bitimkongwe
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 7,794
- 7,551
Kabla ya 1964 alikuwepo Chief Inspector (?) Sultan Ahmed Mugheir ambaye sera zake zililenga zaidi kupendelea Utawala wa Waafrika, kitu ambacho kiliwaudhi Waarabu.
Walijaribu kumuua na kwa bahati nzuri hawakufanikiwa kwa mara ya kwanza ijapokuwa walimjeruhi na alilazwa hospitali na kupewa ulinzi mkali.
Ndipo alipokwenda baba yake Humoud huku ameficha jambia na kuomba akamuone ndugu yake huyo Mugheir. Kwa kuona kwamba alikuwa mtu mzima umri umekwenda walinzi walimruhusu kumwona kumbe masikini ndiyo alikwenda kummaliza kumuua kwa jambia.
Baba yake Humoud alikamatwa na kesi ilipokwenda mahakamani alishinda kesi ile kwa kisingizio kuwa hakuwa na akili timamu.
Baada ya Mapinduzi kesi ilifunguliwa tena (baadhi wanasema alichukuliwa tu) na alihukumiwa kufungwa na wengine wanasema kuuwawa.
Humoud aliapa kwamba angemuua Karume kulipiza kisasi na hata alipokwenda kusomea jeshi Urusi alikuwa akisema hilo.
Inasemekana Karume aliambiwa hilo lakini hakuamini na alimuacha aendelee jeshini.
Ulipotokea mpango wa kumpindua ndipo na yeye alijiunga, ila mpango ulipofeli yeye na Ahmada (na huyu anazo sababu zake) walikwenda Kisiwandui na kutimiza ahadi hiyo.
Inasemekana Humoud alivaa koti refu kumbe ndani ameficha silaha na alipofika tu akammiminia risasi na baadhi wanasema alijiua mwenyewe na wengine aliuawawa na walinzi wake. Yeye na Ahmada na Ali Khatibu Chwaya waliuawa pale Kisiwandui.
Hiyo ilikuwa ni siku ya Ijumaa tarehe 7 April 1972, saa 12 na dakika tano jioni.
Aliyekuwa Chief Inspector Mugheir ni babu yake Edi Riyami kwa baba, ambaye ni maarufu katika siasa za Zanzibar.