Tazama hii picha utahisi uchungu na kulia. Inahusu mnyama

Ng'ombe akiwa kwenye foleni akisubiri kwenda kuchinjwa. Wanyama pia wanaelewa wanacho tendewa🥺😰😥

View attachment 3269463
Basi hata utumie ubongo wako kufikiria japo ulilenga kuwa na ujumbe wenye maana.

Picha unayoiona hapo ni ya ng'ombe mtoto, yaani NDAMA. Kwa kumuangalia tu, muonekano wa ngozi yake, batch number aliyobandikwa na hata nywele zake utafahamu fika hana muda mrefu tangu azaliwe.

Hivyo, wala hayupo kwenye foleni ili akachinjwe. Nani amchinje ndama wa masaa kadhaa?

Picha hapo juu, ni ndama anaumwa jicho. Uwekundu katika jicho lake linathibitisha. Na pengine ni ugonjwa wa ng'ombe uitwao pink eye.

Mimi si Vegetarian na kamwe siwezi kuwa. Mimi ni muumini, na naamini kuwa wanyama tuliopewa ni kwa matumizi yetu.
 
Umempiga za uso. 👊👊👊
 
Wewe kweli Genius . Maelezo yako ni pure kabisa.

Lakini je wanyama hawajui wanacho tendewa?
 
Mkuu hata akiwa mtoto watu tunachinja, kuna nyama wanaita Veal ni tamu sana, hawa viumbe wapo kwa ajili hiyo
 
Mkuu hata akiwa mtoto watu tunachinja, kuna nyama wanaita Veal ni tamu sana, hawa viumbe wapo kwa ajili hiyo
Dah hata huruma huna bruh. Unaandika kikatili sana.
 
Bahati mbaya au nzuri wameandikiwa waliwe maisha Yao ni mafupi so hakuna namna.
Vuta picha wewe pia ungekuwa ng'ombe halafu unasikia fulani anasema mambo hayo?

Kikubwa wanyama wanatendewa ukatili. Kwani hatuwez kula majani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…