Tazama mambo makubwa 5 yaliyoboreshwa Tanzania

Tazama mambo makubwa 5 yaliyoboreshwa Tanzania

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Serikali ya awamu ya sita imeboresha mazingira ya uwekezaji na haya ni baadhi ya maeneo ambayo yameboleshwa;

Uchumi Imara
Uchumi wa Tanzania umekua kwa asilimia 4.9, hii inatokana na mageuzi makubwa ya kiuchumi na sera nzuri nchini zilizofanya na Rais Samia Suluhu Hassan

Utajiri wa maliasili
Rais Samia kupitia filamu ya “The Royal Tour Tanzania” ameweza kutumia maliasili na vivutio vinavyopatikana Tanzania kama vyanzo vya kuwavutia wawekezaji hapa nchini

Eneo la kijiografia
Tanzania inapakana na bahari ya Hindi, Mh. Samia Sulhu Hassan ameimarisha Bandari za Tanzania na kuchochea moja kwa moja Biashara na kuunganisha bala la Asia nachi kama Uganda, DRC Congo, Rwanda na Burundi .

Amani na utulivu wa kisiasa
Rais Samia ameendeleza na kuimarisha Amani na utulivu wa kisiasa, hii imesaidia sana katika uwekezaji Tanzania

Miundombinu bora
Chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, ameendeleza na kujenga miundombinu mipya nchini, huduma hizi zinachochea sana uwekezaji

Rais Samia Suluhu Hassan anatufungulia dunia tuendelee kumuombea afanye mambo makubwa zaidi
 
Uchumi gani huu wa kujivunia mkopo wewe?

Isitoshe tumeshuka kutoka uchumi wa Kati daraja la chini hadi nchi ombaomba.

Hadi mashoga nao wanaleta masharti na tunasujudu.

Embu punguza mbwembwe wakati life limevaa tight.
 
Serikali yapaswa ongelea mfumko wa bei, maana kwa hesabu ya kawaida kwa wastani, yawezekana twalingana na Uturuki
 
Back
Top Bottom