JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Wahudumu wa Afya wakiendelea na shughuli ya mazishi ya watu waliouawa wakati wa mapigano Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yaliyohusisha jeshi la nchi hiyo na Wapiganaji wa Kundi la M23.
Mkuu wa ujumbe mdogo wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu Mashariki mwa DRC, Miriam Favier amesema kuna hitaji la dharura la kuizika miili hiyo, kwani vyumba vingi vya kuhifadhia maiti vipo hospitali, na hii inaonesha kuna hatari ya kuzuka kwa magonjwa ya mlipuko.
Source: AFP, Al Jazeera