu unashawishika kusoma mada za kiroho na kuchangia. Hiyo ni dalili njema kuwa Mungu anakuvuta uingie zizini.

Yesu ametumwa na Mwenyezi Mungu. Ametumwa awendee nani? Hebu tuiache Biblia itueleze:

Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni. Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo. Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu. Akajibu, akisema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Naye akaja akamsujudia, akisema, Bwana, unisaidie. akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani za bwana zao. Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile. Mathayo 15.21-28

Kwa maneno yasiotatanisha Yesu Kristo anasema kuwa yeye hakutumwa ila kwa "kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli."

Hakuwajia Waarabu, wala Wazungu, wala Wahindi, wala Waafrika, wala Machina.

Kama hayo hayakutosha kuonyesha kuwa yeye hakuwajia wasio Mayahudi anazidi kufahamisha kwa mfano wa kumkata mtu kiu:

Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa." Ikiwa ipo shaka yo yote katika akili ya mtu kuwa maana ya maneno hayo ni kuwa Yesu anasema kuwa hakutumwa kwa kabila nyengine zo zote ila Waisiraili tu na atazame mwenye shaka tafsiri kubwa kabisa ya Wakristo inayoeleza maana wazi maneno ya Biblia, The Interpreter's Bible, sahifa 441 jalada VII ambamo imeandikwa hivi:

"Yaonekana wazi kuwa Yesu hakika aliamini kuwa ujumbe wake kwanza na khasa ni kwa watu wake mwenyewe." Ndio maana alisema:

Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.

Mathayo 7.6

Mbwa na nguruwe ni watu wa mataifa yasiyokuwa wana wa Israili.

Ukristo haufai kufundishwa watu wo wote isipokuwa Mayahudi.

Hayo ndiyo mawazo ya Yesu, au ya hao walioandika Injili na wakatia maneno hayo kinywani mwa Yesu.
 
Acha uchoyo, mtumishi!
Dakika 2 unaziona chache wakati masaa 24 yenyewe hayanitoshi
Tunaweza kuongea na Aristotle kwa kusoma kitabu kuhusu Aristotle, lakini tutakua hatuwezi kumuuliza maswali zaidi ya kusoma aliyoandika kwenye kitabu,
Sasa tunataka kutengeneza mfumo ambao utanyonya mawazo yote ya mtu mwingine kama aristotle Ili tuweze kuzingumza nae moja kwa moja ' to and fro'

Nipe sadaka
 
Nadhani bado hujaelewa kwanini jina "AI" limebadilishwa kuwa "Super Intelligence."
 
Reactions: Lax
Umejenga hitimisho kabla hujaangalia Biblia nzima inasemaje.
Ukitaka kuielewa Biblia, usichukue mstari mmoja unaoupenda wewe na kuufanya uwe fundisho lote. Soma mstari huo pamoja na mistari iliyotangulia na inayofuata sura nzima, na mafundisho ya Biblia kwa ujumla. Hivyo soma Biblia yote kuanzia kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo. Soma kitabu kwa kitabu, sura kwa sura na aya kwa aya.

Hata hivyo, huwezi kuielewa Biblia kikamilifu kwa sababu hujaokoka. Ukiokoka, utajazwa Roho Mtakatifu. Kazi mojawapo ya Roho Mtakatifu ni kutuongoza na kututia kwenye kweli yote.

Na baada ya kuokoka na kujazwa Roho Mtakatifu, unatakiwa pia ujiunge na Kanisa la watu waliookoka, lenye watumishi wa Mungu wenye karama ya ualimu. Hao watakufundisha vizuri Maandiko.

Sasa kwa ufupi kuhusu hoja zako: Ni kweli Yesu alisema, “Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli” (Mathayo 15:24), lakini kama ungeendelea kusoma Biblia yote ungeona kwamba baada ya kufufuka, Yesu aliwaagiza wanafunzi wake wawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi (Mathayo 28:19), na Injili itangazwe “hata mwisho wa nchi” (Matendo 1:8). Isitoshe Paulo anasema wazi, “hakuna tofauti kati ya Myahudi na Myunani; maana Bwana ni Bwana wa wote” (Warumi 10:12).

Katika Yohana 3:16 tunaambiwa pia wazi kabisa kwamba Mungu aliupenda ulimwengu(ulimwengu ni sisi sote). Na baada ya kuupenda ulimwengu alimtuma Yesu ili kila mtu atakayemwaminiye asipotee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…