1. KKKT? Kwani amefungia kanisa gani hiyo ndoa?
2. Kubatilisha ndoa wala sio siri. Mfano unafunga ndoa na binti. Baadaye unagundua kuwa ana ndoa halali na mwanaume mwingine waliyetengana. Hakika hiyo ndoa ya pili ni batili. Ama unaoa mwanamke. Anapofia chumbani anagundua kuwa jogoo hawiki na ni tatizo lako la muda mrefu, hiyo ndoa ni batili. Lakini si kwa sababu ya kuzabwa vibao. Ndoa bado inasimama.
3. Kufunga ndoa nyingine bomani ni kuishi katika uzinzi, na kubadili dini haijawahi, na wala haitawahi kuwa sababu ya talaka. Hizi ndio unaziita sababu kuu na kusifia makanisa yako? Soma biblia.