Tazama foleni hii ya wanunuzi wa sukari Morogoro. Juzi Waziri Bashungwa kapitishiwa bajeti ya hovyo iliyoungwa mkono na wanaccm wote Bungeni

Tazama foleni hii ya wanunuzi wa sukari Morogoro. Juzi Waziri Bashungwa kapitishiwa bajeti ya hovyo iliyoungwa mkono na wanaccm wote Bungeni

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
Hii ni foleni ya wanaonunua sukari Morogoro mjini ndani ya duka la mbunge wao.

Kinachonikera zaidi juzi waziri wa viwanda na biashara kapitishiwa bajeti mbovu sana huku wabunge wa CCM pamoja na spika wakijikita kuishambulia Chadema.

Aidha hawa ni wanunuzi wa jumla. Unapata Corona na sukari halafu ukitoka hapo wanakuja watu wa serikali za mitaa wanataifisha.

Kishindo cha awamu ya tano kwelikweli!

IMG_20200510_084158.jpg
 
Jana nimeenda sehemu asubuhi nataka chai naambiwa hakuna, kuuliza kwanini wanasema sukari hakuna madukani.

Wanawalazimisha wauzaji wa rejareja wauze kwa bei wanazotaka serikali (bei elekezi), wakati hao jamaa walinunua sukari yao kwa bei ya juu toka kwa wauzaji wa jumla, wauzaji wa rejareja walichoamua sasa ni kuificha sukari yao, hawaiuzi wasijepata hasara.

Ndio nikapata akili, naona siku hizi kama taifa tumeanza kurudi nyuma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili la sukari nalo mpaka Rais alisemee kweli,,? Sukari tu
 
Hao jamaa hata hawajavaa barakoa, au wapo Lesotho nini? Hawana kabisa wasiwasi, sukari imewavuruga akili. Serikali ilipanga bei elekezi bila kujua upatikanaji wa sukari, acha tu waifiche, hakuna aliye tayari kupata hasara.
 
daahh.. hii kitu miyeyusho sana, ikipanda noma, ikishuka noma, na ndio hivyo hivyo ilivyo hata kwenye miili yetu, balaa lake ukutwe na corona, yaani ni kama kumsukuma mlevi!
halafu kwenye nyomi kama hili huku waliovaa barokoa wanahesabika, aisee poleni
Kumbe hua inashuka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuadimika kwa bidhaa muhimu kama sukari ni moja ya viashiria vya mgogoro wa uchumi. Mgogoro huu unajitokeza mara kwa mara kwenye serikali ya awamu ya tano.

Wasije kusingizia mwezi mtukufu ndo unasababisha uhaba wa sukari wakati hali hii haikuwahi kutokea awamu zilizotangulia na mwezi mtukufu ulikuwepo.
 
Back
Top Bottom