Samedi Amba LLC
Member
- Apr 5, 2024
- 81
- 117
Habari wanajamvi. Ni mimi tena. Leo tutaongelea mambo manne makuu ambayo yatatokea katika ukuaji na utumiaji wa AI (Akili bunifu/bandia/mnemba) nchini Tanzania.
Kama unajiuliza kuwa akili mnemba ndo ipi jamaa kadadavua hapa vizuri: Nini Maana ya AI (Akili Mnemba)
Sasa, turudi kwenye mada. Mambo manne makuu ndo haya hapa:
1. Roboti mazungumzo zilizobinafsishwa (Customized Chatbots)
Leo, ukitaka kutumia AI, unaenda kwenye mitandao kama ChatGPT na Gemini. Sasa, hizi zimetengenezwa na kanzi data ya wazi (open information) ambayo mtu yeyote anaweza kupata mtandaoni.
2024, roboti zilizobinafsishwa zimekuwa hitaji la lazima katika kufanya biashara kidijitali. Roboti kama hizi zimekuwa mahiri katika kukidhi mahitaji muhimu ya biashara na wateja.
Faida zifuatazo ni dhahiri:
GPT kama hizi zinawezeshwa na custom LLMs (mfumo anzishi ya kutengeneza app kama chatGPT). Kwa kutengeneza app binafsi inayofanana na chatGPT, kuna uwezo wa kubinafsisha data (au kuifanya kuwa ya siri), ili isitumike vibaya na makampuni makubwa kama Google na Microsoft ambao tayari washatawala dunia ya AI.
2. Video zitatengenezwa Kutumia AI (Generative AI for Video)
Mwaka 2022, video ya kwanza inayotumia AI ilitengenezwa rasmi. Miezi 22 tu baadaye, utengenezaji huo ulizidi matarajio. Mwaka 2024, tutarajie yafuatayo:
Kumbuka kisa cha Gwajima. Inaonekana ilitengenezwa. Zamani, ilihitaji mtaalam kwelikweli kufanya kitu kama hicho. Ila siku hizi, ni rahisi tu. Shkamo AI.

- Kuhudumia wateja: Roboti hizi zinaweza kuelewa nia ya mtumiaji, kutoa taarifa muhimu, na hata kutarajia mahitaji ya wateja, hivyo kutoa huduma binafsi na inayotarajiwa kuwa muda fulani.
- Kufanya kazi zinazojirudia: Roboti hizi zinaweza kujibu maswali yanayojirudia rudia kama vile kujibu maswali yanayoulizwa mara kwa mara. Hivyo, biashara zinaweza kutumia muda wao katika kuzingatia mamboa ambayo ni nyeti zaidi.
- Ushindani: Kampuni zinazotumia roboti hizi zina uwezo wa kuwa na ushindani mkubwa zaidi sokoni, kwa kuwa wanaonekana kujali wateja zaidi (na hivyo kujenga uaminifu), kufanya maamuzi haraka, na kuwasiliana kwa kasi zaidi.
- Upanuzi wa mawasiliano: Roboti za mawasiliano zina uwezo wa kuwajibu wateja wengi kwa mpigo, hivyo kuwa bora kwa biashara za ngazi yoyote ile.
GPT kama hizi zinawezeshwa na custom LLMs (mfumo anzishi ya kutengeneza app kama chatGPT). Kwa kutengeneza app binafsi inayofanana na chatGPT, kuna uwezo wa kubinafsisha data (au kuifanya kuwa ya siri), ili isitumike vibaya na makampuni makubwa kama Google na Microsoft ambao tayari washatawala dunia ya AI.
2. Video zitatengenezwa Kutumia AI (Generative AI for Video)
Mwaka 2022, video ya kwanza inayotumia AI ilitengenezwa rasmi. Miezi 22 tu baadaye, utengenezaji huo ulizidi matarajio. Mwaka 2024, tutarajie yafuatayo:
- Fursa za Biashara: Kampuni nyingi zitachangamkia fursa hii. AI imewezesha makampuni haya kubadilisha mbinu ya utendaji na uzalishaji wa filamu. Hapa nyumbani, ntashangaa kama Bongo movies hazitatumia fursa hii kuelezea maisha na tamaduni za Tanzania . Teknolojia hii itawezesha uzalishaji mkubwa, wataalam wachache, pesa kibao.
- Kusoma mdomo, na kufikia lugha za asili: Natamani ifiwe wakati iwezekane kutengeneza content kwa ajili ya lugha kama vile Kikurya, Kichaga na Kimasai. AI itawezesha hili. Aidha, utaweza kuchukua picha ya mtu, na kuchezesha ulimi wake mpaka kieleweke.
- Matumizi Mabaya: Kizuri huwa na mabaya na madhaifu. Tutaona uzalishaji wa video feki. Kuna video fulani ya Obama inatembea ikisifia Yanga, lakini jamaa hata uwepo wa Yanga haujui.
Kumbuka kisa cha Gwajima. Inaonekana ilitengenezwa. Zamani, ilihitaji mtaalam kwelikweli kufanya kitu kama hicho. Ila siku hizi, ni rahisi tu. Shkamo AI.
- Meseji za kampeni: Ni rahisi kutengeneza na kutuma Meseji za kampeni. hata hivyo, meseji na jumbe hizi zinaweza kutumika vibaya.
- Habari za uongo: Habari za uongo zitatengenezwa na kusambazwa. Habari hizi zitakuwa silaha za vita vya kisiasa. Kutakuwa na haja ya wataalam ndani na nje ya JF kudhibiti habari kama hizi.